n00b
Platinum Member
- Apr 10, 2008
- 1,031
- 2,741
Kama mnavyojua, linapokuja suala la miradi mikubwa ya miundombinu (mega projects) katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki, mambo huwa hayaishi vituko. Baada ya kelele nyingi, migomo ya wafanyakazi, na kesi mahakamani zilizopelekea kufutwa kwa ule mkataba tata wa uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) uliotaka kupewa Kampuni ya Adani kutoka India, sasa "JIRANI" ameingia kwenye mkenge mwingine!
Serikali ya Kenya imetangaza kuwapa Wachina dili la Dola Bilioni 2.9 (sawa na takribani Shilingi za Kitanzania Trilioni 7.6) kufanya upanuzi mkubwa wa uwanja huo wa JKIA.
Lakini sasa, hapa ndipo mjadala mkubwa unapoibuka. Katika dili hili, kampuni kubwa ya Serikali ya China, China Communications Construction Company (CCCC) ikishirikiana na China Road and Bridge Corporation (CRBC)— hawapo peke yao. Wameshirikiana na kampuni inayoitwa IMC Construction Kenya.
Ni nani mmiliki wa IMC Construction? Ni yule bwana mdogo "bilionea kijana", mfanyabiashara tata na wanasiasa, na mtu wa misifa mingi kutoka Zimbabwe, Sir Wicknell Chivayo!
Je, hapa tunaona "Ufisadi wa Kimitandao ya Kinafasi" (Crony Capitalism) ukivuka mipaka? Inakuwaje kampuni ya mfanyabiashara tata kutoka Zimbabwe ambaye amekuwa akituhumiwa kwa kashfa mbalimbali za zabuni kule kwao (kama mradi wa jua wa Gwanda), apate shavu la mabilioni ya dola Kenya kwa mradi wa kimkakati kama JKIA? Wachina wamemtumia kama "daraja" la kisiasa kuingia nchini Kenya?
Je, uamuzi wa Rais William Ruto kufuta dili la Adani na kukimbilia kwa Wachina ulikuwa ni wa kizalendo kweli, au ni mbinu tu ya "kubadili wapigaji" (from India to China/Zimbabwe)? Mbona bei ya mkataba huu mpya imepaa sana ikilinganishwa na ule wa kwanza?
Ushindani wa Viwanja vya Ndege EAC: Wakati Kenya wakiongeza nguvu JKIA kwa $2.9B, Rwanda wanajenga Bugesera mpya kwa kushirikiana na Qatar Airways, na Ethiopia wakijenga uwanja mkubwa zaidi kule Bishoftu utakaobeba abiria milioni 110, sisi Tanzania tunasimama wapi na uwanja wetu wa JNIA (Julius Nyerere International Airport)? Je, ukarabati wetu unatosha kupambana na hawa majirani zetu?
Ni hayo kwa leo, karibu kwa mjadala!
Source: Wicknell Chivayo company, Chinese partner win $2.9 billion Kenya airport tender

Mambo Muhimu ya Kufahamu Kuhusu Dili Hili:
- Gharama Imepaa Kuliko ya Adani: Kumbukeni Adani walitaka kufanya ukarabati huu kwa Dola Bilioni 1.85 hadi Bilioni 2.0. Sasa Wachina wakishirikiana na Chivayo wamechukua tenda ile ile kwa Dola Bilioni 2.9! Hii ni karibu ongezeko la 50% ya bei ya awali. Wachambuzi wa mambo Kenya tayari wanauliza: Kama Adani alikataliwa kwa sababu ya kutaka kuinyonya nchi, mbona hawa wa sasa wanatupiga bei kubwa zaidi?
- Chivayo na Uhusiano wake na TZ: Huyu Wicknell Chivayo si mgeni sana katika masuala ya miradi ya kifedha. Hapa kwetu Tanzania, kupitia kampuni yake hiyo hiyo ya IMC Construction, anatajwa kuhusika katika ujenzi wa hoteli mbili za kifahari za nyota tano (Five-Star Hotels) katika hifadhi za Serengeti na Ngorongoro kwa mradi wenye thamani ya Dola Milioni 200. Huyu jamaa ni swahiba wa karibu sana wa Marais na viongozi wakuu wa nchi mbalimbali za SADC na EAC (akiwemo Rais Mnangagwa wa Zimbabwe na Ruto wa Kenya).
- Upanuzi Unahusisha Nini? Mradi huu unatarajia kuongeza uwezo wa JKIA kuhudumia abiria milioni 15 kwa mwaka (kwa sasa unazidiwa uwezo ukiwa na abiria milioni 8.8). Pia, unahusisha ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal) na barabara ya pili ya kurukia ndege (Runway) inayotarajiwa kukamilika mwaka 2029, ambayo itaongeza kasi ya kutua na kuruka kwa ndege kutoka 14 kwa saa hadi 63 kwa saa.
- Wapi Pesa Inatoka? Kenya itachangia Dola Bilioni 1.3 kutoka kwenye Mfuko mpya wa Miundombinu (National Infrastructure Fund), na kiasi kilichobaki kitafadhiliwa kwa mikopo ya kibiashara kutoka benki za ndani na zile za nchini China.