Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Utafiti unaonesha Waimbaji wa kike mara nyingi ndoa zao either zina viraka au zimevunjika kabisa
1) Beatrice muhone
2)Rose Muhando
3)Bahati Bukuku
4)Martha Mwaipaja na sasa
5)Angel Bernad
6) Christina Shusho

Hii sio Coincidence kuna shida mahali.
Beatrice Muhone kafanyaje?
 
kumbuka kuwa kuna aina mbalimbali za misalaba ikiwemo hiyo ya masonic. Nenda makaburini utaiona ilivyo na maumbo ya ajabuajabu na ndugu za marehemu hawajui kuwa kuna misalaba ya mason wanaweka tu ili mradi ni msalaba
kwaiyo msalaba unaousema ww ni kitu kizur cha kuweka kanisan?? na maana yake ni nn ukiweka kanisan
 
Kwani Dayamondi anadumu na mwanamke mkuu? Naye ipo siku atambwaga tu kama alivyowabwaga wengine.
mond huwa anaopoa pisi kali yeyote anayoitaka ikinasa kwenye anga zake anayo, anakula mpaka anapata mtoto kisha anaacha mbwa yule
 
Sizani.
Nafsi yangu inakataa kuamini hata kidogo.

Asingeambatana nae wazi wazi vile ktk hali ya kawaida.
Mwanamke akishatoka kwenye ndoa hata akipata mwendani wake atatoka kwa staha na kificho ktk kujiheshimu.
Diamond ni homeboy wake tu na nia ya kuimba as pale ilikuwa ni njema ktk kuwafikia kundi fulani kwenye jamii ambao wanaenda kwenye matamasha ya Diamond lakini kanisani hawaendagi. Hata Mtume Paulo alitumiaga aproach hiyo pia wakati wa kueneza Injili.
hiyo approach ya tina ni ya kihuni hailingani na mtume paulo
 
Hey Ma'am Christine hii nayo hapana,unaanzaje kumuacha mtu alietoka na wewe chini?
Hayo unayotaka sasa si ungetimiza ukiwa solo!
Money na fame zinasumbua ndoa nyingi sana,wanawake sasa hivi wanasumbuka na hivi vitu sana,akiingia tiktok aone fake life za mastaa na tiktokers anakuona we fala tu,hata ataanza kuona unafanana na n'gombe.
Anyway kila mtu na mambo yake,hebu nikondeshwe na yangu.
 
KAMA SHIDA NI NABII MWANAMKE TU, WAPO.

1. LUKA 2:36 INASEMA; 36 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. 38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
2. MKE WA NABII ISAYA; Isaya 8:3 inasema; Ndipo nikamkaribia yule nabii wa kike, naye akapata mimba na baada ya muda akazaa mwana. Mungu sasa akaniambia: “Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi,

3. WAAMUZI 4:4-5 INASEMA; Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. 5 Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.

4. KITABU CHA KUTOKA 15:20 INASEMA; Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.

5. All in all, siku hizi za mwisho, Mungu aliahidi kumwaga roho yake kwa wanaume na wanawake pia. YOEL 2:28 INASEMA: Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
Asante sikuwahi kulijua hili kabla
 
kwa kuwa yule alimpata harmo na huyu naye akaamua ampate mond, wanajimaliza wenyewe hawa waimba injili tuliozipenda nyimbo zao sasa hatuna hamu nazo, tunawaona ni wahuni tu
uimbaji wenye kubadilisha moyo wa msikilizaji ni ule uliohusisha Roho Mtakatifu, yaani Roho ahusike wakati ule unaimba, ni kama vile Roho anaimba kupitia wewe na wimbo au neno lolote utakalotoa huwa lina impact kubwa kwa msikilizaji, hii ndio tofauti kubwa ya waumbaji wa kimwili na wale wanaoimba kwa Roho. sasa kweli unapiga collabo na hamonize muislam anayeamini Yesu Kristo sio Mungu na asiyeokoka na unaamini Roho Mtakatifu yupo pamoja nawe? na kwa shusho, kweli uwe kwenye fungamano moja na diamond wanaoshinda kwa waganga hao na wasiomwamini Mungu waliosambaza tabia chafu hadi kwa watoto wanawaiga, na uamini Mungu yupo pamoja na wewe? ili ukifanikiwa diamond au harmonize wacompete kuchukua utukufu na Mungu,badala ya utukufu kwenda kwa Mungu watu watasema uhusika wa hao wahuni ndio umefanya uibuke au ufanikiwe au vyovyote, mmeingiwa na nini ninyi waimbaji?

hata hivyo tunamwomba Mungu aibue wapya watakaomtumikia Mungu kwa Roho na kweli. Mungu ana watu wengi.
 
Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa amegeukia kazi ya uchungaji, mchungaji Christina Shusho, amesema aliamua kuachana na mume wake ili atimize ndoto zake. Haya sio maneno yangu bali amenukuliwa akitamka maneno hayo na mtandao wa "5newsTZ"

View attachment 2959387

"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"

"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili

MAONI YANGU namuunga mkono mchungaji kwa asilimia 100 kwani mume sio ndugu yako bali ni kama rafiki mliyekutana ili kuunda familia. Ukiona mume/mke anasababisha malengo yako yasitimie, achana naye mara moja. Nawashauri wanaume msiwe vikwazo kwenye ndoto za wake zenu. Namtakia kila la kheri mchungaji Shusho kwenye kazi yake mpya ya kueneza injili ya Bwana. Mungu ambariki sana.
Hivi Mungu yupo kweli??? any way kwasababu kutenda mema, kutoa sadaka , fungu la kumi na kuhudhulia kanisani kunanipa amani ya moyo. acha niendelee kuwa hivyo but swala la kuwepo Mungu sidhani.
 
Ule muda wa maji na mafuta kujitenga umefika
Maono ya mwanandoa yeyote ni kuhakikisha ndoa inadumu
 
Nasibu we endelea kujilia hiyo mbegu ya kirundi bana, hujala cha mtu! Hata ukipiga deki ni msafi.

Nakushukuru eeh Mungu kwa kunifanya niwe mfuasi wa Yesu Kristo (JOSHUA) katika kila jambo.
...Sipendi mafungamano na mwanamke ili asimiliki nafs yangu na kunifunga hatamu, lakin nawahitaji sana( Joshua alipenda hii life style ya kunywa na kula na pisi za nyakati mpaka wafuasi wake wakaanza kusutwa kwamba wako na mhuni. Alimpenda sana Maria Magdalena kwa philia love. (Hata kitendo cha mwanamke kumsafisha kwa nywele laini zenye olive kilimpendeza mno akamfutia dhambi!)
Ukitaka kufurahia uwepo wa mwanamke usimtongoze! Ngono huua urafiki, huzaa chuki na mipaka.
...Napenda mvinyo katika utulivu( hasa mziki laini wa rhumba) huku nikiongea mambo mema/mazuri na ya kutiana nguvu na rafik wachache waletao furaha katika uwepo wao.(Joshua, muujiza wa kwanza ulkuwa kubadirisha maji taka kuwa divai ili watu wanywe na kufurahi, alipenda stori na watoza ushuru na watu wenye maongezi yenye tija....
Ikumbukwe wanasiasa si kati ya watu hao, hakuwapenda kabsa)

Nasisitiza: NDOA NI SADAKA! KAMA HAUKO TAYARI KUPOTEZA KWA AJIRI YA MWINGINE ACHANA NAYO!
 
Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa amegeukia kazi ya uchungaji, mchungaji Christina Shusho, amesema aliamua kuachana na mume wake ili atimize ndoto zake. Haya sio maneno yangu bali amenukuliwa akitamka maneno hayo na mtandao wa "5newsTZ"

View attachment 2959387

"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"

"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili

MAONI YANGU
Mimi namuunga mkono mchungaji kwa asilimia 100 kwani mume sio ndugu yako bali ni kama rafiki mliyekutana ili kuunda familia. Ukiona mume/mke anasababisha malengo yako yasitimie, achana naye mara moja. Nawashauri wanaume msiwe vikwazo kwenye ndoto za wake zenu. Namtakia kila la kheri mchungaji Shusho kwenye kazi yake mpya ya kueneza injili ya Bwana. Mungu ambariki sana.
Kwanini asingetimiza kwanza ndoto zake ndio aolewe? kama hapendi kuitwa mchungaji kwanini ameanzisha kanisa la nini? na kwakuwa ameanzisha kanisa anapendwa tumuite nani?
 
Back
Top Bottom