Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Ndugu zangu wana Mbeya, mimi ni miongoni mwa wapingaji wakuu wa mkataba wa uwekezaji bandarini, hususani ile IGA. Huo mwingine bado hatujui kama ni mzuri au tumepigwa.
Lakini, kuna njia sahihi na njia isiyo sahihi ya kupinga jambo. Njia sahihi ni kama ile aliyoitumia Lissu kwa kuelezea mapungufu ya mkataba ule kwenye mikutano halali ya hadhara.
Njia nyingine sahihi ni ile waliyotumia Mwabukusi na Mpaula ya kwenda mahakamani. Na wengine pia kama TLS , wadau wa hapa JF, wabunge kule bungeni, TEC pamoja na wananzuoni wengine kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Kwakuwa serikali imeamua kupuuzia ‘concern’ za hao wote, basi njia pekee sahihi iliyosalia ni sanduku la kura katika uchaguzi ulio huru na wa haki. Kwamba, nguvu ielekezwe kwenye kidai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya kwa njia halali na kisha sote tutayatoa maoni yetu kupitia sanduku la kura.
Kuna kipindi mkoa wa Mbeya ni kama ulisuswa na serikali kutokana na tabia za watu wake kupenda ‘ligi’ kwenye kila jambo. Wakati wa JPM na hata sasa walau mambo yameanza kwenda vizuri.
Kwahiyo naomba niwasihi ndugu zangu, msitumike kifanya uhalifu wa maandamano yasiyo na kibali ili tu kupaisha ndoto za kisiasa za Mwabukusi na Mpaula.
Bandari sio mali ya Mbeyapeke yake bali Tanzania yote. Kama wenzenu hawaandamani nanyi hamna haja ya kufanya hivyo. Msijifanye mna uchungu saaana hadi mkaanza kuvunja sheria na kujiharibia bure.
Naamini hakuna atakaye andamana, lakini ni muhimu kukumbushana wajibu wetu kama wananchi wapenda maendeleo na amani.