Chochote kizuri nikimhusisha mama kinakufa

Chochote kizuri nikimhusisha mama kinakufa

Kuna wazazi wanajisemea kimyakimya "kaniambia,kanifanyia, nikimuambia hivi hataki eeeh ngoja nione atafika wapi".
Wengine anatamani pato lako apangie yeye. Akikuona umevaa nguo nzuri yeye hana roho inamuuma anakulaani kimyakimya. Mfano unamwmbia unajenga wakati alitamani uwape na wao hela wale vizuri, wavae vizuri, wajenge nyumba nzuri wao kwanza HUTOBOI. Wanakuwa tu hawakuombei mema.
 
Kuna ule msemo unasema hakuna kama mama kila nikiutafakari naona kuna watu wana bahati sana,lkn kuna sisi wengine tunapitia machungu sana kwa mama zetu na inakuwa ni siri tu unaitunza moyoni bila kumwambia mtu yeyote!,yaani hadi inafika kipindi unajiuliza huyu ni mama yangu kweli!?
Kwa hakika na tunayopitia hayo ndio tunaweza kukuelewa
 
Kwa iman ya kiislam Kuna aya moja inasema "wa min shari hasidin idhaa hasad" hii binadam huwa tunamuomba Mungu na ina maana ya "Na unikinge na shari ya hasidi anapo husudu"

Hasad siyo uchawi ila Kuna watu tu wameumbwa akiangalia hata mtoto bas huyo mtoto ataumwa sana, kila atakacho shiriki ni lazima kitaharibika na kwa bahari mbaya watu hawa huwa hawajijui Kama wana hasad inaweza ikawachukua muda mrefu sana wakaja kugundua hata uzeeni.

Nakumbuka nina ndugu yangu ilikua kila akienda kijijin kumsalimia bibi akimpokea lazima amtemee mate na siku ya kuondoka hivyo hivyo siku moja akamuuliza kwann? alificha Ila baadae akamwambie hiyo ni Kinga maana mimi nina jicho la hasad naweza nikaangalia kitu kwa upendo ila kitu hicho kikaharibika, kwahiyo mate yangu ni baraka nakupa ili mambo yawe mazuri, hivyo hivyo hata mimi ninetemewa mate sana na wazee
 
MAMA YAKO NI MCHAWI.

wachawi Wana kawaida ya kuwapenda watoto wao wale wajinga jinga mazobaa ,mapoyoyo ,kula kulala...

Wachawi wanakawaida ya KUUA HATA WATOTO WAO WALE WELEVU ,WENYE MAFANIKIO .

KWAKUA HAMNA MCHAWI MWENYE MAFANIKIO, BASI HATA WEWE UNGEKUA UMESHAKUFA, NI VILE TU MUNGU BADO ANAKUPENDA.
 
Kwa iman ya kiislam Kuna aya moja inasema "wa min shari hasidin idhaa hasad" hii binadam huwa tunamuomba Mungu na ina maana ya "Na unikinge na shari ya hasidi anapo husudu"

Hasad siyo uchawi ila Kuna watu tu wameumbwa akiangalia hata mtoto bas huyo mtoto ataumwa sana, kila atakacho shiriki ni lazima kitaharibika na kwa bahari mbaya watu hawa huwa hawajijui Kama wana hasad inaweza ikawachukua muda mrefu sana wakaja kugundua hata uzeeni.

Nakumbuka nina ndugu yangu ilikua kila akienda kijijin kumsalimia bibi akimpokea lazima amtemee mate na siku ya kuondoka hivyo hivyo siku moja akamuuliza kwann? alificha Ila baadae akamwambie hiyo ni Kinga maana mimi nina jicho la hasad naweza nikaangalia kitu kwa upendo ila kitu hicho kikaharibika, kwahiyo mate yangu ni baraka nakupa ili mambo yawe mazuri, hivyo hivyo hata mimi ninetemewa mate sana na wazee
asante kwa darasa huru, je! hasidi ndiyo hasad?
 
Kama unajiweza ama mkoa uliopo au wilaya alafu mwambie naishi kigoma mbali kabisa na alipo yeye kuna watu watakataa story yako Mimi mtoto WA shangazi mama yake alikuwa hataki kuolewa ilikuwa akija mchumba kumposa mama anamfata uyo mchumba Kwa Siri anamwambia uongo na kumtisha Hadi bidada anaachika wanaume watatu walimtosa sababu ya mama yake bidada baada ya kujua ilo akaenda kuolewa bila kumshirikisha mama yake na wala home hajajaa kitambo mama analala Tu
 
huyo mama kweli ana wivu
 
Namshukuru Mungu nimejenga nyumba na nilifanikiwa kwasababu niijenga kwa siri kubwa.

Chochote ninachofanya kizuri au cha kimaendeleo nikimjulisha tu mama kinakufa.

Iwe ni ajira, akinitembelea ofisini kama sijaachishwa kazi bila sababu basi kampuni itafilisika, ili mradi tu niharibikiwe.

Nikajizoazoa nikafungua mgahawa, alipokuja tu, kwa siku nikawa napata mteja mmoja au wawili au hawaji kabisa, nikashindwa ku run business kabisa hadi nikafunga.

Nilikima matikiti, yakaota vizuri sana, nikampeleka shamba kuona jitihada zangu, baada ya siku mbili tu, matikiti yote yakaibwa shambani usiku na hawakuacha hata moja.

Hajawahi kumpenda mtoto wangu hata mmoja, wala mzazi mwenzangu yoyote.

Mimi ni mzaliwa wake wa pili, licha ya kwamba kwa baba yangu ni mzaliwa wa kwanza.

Huyo kaka yangu ni teja, lakini ndio kipenzi chake, kazaliwa mwaka 1976 lakini hadi leo anakaa kwa mama, watoto wake wanasomeshwa shule nzuri.
Kwanza unaonyesha tayari unachuki na mamako, hayo mengine nikujazia nyama tu. Na unakoelekea utamwua mamako. Changamoto katika utafutaji zipo. Mtangulize Mungu hayo mengine ni hisia tu. Kuna miaka fulani nilikumbana na hali ya kuachishwa kazi kila inapofika mwezi wa nane mpaka ikafikia nikipata kazi sehemu nahakikisha mwezi wa nane nachukuwa likizo. Lakini baadae nilipuuza hizo hisia na kuamini katika ukuu wa Mungu na maisha yakaenda.
Kuhusu ajira hakuna namna namna utaachishwa kazi bila sababu lazima kuna sababu iwe udokozi kazini, utoro,uvivu wa kutokamilisha kazi kwa wakati, ushirikiano mbovu na wafanyakazi wenzako nk.
  • Kampuni kuflisika siyo suala lako ni la wenye kampuni sioni muunganiko wowote na mamako.
  • Kuibiwa matikiti ni suala la jamii inayokuzunguka halina uhusiano na mamako pia.
  • Kuhusu kutowapenda watoto wako hebu oa kwanza uwe na familia inayojitambua siyo unazaa na wanawake ovyo halafu unataka mamako awapende, atawapendaji ili hali hata wewe mwenyewe huwapendi?
  • Kabla ya kumtuhumu mamako chunguza mienendo yako kuhusu kuachishwa kazi. Hasara nyingine zinazosababishwa na jamii hizo unaweza kutafuta ufumbuzi kwa njia nyingine. CHONDE CHONDE ACHA CHUKI NA MAMAKO utazidi kuharibikiwa, acha hisia za kwamba anapendwa flani huo ni utoto. Tafuta maisha yako haya malalamiko yanatokana na stress.
 
If you believe in God, Mlaani shetani na upambane kutoa sadaka na kufanya amali njema.

Usiruhusu mawazo ya kishirikina. That is your Mom for crying out loud.

Huyo Kaka yako teja Mama yako kumpenda haimaanishi anything other than a Mother's pure love for her kids na ukizingatia hali ya kaka yako.

Praying for you and your Mom.
Asante kwa ushauri mzuri uliompatia, kwa kuongezea aache kujenga chuki kwa mamake. Tunasoma maelezo yake lakini pengine mama angekuja hapa stori ingekuwa tofauti kabisa. Anako elekea atamwua mamake.
 
Back
Top Bottom