Chochote kizuri nikimhusisha mama kinakufa

Hicho kiwanja bado kipo? Jitahidi ukiwekee uzio vinginevyo inakula kwako
 
Inasemekana mama hutoa laana baba hutoa baraka, kwa hiyo hata iweje mama hawezi toa baraka ndio maana baba nae hawezi toa laana ipo hivyo

Kwa hiyo tusiwe tunawaambia mama zetu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] daaahh we jamaaa , Dinazarde pole kwa hii shida [emoji1787][emoji1787]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan huyo uttoh ashindwee
 
Kaka
Ujue uchawi upo ni kweli ila mama ni mmoja we we jitahidi to a Masada panspohitajika na miheshimu
 
Akae kwake, uende kumjulia hali wewe peke yako, kama haipendi familia yako, kuna uwezekano hapendi na mafanikio yako pia! Usimshirikishe nini unafanya maishani mwako, bora unamhudumia, inatosha.
 
Amen.
 
Dah ..inaezekana tu kuna namna riziki yako hujaijulia vizuri,,,,unaweza ukaganya biashara 100,ile ya 101 ukapiga maisha ila mama ako ndo anakua kama bahati mbaya labda wakati ilipaswa ndo unaanguka labda ndo mama ako akatokea
Alafu umejuaje ni mama ako wakati watu kibao wanakuja mgahawani na huko kazini?
Trust me.
Wengine tushafanya biashara na kuhangaika zaid yako na mambo yakakwama lakini hatuhusishi uchawi mpaka last minute unasema Mungu nifungulie chaka lingine.
Mi nishafeligi kila kitu mpaka nikahisi mambo ya ajabu ajabu tu.ila guess what?
Huwa namuomba Mungu anifungulie mambo yoote mazuri aliyoniandalia,na kufungua minyororo yote iliyofungwa.
Mambo yamefunguka sana ila nilishajifunza kwenye wakati mgumi,kushindwa kila kitu na kuvunjika moyo sio kitoto
Ongea na watu watu,usi draw conclusions kirahisi.
Unaweza ukafikiri ni stor tu ila watu wanakwama sio kitoto na wananyanyuka.
Kuna bajaji napandaga mara kwa mara huyo mzee akaja akawa rafiki yangu..
Siku moja akanipa story alikua na mabus ya mkoani..lakini yalidondoka moja baada ya jingine na hapo ni baada ya kuwekeza mpaka jasho lake la mwisho.
Sasa hivi ana endesha bajaji kama miaka 4 sasa...
Lakin rodini anazo kama 5.anayoendesha yeye ndo imezaa hizo zingine.
Kwa jitihada zake jamaa hajakata tamaa mpaka uzeeeni anapambana,
Visa ni vingi,ongea na watu
Sikuwahi kuota ipo siku nitalaza laki laki mbili kwa siku kwa jinsi nilivyofeli mara kibao kuliko kufaulu.
Nakusisitiza ongea na raia
Ila ONYO:USIENDE KWA MGANGA.
 
Mkuu pole Sana. Kwa hili ninakuunga mkono. Narudia kuwa hutakaa uendelee kama utamhusisha mama yako mambo yako. Inawezekana kabisa ni mchawi au ana nuksi kali. Nawapeni mfano mmoja wa ukweli. Kulikuwa na mama mmoja na watoto watatu. Wawili wa kiume na mmoja wa Kike. Ufukara ulitawala Sana na pia magomvi na watoto wa kiume na Moja ya sababu huyo mama walimuita mchawi na hao watoto wa kiume wakawa wanamwita mchawi hasa mmoja wa kwanza. Mpaka ikifika kipindi wakamfukuza mama nyumbani. Binti yake alipoona mama amefukuzwa akaamua kumchukua akaishi naye. Hapo ndiyo kosa kubwa. Yaani Yule binti aliandamwa na mikosi na maisha yakaporomoka kabisa. Siku Moja binti akaamua ashirikishe mchungaji mmoja aje kuomba nyumbani angalau apooze machungu. Hakumuambia mchungaji kuhusu mama yake maana hakuwa anawaza kabisa kuwa Ile Hali imetokana na mama. Kifupi hakumuwazia mama yake. Alipofika yule mchungaji aliomba Sana na alimuona Yule mama wa huyo dada. Na alimuombea pia. Siku Moja akamwita Yule dada faragha akamwambia mama yako ana kitu ambacho kama utaendekea kuishi naye hutakaa uendelee kabisa. Alimshauri amwondoe pale nyumbani akamjengee nyumba au ampangishie ili mradi atoke pale nyumbani. Yule dada aliogopa kumuondoa mama yake. Hali ikaendelea kuwa ngumu mafanikio hakuna. Dada akakomaa tu na mama yake. Siku ikafika Yule mama akafariki. Yaani kuanzia siku hiyo Yule dada mpaka na KAZI kubwa ya cheo alipata. Pesa ikatukia ndani. Akaweza kukarabati na nyumba yake. Nilikutana naye akawa na furaha mno akasema mpaka pesa nyingine ameweka fixed account over half a billion.
Hivyo ndugu zangu kwenye familia ninaamini ziko nyingine zina mambo hasi Sana.

Note. Pamoja na kuwa Yule dada alijitoa Sana kumtunza mama yake lakini mama hakuwa anampenda bintiye hata kidogo. Yaani mpaka alikuwa anamfitini Kwa mume wako mpaka waliachana. Ila dada alivumilia na akawa hamshirikishi mama yake Jambo lolote.
 
Kabisa. Wako mama wengine siyo kabisa
 
aongee nn na hao raia ww ndio tufungue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…