Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Ukishamjua YESU kila kitu unaona kawaida, kiu ya kutaka kumjua zaidi ni zaidi ya kiu ya maji...

Tunaweza ona Christina alifurahi kumuacha mumewe ila hakufurahi, ila Yesu akikuita utamfuata tu...

Sio rahisi haya mambo kama watu wanavyodhani...

Fikiria vile Maria alivyopata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu alafu alikuwa na mchumba wake Yusufu...

Yusufu alitaka kumuacha kwa Siri Mariamu ila akapata maelekezo kwa Mungu hakumuacha...

Mambo ya Rohoni zaidi
Umeandika ujinga
 
hawezi kuwa mchungaji, mume wake alihangaika kumpeleka hata chuo cha uchungaji dodoma pale, akasoma miezi kadhaa akaacha. siku hizi huwezi kuwa mchungaji kama hauna cheti cha kisomo kuwa mchungaji. nadhani ndio maana hataki kuwa mchungaji. hata huduma yake kama wakifuatilia watajua ipo kimakosa,labda kama kanunua cheti au amesoma online au kisirisiri. wanaomjua wanajua wanalijua hili.
Kuna uchungaji wa kusoma na uchungaji wa kuitwa na Mungu mwenyewe.
 
Kuna uchungaji wa kusoma na uchungaji wa kuitwa na Mungu mwenyewe.
tunaongelea uchungaji hapa Tanzania, tangu mbarikiwa atibue mambo, hauwezi kusajili kanisa au hata kuitwa mchungaji wa kupata leseni ya kufungisha ndoa kama huna cheti. uliza walioenda kusajili watakuambia hili. although technically, uchungaji hautakiwi kuwa wa kusomea, unatakiwa uwe wa kuitwa na Mungu, wapo wachungaji wakubwa sana walishapita duniani hawakuwa wasomi.
 
Ukishamjua YESU kila kitu unaona kawaida, kiu ya kutaka kumjua zaidi ni zaidi ya kiu ya maji...

Tunaweza ona Christina alifurahi kumuacha mumewe ila hakufurahi, ila Yesu akikuita utamfuata tu...

Sio rahisi haya mambo kama watu wanavyodhani...

Fikiria vile Maria alivyopata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu alafu alikuwa na mchumba wake Yusufu...

Yusufu alitaka kumuacha kwa Siri Mariamu ila akapata maelekezo kwa Mungu hakumuacha...

Mambo ya Rohoni zaidi
Kwamba unamwacha mume Ili ukashirikiane na mondi kuandaa matamasha?
 
Asirudi kuanza kulialia..!!
Unapoolewa au unapoowa, kuna mambo utayaacha. Sasa yeye alitaka aendelee na mambo yake kama bachela..!!?? Atoe ujinga wake..!!!

Katika vitu vinayowashinda wanawake, baadhi ni hivi;

1. Umaarufu
Wengi wa wanawake maarufu ndoa zao zina shida sana. Huwa wakishakuwa maarufu wanaona ndoa ni utumwa. Anataka awe popote muda wowote. Hii inakwenda hadi namna anavyowalea watoto wake.

2. Fedha
Mwanaume, anaweza akaishi na mwanamke asiye na kitu kwa maisha yao yote, lakini kwa wanawake walio wengi mwenye hela kuishi na mwanaume asiye na kitu, ikizidi sana wiki..!!

3. Cheo
Kuwa na cheo nako baadhi ya wanawake wameshindwa kujizuia kuwanyanya waume zao kwa vyeo vyao.

Huyu umaarufu tu unamsumbua..!!
Hayo yote wanayoringia ni ujana tu ,huo umaarufu kuna kipind unaisha kabisa maana hata mvuto unatoweka.

Walikuwepo wakina Luiza Mbutu kweny dansi wapo wapi sasa? Washakuwa wazee hata kupiga picha ni mtihani.

Ujana unapita tu ,wengi waliamua kutulia na kuolewa ila wana pesa zao maana mda wa kuringa hautakuwepo tena .
 
Kwamba unamwacha mume Ili ukashirikiane na mondi kuandaa matamasha?
atuambie, tendo la ndoa kwa umri wake huu, anafanya na nani? na tunamwona anazungukwa na vijana watanashati, kina diamond na wenzake. au hana hamu kabisa? manake sisi tuliookoka huwa tunafanya tendo kwenye ndoa tu, yeye anapomwacha mumewe ambaye ndiye mwenye haki kumfanya, anafanya na nani?
 
hawezi kuwa mchungaji, mume wake alihangaika kumpeleka hata chuo cha uchungaji dodoma pale, akasoma miezi kadhaa akaacha. siku hizi huwezi kuwa mchungaji kama hauna cheti cha kisomo kuwa mchungaji. nadhani ndio maana hataki kuwa mchungaji. hata huduma yake kama wakifuatilia watajua ipo kimakosa,labda kama kanunua cheti au amesoma online au kisirisiri. wanaomjua wanajua wanalijua hili.
Kuna chombo kinachofuatilia kama ana cheti au hana?.
 
Acha samaki wavuliwe, ni njia tu ya kuwafikia watu wa Mungu...

Acheni kuhukumu watu...

Hata Yesu hakuna kwaajili ya wasio na dhambi alikuja kwaajili ya wenye dhambi.
YESU kamwe hawezi kukuita na kukuelekeza uachane na mumeo ambaye ni mtumishi wa Mungu.

Huyo hayo anayoongea ni dalili ya makubwa zaidi yanakuja ya kulichafua Kanisa.

Ameshakengeuka huyo.
 
Nazikubali sana nyimbo zake huyu.
nyimbo zake nzuri sana, na alikuwa na karama hiyo mno, ajabu shetani kwasababu hapendi aendelee kuhudumia mioyo ya watu, amemwingia na anataka kumteketeza kabisa kipawa chake alichopewa na Mungu pamoja na yeye. hatajua hili hadi yamkute, Mungu amsaidie aelewe. kiburi na jeuri iliyomjaa anahitaji kuombewa, wala sio yeye, amepagawa. wenye macho ya kiroho wanajua hili. hakuna aliyepandisha mabega baada ya kuinuliwa ambaye hajawahi kushushwa kwa aibu.
 
Back
Top Bottom