Chini ya utawala wa Magufuli, Taifa limepata hasara ya mabilioni na pia upotevu mkubwa wa fedha uliozua utata

Chini ya utawala wa Magufuli, Taifa limepata hasara ya mabilioni na pia upotevu mkubwa wa fedha uliozua utata

Tusiwe na jazba sana mkuu turuhusu kutofautiana kimawazo.

Nimeshangaa sana kuona watu wanaizungumzia sana report ya CAG ilihali kila mwaka haya yalisemwa kwa intensity zilizotofautiana. Tamisemi haijawahi kuacha kupata hati chafu...mashirika yetu ya umma hayajawahi kujiendesha kwa faida miaka yote iliyodumu. Pengine tatizo ni hivi karibuni hayati kutuaminisha kuwa wanaleta magawio ilhali ukweli si huo(kama CAG alivyoainisha.)

Hilo la juu limenishangaza lakini nikiri wewe umenishangaza zaidi mkuu. Muono wako si tu hauendani na current trend being it economic or political bali hata haugusi kwenye ukweli. Labda nikijibu maswali yako utaelewa.

Umehoji juu ya miradi kuwepo au kutokuwepo....
Nadhani unazungumzia miradi iliyopewa jina ya miradi yakimkakati. well binafsi naomba nikuambie jambo hakuna uongozi uliomaliza awamu yake bila kutekeleza miradi yenye usawia na miradi iliyotekelezwa na awamu ya 5 kwenye nusu ya kwanza ya muhula wake. Mzee kikwete alijenga mara 2 ya kilometa za lami zilizojengwa na awamu hii...View attachment 1748792Source hotuba ya WFM 2021
Labda nikujulishe kuwa unaosema hakuna lolote walilofanya kwenye utendaji wao waliweza kujenga karibu kilometa 10,000 za lami. Nafikiri wasomi wazuri huwa wako objective au labda ulisema ulilosema ukiwa hauyafahamu haya. Likewise kwenye madaraja, masoko, vituo vya mabasi na kadhalika(ikiwa hapa utahitaji maelezo zaidi nitakuja tuzungumzie ya terminal 3, daraja la kigamboni na uwanja wa mkapa vina case inayofannana sana)

Nikiri sijui sana kuhusu meli na ndege. Sitaviongelea

umehoji pia juu ya watoto kusoma bure. Umesoma zama ipi mkuu? Elimu yetu ilikuwa bure miaka mingi sana na baada ya muda ikaja kuwa elimu changizi baina ya wazazi na serikali huku serikali ikibeba jukumu kubwa kwenye kufund elimu(hapa waumini wa elimu bure huwa hawapasemi kabisa) Pengine wewe haujui lakini awamu zilizopita zilijicommit kwenye elimu kuliko awamu unayosema imetoa elimu bure.

awamu ya 3 na ya 4 zilifund shule za kata na kuongeza idadi ya wanafunzi pamoja na walimu kwa karibu mara 2. Tulikuwa na shule za sekondari 1700 tu mwaka 2005, zilifikia zaidi ya 4000 mwaka 2015. Don't tarnish reputations za watu kwa sababu ya kutojua.

Kwenye elimu uliyoitaja sera ya elimu bure haikuwa na lengo. Labda niseme ni mojawapo kati ya sera ambayo ilikuwa more political kuliko kuwa realistic. Labda wewe useme kwanini hakujawa na concurrent policy development kwenye elimu. Tumejenga shule tumtriplicate namba ya wanafunzi tukaweka kipaumbele kwenye uandaaji wa waalimu vyuoni tukawavutia kwa kuwapa mikopo bila kuhoji lakini ghafla sera ikabadilika kuwa kutokutoza 70,000 kwa shule za bweni na 20,000 kwa shule za kata.

Nasema hili kwakuwa shule nyingi michango iko pale pale na hilo liko chini ya wakurugenzi. Tuliandaa sera alafu tukasema lakini mkurugenzi anaweza kuweka kiasi kadhaa.

HAKUNA AWAMU INAYOWEZA KUJUSTIFY WIZI au MATUMIZI MABOVU. Usitetee uovu. Achana na hayo yote concern yangu kubwa ni circus ya ukuaji wa uchumi View attachment 1748805
2021
View attachment 1748807
2016
Sijabahatika kupata taarifa ya 2005 pengine nayo ingetupa somo kubwa pia.
Umefanya argument yako kisomi hasa. Watu wanapenda sana kupaza sauti lakini ndani ya sauti hizo hakuna content zaidi ya ushabiki.

Kwa hakika kabisa ya kweli, tukisema tuweke data hapa za indicators zote za ukuaji wa uchumi na performance ya Serikali, awamu ya 5 haiwezi kufikia hata 25% ya awamu ya 4. Awamu ya 5 iliwekeza sana katika propaganda kuliko uhalisia. Ni katika awamu ya 5, ndiyo wakati pekee tuliposhuhudia kiongozi mkuu akifungua barabara ambazo tayari zilifunguliwa, akifungua viwanda wakati viwanda hivyo vimekuwa kwenye uzalishaji kwa zaidi ya miaka 10. Tulishuhudia kiongozi mkuu akifungua madaraja ya waenda kwa miguu, visima vifupi vya maji vya kupump kwa mikono, masoko, stand, n.k. Yote ikilenga kuwahadaa watu ionekane kuna mengi sana na makubwa yanafanyika kila leo, wakati ni vitu vidogo ambavyo havina hata hadhi ya kufunguliwa na kiongozi mkuu wa Taifa. Na kwa kiasi kikubwa propaganda zile zilifanikiwa, wengine mpaka leo hii wanaamini kulifanyika mambo makubwa mazuri ya ajabu kipindi cha awamu ya 5 kuliko awamu zote zilizotangulia.

Kama laiti baada ya awamu ya 4, ingeingia awamu yenye vision sahihi, uongozi na usimamizi mzuri, hakika sahizi tungekuwa tunaongelea Tanzania yenye wastani wa mapato ya wananchi si chini ya $1,500. Ukuaji wa uwekezaji ungekuwa si chini ya 25% ambao ungepunguza sana tatizo la ajira kwa vijana wetu. Thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo, ambayo yameanguka kwa zaidi ya 50% yangekuwa yamepanda na kuboresha maisha ya wakulima kuliko ilivyo sasa.

Kwa sababu tumerudi nyuma kwenye maeneo mengi, Mh. Rais Samia ni lazima afanye kazi ya ziada ya kuwaongoza watanzania ili kurekebisha haraka maeneo ambayo nchi ilikuwa inarudi nyima badala ya kwenda mbele.
 
Hasara na upotevu huu unaotokana na taarifa za CAG ambapo wanasiasa waliochambua report ya CAG aliepita,Prof. Assad, waliibua utata wa matumizi ya shilling ya shilling trilioni 1.5 na hii ya hivi karibuni inatueleza hasara ya billion 150 katika uendeshaji wa ATCL.

Hasara na upotevu huu uliotokea chini ya utawala wa Magufuli, ni mbali na mamilion na mabilioni mengine yaliyopotea katika sekta za utalii, n.k kama inyoonyeshwa katika report ya CAG ya mwaka huu.

Bado hasara zinazotokana na serikali kufunguliwa makesi katika mahakama za usuluhishi za kimataifa bila kusahau hasara zilizotokana na siasa za hovyo za watu kujiuzulu kwa hoja ya kuunga mkono juhudi na kuliingiza Taifa gharama kubwa za mamilion kugharamia chaguzi ndogo.

Kwa kifupi, katika awamu ya Magufuli, Taifa limepata hasara kubwa Katika baadhi ya maeneo na pia kuna fedha nyingi zimetumika na kuacha utata mtupu kama hayo matumizi ya shilingi trilioni moja yaliyohojiwa na wabunge wa upinzani baada ya kuichambu report ya CAG aliepita(Prof.Assad).

Itakuwa ni jambo jema Bunge kuunda kamati teule kuchunguza utata wa matumizi haya ya shilingi trilioni 1.5 ili umma ujue ukweli ni upi na si hizi kelele za MATAGA kutaka kutuaminisha kuwa ufisadi ulidhibitiwa enzi za Hayati Magufuli tofauti na awamu zilizopita.

Kama hamtaki kuchunguza tuhuma hizi, acheni kumlinganisha Magufuli na watangulizi wake, hasa Kikwete, ambae wakati wake Bunge liliweze kuunda kamati teule na kuchunguza tuhuma zinazoihusu serikali, na pia vyombo vya habari viliweza kuanika kashifa mbalimbali za serikali bila kusahau Whistleblowers (kina Tumbili) waliweza kuanika madudu yaliyokuwa yanaendelea serikalini tofauti kabisa na ilivyokuwa wakati wa Magufuli .
Mgonjwa wa akili ww.....
kila siku ukilala ukiamka unamuwaza Magu....
itakuwa alikutairi kwa msumeno butu....
now you are crying like a little baby
 
Watu mnasemea barabara wakat wa kikwete..mnashindwa kujua kwamba hizo barabara aliekuwa anazisimamia zijengwe ni huyo huyo mnaemsimanga leo..kama sio yeye aliesimamia hyo miradi ya barabara nazan muda huu msingekuwa na lakusema..mnasema kikwete kajenga barabara nyingi..magufuli akiwa mtendaji mkuu..alaf hakuna kingine kilichofanyika pas na barabara wizara zingine zilikuwa zinaiba tuu pesa..
Labda nikuelimishe kidogo mkuu.

Pengine itakuwia sawia iwapo utataja mradi mmoja wa hayati magufuli alafu mimi nitataja mradi uliofanywa na mzee Kikwete nitafanya hivyo huku nikijustify wapi mradi ulipotokea(either kwenye mipango ya maendeleo(FYDP 1, MKUKUTA ama sera iliyokuwa inatekelezwa na sekta husika) I wont trouble you with such formality naelewa how shabby the regime you stamp upon ilivyokuwa. Just name any and I will name and elaborate many.
 
Hizo ndege ulizzotaja kwenye orodha yako unajua zimesababisha hasara ya sh ngapi mpaka sasa?. Au unaropoka tu
Angalia akili fupi hii
mashirika makubwa makongwe yote yamepata hasara......
angalia data za Ethiopian Airlines angalia Kenya airways.....
next time nukileta ujinga kama huu tunakuozesha uolewe bila mahari
 
Jiwe alikuwa hajui tofauti ya mikopo na pesa zetu za ndani.Kwake vyote viwili ni kitu kimoja!
Acha matani trillion 18 miaka 5 ? Mbona tuliambiwa tunajenga miradi kwa pesa zetu za ndani cash kumbe mikopo.

Qmmke nilisha sema usiamini mwana siasa,
 
MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!!

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!!

2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM!!

3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.

4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.

5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.

6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!

7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!!

8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga!!

9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!!

10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye. Tutakua Taifa la kijimga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga, wavivu
wasio na lolote walioachiwa Nchi wasiongoze wakihangaika na umbea, udaku na ushambenga.
Kwa taarifa yenu #SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE!! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.
#TutakukumbukaDaimaJPM.
MenukaJr,
Da'slam-Tanzania.
Huu ushabiki sasa.
Jiongelee nafsi yako sisi wengine tunaona alizingua
 
Angalia akili fupi hii
mashirika makubwa makongwe yote yamepata hasara......
angalia data za Ethiopian Airlines angalia Kenya airways.....
next time nukileta ujinga kama huu tunakuozesha uolewe bila mahari

Watu ni mabwege sana, yani hata kusoma hawataki. CAG kaonyesha kabisa kwenye ripoti yake wapi penye kulitia shirika hasara na sio ununuzi wa ndege lakini wanavyoshabikia humu mpaka nashangaa.
Umaskini wa akili ni mbaya kuliko umaskini wowote ule
 
Hasara na upotevu huu unaotokana na taarifa za CAG ambapo wanasiasa waliochambua report ya CAG aliepita,Prof. Assad, waliibua utata wa matumizi ya shilling ya shilling trilioni 1.5 na hii ya hivi karibuni inatueleza hasara ya billion 150 katika uendeshaji wa ATCL.

Hasara na upotevu huu uliotokea chini ya utawala wa Magufuli, ni mbali na mamilion na mabilioni mengine yaliyopotea katika sekta za utalii, n.k kama inyoonyeshwa katika report ya CAG ya mwaka huu.

Bado hasara zinazotokana na serikali kufunguliwa makesi katika mahakama za usuluhishi za kimataifa bila kusahau hasara zilizotokana na siasa za hovyo za watu kujiuzulu kwa hoja ya kuunga mkono juhudi na kuliingiza Taifa gharama kubwa za mamilion kugharamia chaguzi ndogo.

Kwa kifupi, katika awamu ya Magufuli, Taifa limepata hasara kubwa Katika baadhi ya maeneo na pia kuna fedha nyingi zimetumika na kuacha utata mtupu kama hayo matumizi ya shilingi trilioni moja yaliyohojiwa na wabunge wa upinzani baada ya kuichambu report ya CAG aliepita(Prof.Assad).

Itakuwa ni jambo jema Bunge kuunda kamati teule kuchunguza utata wa matumizi haya ya shilingi trilioni 1.5 ili umma ujue ukweli ni upi na si hizi kelele za MATAGA kutaka kutuaminisha kuwa ufisadi ulidhibitiwa enzi za Hayati Magufuli tofauti na awamu zilizopita.

Kama hamtaki kuchunguza tuhuma hizi, acheni kumlinganisha Magufuli na watangulizi wake, hasa Kikwete, ambae wakati wake Bunge liliweze kuunda kamati teule na kuchunguza tuhuma zinazoihusu serikali, na pia vyombo vya habari viliweza kuanika kashifa mbalimbali za serikali bila kusahau Whistleblowers (kina Tumbili) waliweza kuanika madudu yaliyokuwa yanaendelea serikalini tofauti kabisa na ilivyokuwa wakati wa Magufuli .
Hoja zako ni nzuri ingawa zinaegemea upande mmoja. Hivi kwanini mijadala yetu ni lazima tutoe mfano wa Magufuli na Kikwete tu. Hasara na upotevu wa fedha upo tawala zote bila kubagua ndiyo kazi ya CAG kudhibiti mianya hiyo. Hoja za CAG zimetutoa relini tunashindwa hata kuangalia mambo mengine ya maendeleo. Watu wanaonyesha unafiki wao hadharani. Watu wenye dhamana wamepoteza utu wao kwa kutaka waonekane wanaunga mkono utawala uliopo. Wamekula posho kuongozana na marehemu leo wamekaa na kujifanya wako tofauti. Wanafiki wanaleta hasira sana.
Viongozi wa juu wa CCM msipokaa sawa ilani haitatekelezwa na hili litakua anguko la kishindo kwenu. Chama kimelegea kama vile damu imeganda na Astra Zeneca. Tunataka kurudishwa bandari ya Bagamoyo looooooo. CCM angalieni mnaanza kupoteza dira na muelekeo. Chama kikichagua KM dhaifu na mlegevu basi mmekwisha. Rudisheni Bashiru na uenyekiti abaki Mangula kwanza mtajuta na matalia mkiacha uenyekiti uende upande ule.
 
Stupid! Cooked stories from same people. Tunajua Chadema mliumia na mengi ila hapa hatutoangalia sura bali nani anasimama na ukweli bila hila. Mtaelewa baadae ...
Kwani Chadema ndiyo walimuweka hapo huyo CAG? Kwani Chadema ndiyo wamewatuma nyie maccm muwe majizi na mafisadi?
 
Mtu msafi smart civilized educated katu hawezi kuwa na ukali, hasira,chuki visasi roho mbaya hizi tabia za uncivilized people.
 
Ni bora hii hasara lakini watoto wetu wanasoma bure, barabara zimejengwa, tuna umeme hadi vijijini, madaraja yamejengwa, kuliko kipindi kile cha mzee wa msoga
We hujui mambo makubwa aliyofanya Mzee Wa msoga,mwendokasi,daraja LA kigamboni,shule zote za kata,barabara zilizounganisha nchi nk,
Umeme Wa rea ulianza kipindi cha kikwete hela hizo za Umeme vijijini ni kwa msaada Wa watu Wa marekani,na watu waishio mjini ukinunua luku kuna %unakatwa kulipia gharama za kupeleka Umeme vijjjini rea.
Hiii bhaghoshaa mnampamba sana mwendazake.
 
Hasara na upotevu huu unaotokana na taarifa za CAG ambapo wanasiasa waliochambua report ya CAG aliepita,Prof. Assad, waliibua utata wa matumizi ya shilling ya shilling trilioni 1.5 na hii ya hivi karibuni inatueleza hasara ya billion 150 katika uendeshaji wa ATCL.

Hasara na upotevu huu uliotokea chini ya utawala wa Magufuli, ni mbali na mamilion na mabilioni mengine yaliyopotea katika sekta za utalii, n.k kama inyoonyeshwa katika report ya CAG ya mwaka huu.

Bado hasara zinazotokana na serikali kufunguliwa makesi katika mahakama za usuluhishi za kimataifa bila kusahau hasara zilizotokana na siasa za hovyo za watu kujiuzulu kwa hoja ya kuunga mkono juhudi na kuliingiza Taifa gharama kubwa za mamilion kugharamia chaguzi ndogo.

Kwa kifupi, katika awamu ya Magufuli, Taifa limepata hasara kubwa Katika baadhi ya maeneo na pia kuna fedha nyingi zimetumika na kuacha utata mtupu kama hayo matumizi ya shilingi trilioni moja yaliyohojiwa na wabunge wa upinzani baada ya kuichambu report ya CAG aliepita(Prof.Assad).

Itakuwa ni jambo jema Bunge kuunda kamati teule kuchunguza utata wa matumizi haya ya shilingi trilioni 1.5 ili umma ujue ukweli ni upi na si hizi kelele za MATAGA kutaka kutuaminisha kuwa ufisadi ulidhibitiwa enzi za Hayati Magufuli tofauti na awamu zilizopita.

Kama hamtaki kuchunguza tuhuma hizi, acheni kumlinganisha Magufuli na watangulizi wake, hasa Kikwete, ambae wakati wake Bunge liliweze kuunda kamati teule na kuchunguza tuhuma zinazoihusu serikali, na pia vyombo vya habari viliweza kuanika kashifa mbalimbali za serikali bila kusahau Whistleblowers (kina Tumbili) waliweza kuanika madudu yaliyokuwa yanaendelea serikalini tofauti kabisa na ilivyokuwa wakati wa Magufuli .
Da aibu sn
 
We hujui mambo makubwa aliyofanya Mzee Wa msoga,mwendokasi,daraja LA kigamboni,shule zote za kata,barabara zilizounganisha nchi nk,
Umeme Wa rea ulianza kipindi cha kikwete hela hizo za Umeme vijijini ni kwa msaada Wa watu Wa marekani,na watu waishio mjini ukinunua luku kuna %unakatwa kulipia gharama za kupeleka Umeme vijjjini rea.
Hiii bhaghoshaa mnampamba sana mwendazake.
Udom, ESAMI, chuo cha mipango, B.Mkapa hosp, JKCI, MOI n.k
 
We Kenge..umesahau EPA, ESCROW, IPTL, TWIGA, GAS ILIOUZWA WA WACHINA, WATUMISH HEWA, DAWA ZA KULEVYA, RICHMOND.
Kaa kimya..leo tunaona madaraja, flyover, meli zilizonunuliwa, ukarabati wa shule kongwe, viwanja vya ndege, ndege 11..watoto wamasoma buree..
Wakat hizo pesa za escrow zilipopigwaa hayo yote hayakuwepo.
Kaa kimyaa nyau kabisaa ww..
Baambie baelewe! Hizi nyang'au zinakera sana
 
Back
Top Bottom