Chonde chonde wabunge wa CCM msichague Tulia Ackson kuwa Spika, tayari ameshaonesha udhaifu wa kutosimamia katiba ya JMT. Hafai kabisa kuwa spika

Chonde chonde wabunge wa CCM msichague Tulia Ackson kuwa Spika, tayari ameshaonesha udhaifu wa kutosimamia katiba ya JMT. Hafai kabisa kuwa spika

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Tunajua mpo wengi ndani ya mjengo wa National Assembly. Maana ni karibu ya 98 % ya wabunge wote.

Japokuwa wengi mpo bungeni kimazabe mazabe baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 kuwa na maluelue lakini hili la spika kuweni na Uzalendo.

Bunge haliwezi kuwa na spika ambae ataona staha kuisimamia na kudhibiti serikali kuu kisa tu mkuu wa serikali ni amiri jeshi mkuu. Mathalani ukitokea ufisadi wa kutisha kama wa Rischmond je? Aone staha?

Wekeni ushabiki wa siasa kando na msichague spika kama huyu.
 
Tunajua mpo wengi ndani ya mjengo wa National Assembly. Maana ni karibu ya 98 % ya wabunge wote...
Mungu ndio huweka serikali za mataifa na viongozi wake, hivyo hata JPM aliletwa na Mungu na akaitwa na Mungu, Samia ameletwa na Mungu. Ndugai pia alipangiwa na Mungu, na ni Mungu alimruhusu shetani kumuingia na kumtelezesha ulimi, hivyo akaruhusu aondolewe, hivyo Spika ajaye tayari Mungu ameisha mpangia, na sisi baadhi yenu ni watu wa Mungu, tumeisha ambiwa Spika mpya ni Dr. Tulia!.

Tembelea hapa uangalie hili tuliambiwa lini!
P
 
Mungu ndio huweka serikali za mataifa na viongozi wake, hivyo hata JPM aliletwa na Mungu na akaitwa na Mungu, Samia ameletwa na Mungu. Ndugai pia alipangiwa na Mungu...
Moja Tulia alipaswa kujiuzulu kufuata nyendo za bosi wake!

Pili alipaswa kujiuzulu kwa kauli yake ya ajabu zaidi ya ile ya Ndugai.

Tatu yeyote atayeteuliwa kuwa Spika mpya mwambieni akome kujikomboleza Ikulu. Yeye na mwenzake wa Mahaka si kila hafla ya Ikulu ni lazima waende...
 
Mbeya kwa muda mrefu hatujawah kuwa na kiongozi mkuu Kati ya mihimili mitatu ya nchi it's our time go Tulia
Naunga mkono hoja, wanaosema, waache waseme, tayari kuna sauti imesema Spika ajaye ni Tulia.
P
 
Kumbe nawewe huna nafasi ya maamuzi kwenye chama?
 
Mungu ndio huweka serikali za mataifa na viongozi wake, hivyo hata JPM aliletwa na Mungu na akaitwa na Mungu, Samia ameletwa na Mungu. Ndugai pia alipangiwa na Mungu...
Na hapo ndipo ngoz nyeus tunapofeli kuamini kuwa eti viongozi wanaletwa na Mungu..mbona mnamsingizia Mungu kwa mambo ya ajabu hata hamuoni aibu, umefanya ngono zembe umepata ukimwi unakufa .."mapenz ya Mungu"..unaendesha gar unachat unapata ajal unakufa " mapenz ya Mungu"..uongoz mbaya watu wanakufa kama rwanda " mapenz ya Mungu.

Mungu alishamaliza kaz yake dunian baada ya Uumbaj na kutupa kiila kitu ..yanayoendelea ni creation zetu sis wanadamu na ndomana kuna free will.

Achen kupotosha watu na hii ndio ilifanya mzungu atawale africa kwa maneno kama hayo..et viongoz wanaletwa na Mungu....mkoloni alikua akikosewa anatoa adhabu halaf anasema kaambiwa na Mungu unapewa bible unasoma samehe 7×70 game over.
 
1641872223000.jpeg
 
Tunajua mpo wengi ndani ya mjengo wa National Assembly. Maana ni karibu ya 98 % ya wabunge wote.

Japokuwa wengi mpo bungeni kimazabe mazabe baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 kuwa na maluelue lakini hili la spika kuweni na Uzalendo...
Tatizo wabunge wetu wakiingia bungeni uwezo wao wa kufikiri na kutenda huwa wanaziacha akili zao reception
 
Mungu ndio huweka serikali za mataifa na viongozi wake, hivyo hata JPM aliletwa na Mungu na akaitwa na Mungu, Samia ameletwa na Mungu. Ndugai pia alipangiwa na Mungu, na ni Mungu alimruhusu shetani kumuingia na kumtelezesha ulimi...
Wacha kumkashifu Mungu wewe.

Sema hao wote waliletwa na tume ya uchaguzi.
 
Moja Tulia alipaswa kujiuzulu kufuata nyendo za bosi wake!
Pili alipaswa kujiuzulu kwa kauli yake ya ajabu zaidi ya ile ya Ndugai.
Tatu yeyote atayeteuliwa kuwa Spika mpya mwambieni akome kujikomboleza Ikulu. Yeye na mwenzake wa Mahaka si kila hafla ya Ikulu ni lazima waende...
Kujikombakomba tayari ni gonjwa hatari ndani ya ccm
 
Back
Top Bottom