Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Umefanya argument yako kisomi hasa. Watu wanapenda sana kupaza sauti lakini ndani ya sauti hizo hakuna content zaidi ya ushabiki.Tusiwe na jazba sana mkuu turuhusu kutofautiana kimawazo.
Nimeshangaa sana kuona watu wanaizungumzia sana report ya CAG ilihali kila mwaka haya yalisemwa kwa intensity zilizotofautiana. Tamisemi haijawahi kuacha kupata hati chafu...mashirika yetu ya umma hayajawahi kujiendesha kwa faida miaka yote iliyodumu. Pengine tatizo ni hivi karibuni hayati kutuaminisha kuwa wanaleta magawio ilhali ukweli si huo(kama CAG alivyoainisha.)
Hilo la juu limenishangaza lakini nikiri wewe umenishangaza zaidi mkuu. Muono wako si tu hauendani na current trend being it economic or political bali hata haugusi kwenye ukweli. Labda nikijibu maswali yako utaelewa.
Umehoji juu ya miradi kuwepo au kutokuwepo....
Nadhani unazungumzia miradi iliyopewa jina ya miradi yakimkakati. well binafsi naomba nikuambie jambo hakuna uongozi uliomaliza awamu yake bila kutekeleza miradi yenye usawia na miradi iliyotekelezwa na awamu ya 5 kwenye nusu ya kwanza ya muhula wake. Mzee kikwete alijenga mara 2 ya kilometa za lami zilizojengwa na awamu hii...View attachment 1748792Source hotuba ya WFM 2021
Labda nikujulishe kuwa unaosema hakuna lolote walilofanya kwenye utendaji wao waliweza kujenga karibu kilometa 10,000 za lami. Nafikiri wasomi wazuri huwa wako objective au labda ulisema ulilosema ukiwa hauyafahamu haya. Likewise kwenye madaraja, masoko, vituo vya mabasi na kadhalika(ikiwa hapa utahitaji maelezo zaidi nitakuja tuzungumzie ya terminal 3, daraja la kigamboni na uwanja wa mkapa vina case inayofannana sana)
Nikiri sijui sana kuhusu meli na ndege. Sitaviongelea
umehoji pia juu ya watoto kusoma bure. Umesoma zama ipi mkuu? Elimu yetu ilikuwa bure miaka mingi sana na baada ya muda ikaja kuwa elimu changizi baina ya wazazi na serikali huku serikali ikibeba jukumu kubwa kwenye kufund elimu(hapa waumini wa elimu bure huwa hawapasemi kabisa) Pengine wewe haujui lakini awamu zilizopita zilijicommit kwenye elimu kuliko awamu unayosema imetoa elimu bure.
awamu ya 3 na ya 4 zilifund shule za kata na kuongeza idadi ya wanafunzi pamoja na walimu kwa karibu mara 2. Tulikuwa na shule za sekondari 1700 tu mwaka 2005, zilifikia zaidi ya 4000 mwaka 2015. Don't tarnish reputations za watu kwa sababu ya kutojua.
Kwenye elimu uliyoitaja sera ya elimu bure haikuwa na lengo. Labda niseme ni mojawapo kati ya sera ambayo ilikuwa more political kuliko kuwa realistic. Labda wewe useme kwanini hakujawa na concurrent policy development kwenye elimu. Tumejenga shule tumtriplicate namba ya wanafunzi tukaweka kipaumbele kwenye uandaaji wa waalimu vyuoni tukawavutia kwa kuwapa mikopo bila kuhoji lakini ghafla sera ikabadilika kuwa kutokutoza 70,000 kwa shule za bweni na 20,000 kwa shule za kata.
Nasema hili kwakuwa shule nyingi michango iko pale pale na hilo liko chini ya wakurugenzi. Tuliandaa sera alafu tukasema lakini mkurugenzi anaweza kuweka kiasi kadhaa.
HAKUNA AWAMU INAYOWEZA KUJUSTIFY WIZI au MATUMIZI MABOVU. Usitetee uovu. Achana na hayo yote concern yangu kubwa ni circus ya ukuaji wa uchumi View attachment 1748805
2021
View attachment 1748807
2016
Sijabahatika kupata taarifa ya 2005 pengine nayo ingetupa somo kubwa pia.
Kwa hakika kabisa ya kweli, tukisema tuweke data hapa za indicators zote za ukuaji wa uchumi na performance ya Serikali, awamu ya 5 haiwezi kufikia hata 25% ya awamu ya 4. Awamu ya 5 iliwekeza sana katika propaganda kuliko uhalisia. Ni katika awamu ya 5, ndiyo wakati pekee tuliposhuhudia kiongozi mkuu akifungua barabara ambazo tayari zilifunguliwa, akifungua viwanda wakati viwanda hivyo vimekuwa kwenye uzalishaji kwa zaidi ya miaka 10. Tulishuhudia kiongozi mkuu akifungua madaraja ya waenda kwa miguu, visima vifupi vya maji vya kupump kwa mikono, masoko, stand, n.k. Yote ikilenga kuwahadaa watu ionekane kuna mengi sana na makubwa yanafanyika kila leo, wakati ni vitu vidogo ambavyo havina hata hadhi ya kufunguliwa na kiongozi mkuu wa Taifa. Na kwa kiasi kikubwa propaganda zile zilifanikiwa, wengine mpaka leo hii wanaamini kulifanyika mambo makubwa mazuri ya ajabu kipindi cha awamu ya 5 kuliko awamu zote zilizotangulia.
Kama laiti baada ya awamu ya 4, ingeingia awamu yenye vision sahihi, uongozi na usimamizi mzuri, hakika sahizi tungekuwa tunaongelea Tanzania yenye wastani wa mapato ya wananchi si chini ya $1,500. Ukuaji wa uwekezaji ungekuwa si chini ya 25% ambao ungepunguza sana tatizo la ajira kwa vijana wetu. Thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo, ambayo yameanguka kwa zaidi ya 50% yangekuwa yamepanda na kuboresha maisha ya wakulima kuliko ilivyo sasa.
Kwa sababu tumerudi nyuma kwenye maeneo mengi, Mh. Rais Samia ni lazima afanye kazi ya ziada ya kuwaongoza watanzania ili kurekebisha haraka maeneo ambayo nchi ilikuwa inarudi nyima badala ya kwenda mbele.