Chondechonde Serikali: Msiwaonee walimu haswa walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu elimu kata

Chondechonde Serikali: Msiwaonee walimu haswa walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu elimu kata

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,848
Reaction score
7,762
Halo wadau wa JF.

Kuna tetesi nimezinasa kuwa serikali ina mpango wa kuwanyima posho walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu elimu kata. Madai ya serikali ni kuwa hawa watu hawapo kazini ktk kipindi cha likizo isiyo rasimi au likizo ya corona.

Lengo ni kuwa posho zao zielekezwe kuikabili eti corona. Hamuwaoni wabunge, DC, RC, DAS, RAS, makatibu wakuu, mawaziri, manaibu waziri, wakubwa kwenye jeshi, polisi, DED, Wakurugenzi wa mashirika ya umma?

Kwanini posho za walimu eti wapo likizo hawana kazi? Mbona wanaagizwa kupeleka nyaraka na takwimu mbalimbali za kishule na kata wilayani hata kipindi hiki? Wasafiri na nini?


Hivi walimu wameikosea nini jamii na serikali mbona wao tu?
CWT kaeni chonjo!

Japo Mimi sio mnufaika wala sifanyi kazi za elimu, ila inaakera kuona wadogo zetu, kaka zetu, Dada zetu na wazazi wetu wakidhulumiwa kwa ukimya wao.

Ni hayo tu.
 
Mkuu umeandika kwa uchungu pole sana tutawanyang'anya posho tu mshahara tutakuja baadae kuwalipa nusu pamoja na wale ambao watakuwa likizo ya corona
Huu ni ujinga na uoga kabisa, nitawaona CWT kama wana meno kipindi hiki. Au hata TUCTA.
 
Wazuie posho ziende kwenye corona,kama hutaki andika barua uachie ngazi kuna walimu wengi wenye kuweza kufanya kazi hizo.
Ungejua Mimi sio mwalimu na hata kazi hiyo siitaki bure, usingeandika hayo. Nikiri tu ndugu zangu wengi ni walimu. Pia tuna Mratibu ambaye ni mjomba wangu.
 
Ungejua Mimi sio mwalimu na hata kazi hiyo siitaki bure, usingeandika hayo. Nikiri tu ndugu zangu wengi ni walimu. Pia tuna Mratibu ambaye ni mjomba wangu.
Sasa kama huko kwenye tasnia hiyo,ni mjomba na ndugu zako,hiyo posho unataka wapewe ya nini wakati wapo kwenye karantini,au unataka wazuie na mshahara?
 
Alaf baadae serikali hulalamikaga kwanini shile za serikali hazifqnyi vizuri...
Shida huanzia kwenye mambo kama izi
 
Sasa kama huko kwenye tasnia hiyo,ni mjomba na ndugu zako,hiyo posho unataka wapewe ya nini wakati wapo kwenye karantini,au unataka tuzuie na mshahara?
Hao wakubwa niliowataja hapo juu hadi wengine wametajwa na CAG kwa wizi mbona hawaguswi? Hapo ndiyo napoona huruma kwa wanyonge hawa.
 
Back
Top Bottom