May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Hapa karibuni kumekuwa na mjadala kuhusu matumizi ya dawa zitumikazo kuhifadhia maiti kwenye kuhifadhia Samaki.
Hivi ni lipi jipya hapa? na ni nani tunajaribu kumtetea, Huyu huyu Mtanzania Mfanya biashara anayejali yeye kupata hata kama wengine mnakufa?.
Sanasana labda tuhamaki kwa kuwa hili kutamkwa na Mtu mwenye wadhfa wa Makamu wa raisi ni imetumika spika kubwa sana, ila kiukweli hakuna jipya ambalo hatujawahi kusikia kabla....Sasa tujiulize ni lini Mtanzania umechukua tahadhari?.
Na sidhani kama ni Samaki tu kwani kulishakuja pia taarifa kuhusu dawa hizo pia kutumika kuhifadhia nyama za Ng'ombe n.k.
Kinachonishangaza leo hii ni namna Watanzania wanavyohamanika kusema kwamba hili limewashtua saana na kuwashangaza. Hivi ni lini Watanzania hawa ninaowafahamu mimi wamekuwa ni watu wa kujali hatari za kiafya zinazowazunguka?.
Hivi hata kama sio hizo chloroform ni kwa kiasi gani tunanunua Samaki wanaokaangwa na mafuta machafu Mitaani kwetu?. Unafika au unapita kwa Mama mkaanga Samaki utafikiri anatumia matope au oili chafu...na bado tunanunua tena unakuta foleni ya Wateja wakigombea....achilia mbali zile taarifa kwamba wapo wanaotumia mafuta ya transfoma.
Kwa hiyo kwa mfano leo hii Makamu wa Raisi akisema Watu waache kuuzia wenzao mishikaki ya nyama za Mbwa na Paka tutashika tena midomo na kutoa macho kwa mshangao? Wanafiki kweli sisi...hivi hapo ni lipi jipya hatujasikia?. ni mara ngapi tumeona hata kwenye vyombo vya habari au mitandaoni watu wanaokamatwa red handed wakiwa wanachinja au wamechinja na wanaonesha mabaki ya Mbwa au Paka?....hivi tunachukua tahadhari yoyoyte zaidi ya kuona kushamiri kwa wachoma mishikaki kila kona ya jiji?.
Juzijuzi hapa nilikuwa kwa Fundi Seremala mmoja, jirani yake Mwenzake alikuwa anapiga rangi akitumia mashine ya ku spray, ile harufu tu ya rangi inatosha kukwambia kuwa hii kitu si rafiki wa afya haswa kama itapenya mwilini...Watanzania wasivyopenda kuhojiwa mambo hayo...baadae nikaamua tu kumuuliza "hivi kwa nini usijifunge hata kitambaa cha mia tano mdomoni na puani hiyo kitu sio nzuri" kama nilivyotarajia yule Bw aliniangalia tu, ni kama vile alijizuia kunijibu vibaya au kunitukana kisha akaendelea na alichokuwa anakifanya...sikushangaa maana hata angenitukana hicho ndio nilichokuwa nakitarajia.
Tuache unafiki Watanzania, sisi ni kati ya Jamii tusiojali kabisa kuchukua tahadhari kwa mambo yanayohusu afya zetu wenyewe, na Wafanya biashara nao wana take advantage ya udhaifu huo kufanya watakavyo ali mradi wao wapate riziki zao.
Na Serikali iendeleze elimu kwa Wananchi wake, hao Mabwana na Mabibi lishe kazi zao ni nini?...hatusemi mkafunge biashara za Watu la hasha...lakini mhakikishe Jamii wana uwezo wa kuhoji usalama wa anachotaka kutumia kama chakula kabla ya kununua na kwenda kutumia.