Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Katika makosa ambayo Hayati Magufuli aliyafanya kwa kujua au kutojua ni kutoa vyeo kwa wapinzani wanajiunga CCM kutokea upinzani. Ni ukweli usiosemwa lakini unawaumiza wanaCCM, watu walioshirika kupunguza kura leo wanafikiriwa zaidi.
Kuna wale wabunge 19 wa CHADEMA ambao maamuzi pengine yatatolewa ya kufukuzwa uanachana na ikatokea hivyo, Chondechonde wasifikiriwe kwa vyeo kwanza hata wakiamia CCM kwa Sababu
1. Wameonesha waziwazi kabisa wapo tayari kufanya usaliti kwa Sababu ya vyeo, ikiwa walijua ukweli hawana uhalali wa kuendelea wangejiondoa ubunge hata kama Kuna ugumu
2. Wametolewa na vyama vyao wakiwa ni wachafu hivyo CCM lisitumike kama dodoki la kusafishia uchafu wao, madhara ya kuwa dodoki yanagharimu Sana.
3. Mdee na wenzake hawajawahi kuikubali CCM hivyo ikitokea wamehamia CCM hasa kipindi hiki ni kujidanganya wenyewe.
4. Badala ya kupewa nafasi za uteuzi moja kwa moja waanze na nafasi za ugombea ili kupima kukubalika kwao kwa wananchi.
5. Wakijiunga na CCM wawe wanachama wa kawaida lakini ikiwapendeza wagombee nafasi zinapojitokeza na wapewe nafasi kuonesha utayari wao kukitumikia chama.