Watu wengi huwa wanashangaa kwanini watu maarufu wanawindwa sana na shetani. ukienda kwenye dunia, hata hao mafreemasons, au cult zozote zile, huwa zinapenda sana kuwachukua watu maarufu, kwasababu shetani akiwaingia impact yao kwa wanadamu inakuwa kubwa,shetani anavuna matunda mengi. mfano, diamond tu na wengine wanamuziki wa marekani, nyimbo zao zinachafua sana nafsi za watu na kufungua milango shetani kuingia kwao, na kwa watoto pia.
ukija kwa waliookoka na ni maarufu, shetani atawinda sana ndoa zao au hata maisha yao awadondoshee kwenye uzinzi au dhambi inayokera kwa macho ya kibinadamu, na anguko lao linaondoka na kundi kubwa sana la watu waliokuwa wanawafuatilia. shusho mfano, ana wafuasi wengi kwa sababu ya nyimbo zake, akifanya chochote cha ajabu mioyo ya wengi itarudi nyuma na kuona walikuwa wanafuata kisicho sahihi, na yeye atalipa garama hiyo mbele za Mungu. ukikabidhiwa uwakala wa chochote na Mungu hakikisha unakilinda kisilete negative impact kwa wanadamu.
hatutakiwi kumpiga mawe weee, ila tunatakiwa kumwombea Mungu amrehemu, na akishupaza shingo yake, yeye mwenyewe atarudi na kukiri kwamba alipotea baada ya kukutana na aliyemwita awali.