Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa amegeukia kazi ya uchungaji, mchungaji Christina Shusho, amesema aliamua kuachana na mume wake ili atimize ndoto zake. Haya sio maneno yangu bali amenukuliwa akitamka maneno hayo na mtandao wa 5newsTZ.
View attachment 2959387

"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"

"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili

MAONI YANGU
Mimi namuunga mkono mchungaji kwa asilimia 100 kwani mume sio ndugu yako bali ni kama rafiki mliyekutana ili kuunda familia. Ukiona mume/mke anasababisha malengo yako yasitimie, achana naye mara moja. Nawashauri wanaume msiwe vikwazo kwenye ndoto za wake zenu. Namtakia kila la kheri mchungaji Shusho kwenye kazi yake mpya ya kueneza injili ya Bwana. Mungu ambariki sana.
Katika maisha haya nimejifunza kwamba unaweza kuwa na karama au kipaji purely but kipaji na tabia ni vitu viwili tofauti.... Ndomana imeandikwa kila neno atakalolifanya mwanadamu chini ya jua atatoa hesabu..... Pia watasema tulikuwa wachungaji, manabii, waliimu na tuliponya kwa jina lako naye atasema ondokeni kwangu mimi siwatambui......
 
Ndoa sasa hivi hazina thamani kabisa, hata hao wanawake wenyewe hawataki tena kuzaa Kwa uchungu wanataka kuzaa Kwa oparesheni.

Haya sasa hawa ndio tuwaite wacha Mungu hali iko hivi, vipi Sisi tusioujuwa hata mlango wa kanisa?

Mungu atusaidie tu.
 
Hiyo ndio nature ya mwanamke ninayoifahamu, huyo jamaa ashukuru huyu hata alikuwa amejificha kwenye kivuli cha dini vinginevyo huyo jamaa angekuwa futi sita chini muda huu, huku bibie akibaki na siri yake moyoni.

Kama unapanga mipango yako then ukamuweka mwanamke kwenye ramani 90% utakwama, nafasi ya mwanamke ni jikoni, ukimleta sebuleni lazima akumalize
 
Sawa mama umeamua kuwa mchungaji, sasa utakuwa mchungaji wa namna gani usiye na ushuhuda mzuri wa ndoa? Waumini wako watakuwa kama wewe mchungaji wao, hawatakuwa na utii kwa waume zao, watakuwa ni wakaidi kutaka ndoto zao zitimie nje ya ndoa
Kama Masanja ameweza kuwa Mchungaji hilo siyo tatizo hata kidogo.

Ila watu wanapaswa kuelimishwa hayo siyo Makanisa (Churches) bali ni huduma (Ministries).
 
Hiyo ndio nature ya mwanamke ninayoifahamu, huyo jamaa ashukuru huyu hata alikuwa amejificha kwenye kivuli cha dini vinginevyo huyo jamaa angekuwa futi sita chini muda huu, huku bibie akibaki na siri yake moyoni.

Kama unapanga mipango yako then ukamuweka mwanamke kwenye ramani 90% utakwama, nafasi ya mwanamke ni jikoni, ukimleta sebuleni lazima akumalize
Taliban ndio wanaijuwa nafasi ya mwanamke Kwa usahihi.

Shida zote hizi zimeletwa na Wamagharibi.
 
Back
Top Bottom