Chongoleani, Tanga: Rais Magufuli na Museveni waweka la jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima - Tanga

Chongoleani, Tanga: Rais Magufuli na Museveni waweka la jiwe la Msingi mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima - Tanga

Faida ya muda mfupi mkuu.

Mradi ukikamilika wote waliopata kibarua wanabwagwa chini
Amka mkuu..

The world is so fast..!

Pale Tanga kuna Bandari, hiyo shehena ya Mafuta itakuwa inahifadhiwa Tanga na ndio sehemu ambapo meli zitakuwa zinakuja kupakia mzigo wa mafuta..

Sasa kwa Taarifa:

Kuna ajira zaidi ya 15, 000 za muda wa miaka 3 hadi 2020 ambapo hili bomba litakamilika mkuu.

Na kuna kazi za kudumu zaidi 2500 baada ya ujuenzi kukamilika .

Bomba litatoka Hoima - Magharibi mwa Uganda hadi Tanga

Kuna umbali wa maili 880( zaidi ya km 1400)

Sasa mkuu wewe kama huoni faida bado...wacha watu waendelee.
 
Uganda wana hasara aisee. huyu simuelewi anachozungumza
 
Tujifunze kutafuta na positive angle kdogo! Mradi huu ungekwenda Kenya kama ilivyokuwa imepangwa awali mngekuja hapa na mzigo wa matusi kwa Serikali.

Leo Viongozi wetu wamejitahidi kushawishi mradi huu mkubwa wenye faida kubwa kwenye nyanja zote za kijamii tunabeza tena, hv ni lini tutaanza kuona kama hata makubwa kiasi hiki hatuoni?

Sent using Jamii Forums mobile app


Mkuu usishangae,hilo ndo Taifa ambalo wahenga, wazazi wetu walitutengenezea.Ni Kizazi kama kile cha Kiyahudi enzi zile za Yesu.Yesu aliwahi kulalamikia Tabia kama hii.Wayahudi walimuita Yohane Mbatizaji kama mtu "chizi" na aliyechanganyikiwa kwa kuendesha yake maporini kwa kula asali na kuvaa nguo za ajabu ajabu.Lakini wakati huo huo, Yesu alipokuja na kuamua kuishi tofauti na mtangulizi wake,Yohane Mbatizaji, akaishi katikati yao; akala nao na kunywa nao na kupiga nao stori lakini wakachomoka baadhi ya watu na kusema Yesu ana "vimelea" vya ulafi kwa tabia zake za kupenda kula na kunywa tena pamoja na wadhambi.

Wako watu kwa sababu ndimi zao na midomo yao hazilipiwi VAT basi wanaropoka lolote tu bila kuchuja maneno yao kabla ya kuyatoa nje ya meno yao.

Kwa mfano,leo nimeshangazwa na Gazeti la Tanzania "kushobokea" ununuzi Wa ndege ya Gwajima kuwa ni ndege ya kifahari kuzidi Bombardier!Bila shaka wanapiga dongo Bombadier zilizonunuliwa na Magu. Hivi hilo la Gwajima nayo ni habari ambayo ina umuhimu Wa kiasi hicho? Gwajima amenunua ndege hiyo kwa maslahi yake binafsi na wala sio kwa ajili ya faida ya waamini wake moja kwa moja.

Ndege ya Gwajima ni ya kibiashara.Ameshaona soko hapa East Afrika.Wako wafanyabiashara na watu wengine wenye uhitaji watakuwa wanaikodi na yeye kujipatia pesa.Kwa ufupi ni uwekezaji wake na marafiki zake walioko nje.

Gwajima kwa ndege hiyo pia atavuna pia waumini wajinga.Waumini watakaoamini na kupenda kujivuna kuwa kiongozi wao ni wa ukweli na ana "kibali" mbele ya Mungu kwa sababu anamiliki Helikopta,treni na JET ya kifahari!

Gwajima anaboresha mradi wake wa kubiashirisha Injili.Wahubiri wa kweli Wa nyakati zetu wanakazania kusimika na kuboresha huduma za kijamii.Wanajenga shule,hospitali,wanahudumia watoto na watu wengine walioko katika mazingira magumu.Kwa lugha nyingine wanawafundisha watu waliotengwa na ulimwemgu kujipatia furaha na amani kamilifu mioyoni mwao.Watu wakielimika sawasawa watakuwa na Amani mioyoni na watatawaliwa na furaha tele.Wagonjwa wakipatiwa tiba watarejewa na furaha na matumaini makubwa.Mhubiri anayeshindwa kuwekeza katika huduma za kijamii na kufanya mambo ya kuchochea watu waende kwenye "miujiza", huyo ni mfanya biashara na bila shaka anatengeneza jamii ya watu wenye macho yanayoona lakini hayaoni chochote.Ndio kama hawa wachangiaji na watanzania wengine wasioona umuhimu wa hili Bomba la Mafuta.
 
Leo tumesika kuwa bomba linalojengwa ambalo ufunguzi wake ni leo lina urefu wa takriban Km 1400 na kwamba ndilo litakuwa bomba refu kuliko yote Africa.Wakati huohuo tuliashaelezwa kuwa bomba la mafuta la TAZAMA kutoka Dar es salaam mpaka Ndola ,Zambia lina takriban urefu wa Km 1700 ambalo vilevile lipo ndani ya Africa.Wadau mahesabu haya yamekaaje ?
La zambie ndio bomba refu mkuu..
 
Naungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Magufuli na Serikali yake pamoja na Rais Mseveni wa Uganda kwa kuandika historia mpya ya ushirikiano wenye tija.

Historia inaandikwa kwa nchi mbili za Tanzania na Uganda ambapo jiwe la msingi linawekwa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo jiwe la msingi la kuanza ujenzi huo litawekwa.

Ni heshima Kubwa nchi yetu ya Tanzania kupata fursa hii ya bomba la mafuta kupita nchini Tanzania ambao utapita mikoa 8, Wilaya 24 na vijiji 184.

Kuna faida nyingi sana kama Taifa tutapata kutokana na uwepo wa mradi huu wa bomba la mafuta.

Wakati wa ujenzi Watanzania wengi watapata fursa ya ajira ambapo jumla ya ajira 40,000 zitapatika. Ajira za ufundi, ulinzi, upishi, usafiri, fursa za malazi, na huduma za kifedha.

Ukiachilia mbali fursa hiyo mradi huu utapelekea kufunguka kwa Ukanda wa Biashara kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Rwanda, Burundi, Kongo, Sudan ambapo wanaweza kuunganishwa na miundombinu hiyo na kusafirisha mafuta kwa urahisi.

Kukamilika kwa mradi huo nchi za Tanzania na Uganda zitapata mapato na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wake.

Faida nyingine ya bomba la mafuta kuwa ni pamoja na gharama za mafuta kupungua kutokana na nchi za Afrika Mashariki kutumia mafuta yake yenyewe kwenye magari pamoja na ndege hivyo kuchochea kasi ya utalii katika nchi husika pamoja na ajira.

Gharama ya mafuta itakapo pungua ni dhahiri gharama za usafiri, usafirishaji na bidhaa nazo pia zitapungua. Maisha kuwa rahisi.

Naipongeza Serikali ya Dk. Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa ujenzi huu wa bomba la mafuta kutoka Uganda. Haikuwa kazi rahisi Tanzania kupata fursa hii ya bomba la mafuta kutoka nchini Uganda kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo.

Narudia tena kumpongeza Dk. Magufuli kwa kutuletea mradi huu wa bomba la mafuta utakaokuwa na tija kwa Taifa vizazi na vizazi. Ni jukumu letu Watanzania kuulinda mradi huu wa bomba la mafuta.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Dk. Magufuli

Na Emmanuel J. Shilatu

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuko pamoja nawe kupongeza Serikali zetu katika hili
 
Amka mkuu..

The world is so fast..!

Pale Tanga kuna Bandari, hiyo shehena ya Mafuta itakuwa inahifadhiwa Tanga na ndio sehemu ambapo meli zitakuwa zinakuja kupakia mzigo wa mafuta..

Sasa kwa Taarifa:

Kuna ajira zaidi ya 15, 000 za muda wa miaka 3 hadi 2020 ambapo hili bomba litakamilika mkuu.

Na kuna kazi za kudumu zaidi 2500 baada ya ujuenzi kukamilika .

Bomba litatoka Hoima - Magharibi mwa Uganda hadi Tanga

Kuna umbali wa maili 880( zaidi ya km 1400)

Sasa mkuu wewe kama huoni faida bado...wacha watu waendelee.
Yaani BAWACHA ni janga
 
Actually..! Magufuli is sometimes missing his point..!

I don't see if there was neccessity of having all goverment officials for just one event..

Vyombo vya usalama vyotee vya nini sasa kwa mfano..?

Sijui nini kimejificha hapa..Muda ni mwalimu mzuri
 
Amka mkuu..

The world is so fast..!

Pale Tanga kuna Bandari, hiyo shehena ya Mafuta itakuwa inahifadhiwa Tanga na ndio sehemu ambapo meli zitakuwa zinakuja kupakia mzigo wa mafuta..

Sasa kwa Taarifa:

Kuna ajira zaidi ya 15, 000 za muda wa miaka 3 hadi 2020 ambapo hili bomba litakamilika mkuu.

Na kuna kazi za kudumu zaidi 2500 baada ya ujuenzi kukamilika .

Bomba litatoka Hoima - Magharibi mwa Uganda hadi Tanga

Kuna umbali wa maili 880( zaidi ya km 1400)

Sasa mkuu wewe kama huoni faida bado...wacha watu waendelee.
Yaani BAWACHA ni janga la watu wasio na kumbukumbu na watu wanafiki kupitiliza
 
Yaani Uganda Wanahasara Sna Huyo Jamaa Yao Kaongea Nn Hata Haeleweki,kuwa Na Mtu Km Yule Anaboa Sna
 
Actually..! Magufuli is sometimes missing his point..!

I don't see if there was neccessity of having all goverment officials for just one event..

Vyombo vya usalama vyotee vya nini sasa kwa mfano..?
Anabana matumizi mkuu
 
Mzee kaongea vitu murua kabisa hapa, sijui kama braza niko naye kwa mbali kidogo kama kaelewa au kuna mtu jirani anamwelezea, {reli, power station, etc.}
Any way. Hivi watani wangu, kuna haja gani kuvaa sare za ccm kwenye uzinduzi wa bomba la mafuta, linaenda uganda sare inahusika nini jamani????
 
Kwanini mkuu?
Likifanyika jambo A wanasema walitaka B, Likifanyika B wanasema wanataka A. Likifanyika A na B watasema hayakuwa na umuhimu huku wakiporomosha mitusi mizito. Lakini kama wao wakifanya kidude kiduchu KELELE KIBAO KAMA TEAM KIBA !
 
Back
Top Bottom