Choo cha kukaa hakimalizi haja; Wamasai wa Loliondo wapewe pesa wajenge nyumba zao wenyewe kulinda asili yao

Choo cha kukaa hakimalizi haja; Wamasai wa Loliondo wapewe pesa wajenge nyumba zao wenyewe kulinda asili yao

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kila mtu ana asili yake! Na maendeleo ya mtu ili yawe na maana lazima yaguse asili ya mtu!

Ukimtoa masai umasaini aje aishi masaki, hii siyo maendekeo kwake bali ni kashfa na ni kumuua (kumharibu kiasilia na lazima siku atarudi alikotoka)

Mtu aliyezoea kunjunga haja yake polini ukimjengea choo cha kukaa hawezi kufulahia hata kidogo!

Mfano! Mimi mwenyewe siyo masai, pamoja na kufika mataifa kadhaa lakini raha ya choo cha kuchuchumaa bado naona ni bora sana kuliko choo cha kukaa!

Kwanza utafiti wangu huwa unaniambia choo cha kukaa huwa hakimalizi haja vizuri kama ilivyo choo cha kuchuchumaa!

Ebu waza ukila matunda ya FURU unavyopata tabu kutenga vifungu vifungu huko polini halafu leo ukajisaidie haja kwenye choo cha kukaa hata iweje HAKITOKI hata ukae chooni siku nzima!

Choo cha kukaa ni kwa ajili ya wazee, wagonjwa, vibonge na wala urojo!

Lakini mtu jabari shababi choo cha kukaa hakifai, kwanza huwa kinanichanganya hata nisijue MKONGE uning'inie kwa ndani au uegemee sinki inje!

Wamasai wa loliondo hawakutakiwa kabisa kujengewa nyumba, Bali wangepewa chaguo ili wajenge nyumba zao wenyewe popote wanapotaka kwenda! Yaani watawanyike kila mtu aende kijiji anachokijua yeye mwenyewe!

Hivi Masai aliyezoea choo cha pori kwa pori atamudu vipi usafi wa choo cha kuflashi kweli?
Hiyo bili ya maji na umeme nani atamlipia?

Amezoea nyumba ya dongo na nyasi unamuwekea bati hizo kelele za mvua kwenye bati mnauhakika masai atazivumilia kweli?

Mtu aliyezoea upepo asilia kuanzia chumbani hadi mavazi yake havai hata chupi Leo mnamuwekea dirisha la vioo mnauhakika ataishi humo?

Asilimia 80% masai wanategemea dawa kutoka polini (mitishamba), Leo unamhamisha kutoka LOLIONDO kwenye miti ya tiba aliyozoea unampeleka wapi? Ebu niambie tanga kuna Mkongoraah?

Masai kazoea kuhama nyumba kulimotokea msiba sasa leo hii nyumba ya kudumu ya vioo itakuwa vipi?

Halafu hizo waya za umeme mmeweka vizuri kweli? maana kukiwa kunashoti mkumbuke masai mmoja akifa kwa umeme wote watakimbia hizo nyumba

Tuache utani ,Nina wasiwasi sana kama hiyo project ya kuwahamisha wamasai kama itadumu!

Tunaweza kuwahamisha kimwili lakini kiroho na akili bado watarudi LOLIONDO!

Hesabu za kisayansi zinaniambia masai atahamishwa Leo kutoka LOLIONDO lakini siku si nyingi atarudi LOLIONDO!

Wacha tuone?
 
Waeza rudia mara mbili ama tatu kwa kitu ambachoo ni cha once a day. Eti kwa mwenye shibe njia ya kwenda chooni huwa haioti nyasiii..hahaaaa
 
Kwa kweli choo cha kukaa ni mtihani mkubwa saana, nilipanga nyumba choo ni cha kukaa, ilibidi niwe napanda kwa juu juu tu, au kutega ndoo chini, la sivyo nikitaka kukaa niende na pc chooni ama simu kabisa na bado mtihani tofauti na kuchuchumaa

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli choo cha kukaa ni mtihani mkubwa saana, nilipanga nyumba choo ni cha kukaa, ilibidi niwe napanda kwa juu juu tu, au kutega ndoo chini, la sivyo nikitaka kukaa niende na pc chooni ama simu kabisa na bado mtihani tofauti na kuchuchumaa

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
Kuchuchumaa ni fasta tu mwaaaah mambo ya kubakisha uchafu tumboni hainaga
 
"choo cha kukaa hakimalizi haja" hii nimechukua.
Ni kweli mkuu wala siyo utani, mi nikijisaidia kwenye cha kukaa huwa kama napunguza tu!
Lakini nikitaka mzidmzigo wote utoke lazime nitafte choo cha kuchuchumaa
 
Hawa walioko huku mjini huwa wanaenda Vijijini kwao kujisaidia kisha wanarudi tena mjini?????

Hadi kunya vichakani ni sehemu ya tamaduni zetu??? Kweli??
Hawa waliko mjini ushawahi kuwaona wameingia choo cha kufrash?
Ebu niambie kama ushawahi kukutana na masai kwenye korido yoyote ya choo mjini!

Mara nyingi wanatenga kwenye mitaro, magofu na vichochoroni
 
Back
Top Bottom