Mkuu vuka umri wa miaka 55 ili uvipende kwa lazima na kuviona umuhimu wake, vya kuchuchumaa kumbuka unajibeba mzee baba?
Kama walivyotangulia kusema wadau wengine hapo juu, choo hicho kinafaa private bedroom(wanaita self)na kama ni hotelini, usafi wa hoteli hiyo usiwe ni wa kutiliwa mashaka.
Ukikizoea aina hii ya choo, hata ukiwa matembezini, ukibanwa haja utatamani kurejea nyumbani ukanyee huko.
Ukisikia mtu anachatia chooni ndo yupo kwenye ivo vitu, unawezafanya mambo zaidi ya moja kwa wakati mmoja tana bila ya bughudha yoyote.
Hata kama unaumwa tumbo la kuhara, vyoo hivyo vina sound proof, zile 'mbwiii mbwiii, tratatatata' hazitoki kusikika nje, kwa sababu unapokaa sauti unaibana kuizuia automatik haitoki nje kusikika kama vyoo vya uswahilini, ambavyo ukitoka kujisaidia na kopo lako mkononi hadi unajihisi aibu kwa sauti uloizalisha chooni.