ngoja nikuulize swali naomba unijibu mafundi wote hao against ronaldo.
1. kati ya hao mafundi uliowataja ni nani mpira ukae kushoto au kulia anaweza piga shuti kali nje ya 18 na kufunga? tena sio goli moja wala mawili magoli kibao kwa kutumia miguu yote miwili?
2. ni nani kati ya hao ana uwezo wa kuruka juu kushinda majority ya wachezaji kikapu wa NBA marekani na kufunga goli?
3. kati ya hao uliowataja ni nani anaweza nata hewani sekunde 2 au 3 kusubiria mpira ambao haujafika na kupiga kichwa na kufunga?
kuongezea tu ronaldo ana magoli zaidi ya 100 ya vichwa, magoli zaidi ya 100 ya mguu ambao hautumii sana (weak foot) hio ndio strength ya ronaldo na kitu kinachomfanya yeye awe wa kipekee kuliko fundi yoyote duniani.
kama unae unaemjua wewe alofanya zaidi ya ronaldo kwenye hayo mambo naomba umtaje hapa. nakusubiria.