CHLOROFORM: Dawa ya usingizi inayotumiwa na wezi kuwapulizia watu kabla ya kuiba

Kwa muda mrefu kumekithiri vitendo vya uhalifu unaohusisha wezi kuingia kwenye nyumba za watu nyakati za usiku na kuwapulizia dawa ya usingizi na kisha kuchukua chochote wanachokitaka ndani ya nyumba.

Baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha aina hiyo ya uhalifu na ushirikina lakini ukweli ni kwamba ipo dawa mojawapo ya usingizi ambayo hutumiwa na wezi wengi kutekeleza uhalifu huo. Dawa hiyo kitaalamu inaitwa CHLOROFORM.

Dawa hiyo ina uwezo wa kumlegeza au kumzimisha mtu kiasi kwamba ashindwe kujitambua na kuhisi chochote na wahalifu wakafanya chochote wanachoweza kwa muda wa kutosha. Wataalamu wa afya huitumia katika shughuli za kitabibu hasa wakati wa upasuaji.

Madhara ya Chloroform kwa binadamu huongezeka sambamba na kiwango cha dozi yake. Wakati kiwango kidogo kinasababisha kutojielewa, kadri dozi inavyoongezeka huweza kukufanya uzimie kabisa au usisikie mguso wowote. Kwa kiwango kikubwa zaidi huweza kusababisha upumuaji wa shida, misuli ya mwili kutulia kabisa, misuli ya kifua kupooza na mwishowe kupelekea kifo.

Inahitajika tahadhari kubwa hasa kwa wasambazaji wa dawa hii ambayo imekuwa ikileta hasara kwa mali za watu kuibiwa katika nyumba zao nyakati za usiku.
What I can suggest watu walale feni zikiwa zinazunguka, labda hii inaweza kusaidia kwa kiasi fulani
 
Hii tulikuwa tunatumia kulaza panya na chura kwenye practical za biology A-level
"" Ripoti ya vyanzo vya habari kutoka nchini Uganda zinasema kuna baadhi ya maeneo nchini humo watu wanaomiliki mabucha wamekuwa na tabia ya kutumia dawa ya kuhifadhia maiti aina ya chloroform kwa kuhifadhia nyama iliyobaki ili isioze""
 
Kwa muda mrefu kumekithiri vitendo vya uhalifu unaohusisha wezi kuingia kwenye nyumba za watu nyakati za usiku na kuwapulizia dawa ya usingizi na kisha kuchukua chochote wanachokitaka ndani ya nyumba.

Baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha aina hiyo ya uhalifu na ushirikina lakini ukweli ni kwamba ipo dawa mojawapo ya usingizi ambayo hutumiwa na wezi wengi kutekeleza uhalifu huo. Dawa hiyo kitaalamu inaitwa CHLOROFORM.

Dawa hiyo ina uwezo wa kumlegeza au kumzimisha mtu kiasi kwamba ashindwe kujitambua na kuhisi chochote na wahalifu wakafanya chochote wanachoweza kwa muda wa kutosha. Wataalamu wa afya huitumia katika shughuli za kitabibu hasa wakati wa upasuaji.

Madhara ya Chloroform kwa binadamu huongezeka sambamba na kiwango cha dozi yake. Wakati kiwango kidogo kinasababisha kutojielewa, kadri dozi inavyoongezeka huweza kukufanya uzimie kabisa au usisikie mguso wowote. Kwa kiwango kikubwa zaidi huweza kusababisha upumuaji wa shida, misuli ya mwili kutulia kabisa, misuli ya kifua kupooza na mwishowe kupelekea kifo.

Inahitajika tahadhari kubwa hasa kwa wasambazaji wa dawa hii ambayo imekuwa ikileta hasara kwa mali za watu kuibiwa katika nyumba zao nyakati za usiku.
"wataalamu wa afya huitumia kitabibu..."

Si, kweli Kwa sasa as ni toxic substance as inaweza kusababisha kifo due to Cardiac arrthymiasis!

Ilitumika zamani kama anarthetic substance but Siku hizi zinatumika Dawa nyingine Bora kama Pancuronium, Propofol, Atraculium, Halothane, Esoflurane, Nitrous Oxide nk.
 
"" Ripoti ya vyanzo vya habari kutoka nchini Uganda zinasema kuna baadhi ya maeneo nchini humo watu wanaomiliki mabucha wamekuwa na tabia ya kutumia dawa ya kuhifadhia maiti aina ya chloroform kwa kuhifadhia nyama iliyobaki ili isioze""
Hao ni laymen, wanaweza wasielewe kwa usahihi dawa inayotumiwa kuhifadhi maiti ndo wakakurupuka na hilo jina chloroform. Usiwaamini sana waandishi wa kiafrika hawana muda wa kufanya consultation kwa wataalamu kupata habari sahihi, kila kitu wanajua
 
Itakua inafosi kuingiza hewa puani,gues nini kitatokea.
Kuna watu wanalala na feni throughout hasa kipindi cha joto na hawajapata shida yoyote kwenye mapafu wala upumuaji
 
Mkuu me niki lala na fen huwa ina nichosha Sana mwili!
 
Umenikumbusha siku niliyo jaribu kunusa hiyo spiriti aiseee niliona dunia yote inataka kuniangukia upside down nilipokuwa maabara ya chemistry sekondari school*********
 
Kama ni hivyo basi tuliwahi kupuliziwa home, tuliamka saa3 asubuhi tukiwa wachovu hatari sebule nyeupeee na ubwabwa ulobaki wakala, wakabeba na mikate.
Hahaha yaan wezi wanadharau sana. Kuna mmoja walimuibiaga ng'ombe wakamchinja hapo hapo, wakachuna wakasepa na nyama wakamuachia ngozi, makwato na mavi ya ng'ombe
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Inatia hasira.
Hahaha yaan wezi wanadharau sana. Kuna mmoja walimuibiaga ng'ombe wakamchinja hapo hapo, wakachuna wakasepa na nyama wakamuachia ngozi, makwato na mavi ya ng'ombe
 
Madaktari waje hapa!!,chloroform siyo dawa ya kuhifadhi maiti kweli nahisi UONGO MKALI UKO HAPA.
Kwa hiyo wewe unafikiri ina kazi moja tu, hiyo ya kuhifashia maiti? Jaribu kujipaka kwenye mkono wako uone kama hujapata ganzi ya kufa mtu!!
 
Back
Top Bottom