Chonde chonde wana Mbeya msikubali kutumika, msishiriki hayo maandamano haramu

Mimi mwanaume wa Mbeya, nafahamu vema hasara ya maandamano yasiyo halali. Wengi mnaochochea hui ujinga hampo Mbeya.

Narudia tena, wana Mbeya msiwasikilize wahalifu hawa. Mheshimiwa Rais SSH amewaheahimu sana Mbeya na kuwapendelea. Ukibebwa bebeka. Waachieni Mpaula na Mwabukusi maandamano yao.
Mbowe na huko kwao Hai wamekaa kimyaaa huku kwenye keyboard mnaparurana.
Chadema hovyo kabisa.
 
Uzuri Wana mbeya Wana ghala la chakula
Hawana njaa
Huwa wanakula wanashiba😂🤣
Wana shibe na nguvu
Sio wanaume wa buguruni wanaoshindia miguu ya kuku na maji ya kandoro🤣😂
Hakuna shibe kwenye mabomu ya machozi, virungu na maji ya washawasha. Wana Mbeya wanalitambua hilo. Kesho hawatoandamana.
 
Ndugu zangu wana Mbeya, mimi ni miongoni mwa wapingaji wakuu wa mkataba wa uwekezaji bandarini, hususani ile IGA. Huo mwingine bado hatujui kama ni mzuri au tumepigwa.

Lakini, kuna njia sahihi na njia isiyo sahihi ya kupinga jambo. Njia sahihi ni kama ile aliyoitumia Lissu kwa kuelezea mapungufu ya mkataba ule kwenye mikutano halali ya hadhara.

Njia nyingine sahihi ni ile waliyotumia Mwabukusi na Mpaula ya kwenda mahakamani. Na wengine pia kama TLS , wadau wa hapa JF, wabunge kule bungeni, TEC pamoja na wananzuoni wengine kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Kwakuwa serikali imeamua kupuuzia ‘concern’ za hao wote, basi njia pekee sahihi iliyosalia ni sanduku la kura katika uchaguzi ulio huru na wa haki. Kwamba, nguvu ielekezwe kwenye kidai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya kwa njia halali na kisha sote tutayatoa maoni yetu kupitia sanduku la kura.

Kuna kipindi mkoa wa Mbeya ni kama ulisuswa na serikali kutokana na tabia za watu wake kupenda ‘ligi’ kwenye kila jambo. Wakati wa JPM na hata sasa walau mambo yameanza kwenda vizuri.

Kwahiyo naomba niwasihi ndugu zangu, msitumike kifanya uhalifu wa maandamano yasiyo na kibali ili tu kupaisha ndoto za kisiasa za Mwabukusi na Mpaula.

Bandari sio mali ya Mbeyapeke yake bali Tanzania yote. Kama wenzenu hawaandamani nanyi hamna haja ya kufanya hivyo. Msijifanye mna uchungu saaana hadi mkaanza kuvunja sheria na kujiharibia bure.

Naamini hakuna atakaye andamana, lakini ni muhimu kukumbushana wajibu wetu kama wananchi wapenda maendeleo na amani.
Mzalendo uchwara
 
Naona unaliishi jina lako la Mzalendo uchwara. Na ushauri wako ni wa uzalendo uchwara.
 
Mimi mwanaume wa Mbeya, nafahamu vema hasara ya maandamano yasiyo halali. Wengi mnaochochea hui ujinga hampo Mbeya.

Narudia tena, wana Mbeya msiwasikilize wahalifu hawa. Mheshimiwa Rais SSH amewaheahimu sana Mbeya na kuwapendelea. Ukibebwa bebeka. Waachieni Mpaula na Mwabukusi maandamano yao.
Siamini. Mbeya haina watu wa namna yako. Wewe ni lazima utakuwa unatoka katika jamii zile zenye tabia za ajabu ajabu.

Jamii za watu wa bara, wengi wao ni watu walionyoka, ukiacha wale wachache walioharibiwa na CCM.
 
Siamini, Mveya haina watu wa namna yako. Wewe ni lazima utakuwa unatoka katika jamii zile zenye tabia za ajabu ajabu.

Mzalendo Uchwara ni chawa. Kwanza hata jina lake linaonyesha kwamba jamaa ni fake man, hawa ndio wako tayari hata kuingiliwa kinyume ili tu wapate hata 10,000
 
Kwa mujibu wa sheria zetu maandamano halali yanahitaji kibali. Hayo ya Mpaula na Mwabukusi hayana. Hivyo ni haramu.

Nakuunga mkono, tume huru ni takwa letu wananchi, na ndio itakayotupa njia sahihi ya kuiwajibisha serikali pale inapofanya yasiyotakiwa.
Wewe kumbe ni wale waliokosa uelewa karibia wa kila kitu! Pumzika hujui chochote.

Hakuna mahali popote ambapo Polisi wamepewa mamlaka ya kutoa kibali cha mikutano au maandamano. Wanapewa taarifa, na jukumu lao ni kuwahakikishia waandamanaji usalama.

Polisi ni waajiriwa wa wananchi. Boss akitaka kuandamana, anamwambia mwajiriwa wake kuwa anataka kuandamana, na yeye polisi aje ahakikishe usalama wa boss.
 
Siamini, Mveya haina watu wa namna yako. Wewe ni lazima utakuwa unatoka katika jamii zile zenye tabia za ajabu ajabu.

Jamii za watu wa bara, wengi wao ni watu walionyoka, ukiacha wale wachache walioharibiwa na CCM.
🤣😂
Si waliimbaga watu wa bara hawajui meli
Ni kweli manake bara hakuna bahari,Kuna mito ya asili
 
Back
Top Bottom