BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Katibu mkuu amekusikia.Awaambie ukweli hao wakuu wa shule na baadhi ya makada wenzake wa ccm, shule zinakufa kwa sababu ya upigaji uliopitiliza.
Leo shule ya sekondari Meta kule Mbeya imekufa kwa sababu ya ufisadi! Mbalizi nayo iko mahututi! Walimu hawalipiwi mishahara! Sangu Sekondari haisikiki tena! Achana na shule nyingine! Zote ziko hoi bin taaban! Kisa tu ubadhirifu uliopitiliza.
Yaani ccm na ufisadi/wizi kama pete na kidole vile.
JIWE na sanaa zake zote kwa hizi shule hakufua dafu. Shule za kata ndo zimeua hizi shule maana hazina tena maajabu.CHONGOLO MGENI RASMI KIKAO CHA WAKUU WA SHULE ZA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA- ASUBUHI HII.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo, Leo Ijumaa tarehe 15 Julai, 2022 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kikao cha Wakuu wa Shule za Umoja wa Wazazi Tanzania.
Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma kuanzia saa nne asubuhi.
#Chongolokazini
#Kaziinaendelea
Chama cha wapigaji hicho! Kimejimilikisha pia maeneo ya wazi na kujenga vibanda vya biashara, majengo ya serikali, viwanja vya michezo, nk.Sijwahi kuona kwingine duniani chama cha siasa kinamiliki na kuendesha shule.
Ccm ni chama kikuu cha mafisadi ulimwenguni.Sijwahi kuona kwingine duniani chama cha siasa kinamiliki na kuendesha shule.
Tukumbushane.CHONGOLO MGENI RASMI KIKAO CHA WAKUU WA SHULE ZA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA- ASUBUHI HII.