Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Hamna mtu anayeweza muelewa Christina kwakuwa ukiitwa na Mungu Kuna vitu unatakiwa uache ..

Hata wanafunzi wa Yesu waliacha hata kazi wakamfuata Yesu...

Mambo ya Rohoni na mwilini ni tofauti kabisa...
Kuna Mahali YESU aliteua mtume mwanamke?

Na mitume wote wa YESU hatusomi popote kuwa walivunja NDOA zao.

Walienda kutumika, na walirudi Kwa wake zao.
 
Asirudi kuanza kulialia..!!
Unapoolewa au unapoowa, kuna mambo utayaacha. Sasa yeye alitaka aendelee na mambo yake kama bachela..!!?? Atoe ujinga wake..!!!

Katika vitu vinayowashinda wanawake, baadhi ni hivi;

1. Umaarufu
Wengi wa wanawake maarufu ndoa zao zina shida sana. Huwa wakishakuwa maarufu wanaona ndoa ni utumwa. Anataka awe popote muda wowote. Hii inakwenda hadi namna anavyowalea watoto wake.

2. Fedha
Mwanaume, anaweza akaishi na mwanamke asiye na kitu kwa maisha yao yote, lakini kwa wanawake walio wengi mwenye hela kuishi na mwanaume asiye na kitu, ikizidi sana wiki..!!

3. Cheo
Kuwa na cheo nako baadhi ya wanawake wameshindwa kujizuia kuwanyanya waume zao kwa vyeo vyao.

Huyu umaarufu tu unamsumbua..!!
Kiufupi mwanaume ndiye aliyepewa jukum la kutawala au kuongoza au mamlaka kwaiyo kwasababu ni kitu kipo ndani yake hakiwezi kumvua utu wake na kwa mwanamke ni kinyume chake.
 
Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa amegeukia kazi ya uchungaji, mchungaji Christina Shusho, amesema aliamua kuachana na mume wake ili atimize ndoto zake. Haya sio maneno yangu bali amenukuliwa akitamka maneno hayo na mtandao wa "5newsTZ"

View attachment 2959387

"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"

"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili

MAONI YANGU

Mimi namuunga mkono mchungaji kwa asilimia 100 kwani mume sio ndugu yako bali ni kama rafiki mliyekutana ili kuunda familia. Ukiona mume/mke anasababisha malengo yako yasitimie, achana naye mara moja. Nawashauri wanaume msiwe vikwazo kwenye ndoto za wake zenu. Namtakia kila la kheri mchungaji Shusho kwenye kazi yake mpya ya kueneza injili ya Bwana.

Mungu ambariki sana.
Kwa hiyo kanisa lake litakuwa la ma single mom pekee!
 
Ameshakichuna kibabu cha watu sasa anaropoka kama anaharisha.Anzisha kanisa tuje kuabudu sintaacha kufika ibada hata siku moja na mkoba wako nitaubeba mimi nitakuwa karibu yako hadi ushangae kipenzi, alisikika muumini mmoja
 
Back
Top Bottom