sa mdau kibongo bongo mgahawa gani wa kichina mzuri...maana nataka kula point 3 kwa mtoto mmoja nikimpeleka dinner...picha nakua mi ndio starling najifanya najua majina ya kichina ya misosi ka Jack Chen vile.
Ila niambie katika hiyo list uliyotoa kwa hela za madafu hipi expensive hipi kawaida..maana sio unaenda dinner inakucost gharama ya kununua vits
Hahahah!!!
Mkuu vyakula nilivyoweka vyote bei zake ni za kawaida ingawaje hiyo mboga ya mayai na ile ya majani huenda ikawa rahisi zaidi lakini sidhani kama itakuwa ni special meal kwa mtoko kama uutakao.
Sina uzoefu sana na bei za migahawa ya Kichina hapa Dar es Salaam, labda kwa Nairobi au Zanzibar ndio kidogo nina clue.
Kwa uzoefu huo maybe hakikisha uwe na pocket money kuanzia elfu sitini hivi kwa kuwa ni dinner ya watu wawili...(hii bei nimejaribu kufananisha na ile ya Zenji).
Ila huenda ikawa chini ya hapo just give it a try kwa kwenda kuulizia kwanza kabla ya mtoko, ili siku ya mtoko uwe na details za kutosha(kwenye migahawa kuuliza huwa yaruhusiwa).
Kuna "Istana Restaurant" wao huwa na cuisines mbali mbali kama Indian, Malaysian, Chinese. Unaweza kuangalia kupita pale siku ya Jumanne jioni ukacheck maana ndiyo siku wanakuwa na Buffet la Vyakula vya Kichina.
Istana ipo karibu na BMTL Victoria au opposite na Oilcom ya Victoria na bei zao ni very standard.
Pia kuna mgahawa mwingine unaitwa Tangren, upo Mtaa wa Ursino(Mikocheni) karibu kabisa na mgahawa wa "Addis in Dar".
Nimetafuta hii link walau uone walivyo navyo hawa jamaa, pia bei zao ni kawaida ...
Narudi Nyumbani !: Tangren chinese restaurant