Interlacustrine R
JF-Expert Member
- Jan 22, 2022
- 7,186
- 14,274
Kumbe wewe ndiwe Tapeli uliyeimba nyimbo ya "Adamu"kwenye albamu yako ya Utukumbuke kuthibitisha ndoa iliyoasisiwa na Mungu afu unajipinga mwenyewe?Alivyotangaza habari za ufufuo wa Yesu...
Tena alikuwa na macho ya Rohoni...
Maana hata hao mitume wengine hawakuwa na macho ya Rohoni, ni Petro tu alimjua kuwa Yesu ni nani...
Mariam Magdalene mwanamke ambaye alikuwa wa kwanza kutanganza injili ya ufufuo wa Yesu...
Nabii gani wa Mungu ambaye hakuwa na macho ya rohoni ilihali kazi ya Roho Mtakatifu ni kumuongoza Nabii wa Mungu kwa kila jambo kiinjili?
2 PETRO 1:19-21.
[19]Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
[20]Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
[21]Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
2 TIMOTHEO 3:16-17.
[16]Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
[17]ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Unathubutu vipi kukashfu Manabii wa Mungu hawakuwa na ufunuo wa Roho Mtakatifu ilihali neno la Mungu ni kweli?
YOHANA.
[14]Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
[24]Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.