Chuki dhidi ya January Makamba inatoka wapi?

Mengi tu ikiwemo kukomesha matumizi ya mifuko ya Plastics nchini jambo ambalo ni la kihistoria na lilikuwa mzigo kwa Taifa.
Hilo ni magufuli ndo alofanikisha Hana zuri lolote ndomana anakulipeni chawa km ww na waganga kiumsafishia njia ya kupata madaraka zaid
 
Chuki dhidi ya Jan Makamba inathibitisha msemo "hasidi hana sababu".
1. Hivi kukiwa na ukame mabwawa ya kufua umeme yakakosa maji na njaa ikaingia waziri wa nishahti na waziri wa kilimo walaumiwe?
2. Ikiwa ni kweli January aliiba mtihani zaidi ya miaka 30 iliyopita, apewe hukumu ya maisha asipate cheo chochote? Wewe unayekomalia kosa la wizi wa mtihani u mtakatifu kiasi gani?
3. Kuhusu level ya elimu hivi unajua katika mawaziri wakuu 57 wa UK hadi Oct.2022 zaidi ya 75% wamepitia vyuo vya Oxford na Cambridge, lakini Winston Churchill ndiye Waziri Mkuu aliyeokoa Uingereza katika vita Kuu ya pili-WWII? Huyu Churchill hakuwa na hata A level. "W.Churchill saved Britain in its darkest hour." Kwenye siasa elimu ni muhimu lakini kuna sifa nyingine muhimu zaidi.
4. Hivi waziri wa nishahti wajibu wake ni Tanesco tu, na awe anavunja bodi ya Tanesco kila umeme unapokatika katika?
Chawa
 
January Makamba, mtoto wa Katibu Mkuu mstaafu wa CCM amekuwa akiandamwa katika mitandao mingi ya kijamii na kujaribu kuaminisha umma ya kuwa ni mtu hafai katika uongozi.

Binafsi Makamba nilimuona wakati wa utawala wa Kikwete akiwa ni mmoja wapo wa wasaidizi wa Rais Kikwete.

Mwenye ushahidi wa wazi kuhusu mabaya yake atuwekee hapa ingawa mimi namuona ni mtu humble, focused na mwenye uvumilivu.
Wagalatia ndo wanaomchukia January makamba
 
Ukweli ni kwamba sio kiongozi mmbaya, ila wanampa majukumu yaliyo juu ya uwezo wake.

Makamba is overly ambitious to change the world, shida ni kwamba uelewa wake ni mdogo sana to how things work, kutofautisha mfuko wako na huko unapotaka kukopi mambo, njia sahihi ya kufikia hiyo hazma.

Kupitia nishati ameonyesha huyu sio mtu wa kuaminiwa na kupewa sensitive posts za maamuzi he is a liability. Anafaa kwenye wizara ya muungano, utumishi na kwengineko ambapo ubunifu wake hatari kwa uchumi autumiki.
 
January yupo kwenye Vita tangu aingie 5 bora Urais 2015.

Anaonekana ni threats kwa wenzake kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Ujao.

Wapo wanaotoa hoja kuwa hana Uwezo wa kuongoza ndiyo maana Wizara kadhaa alizoziongoza zimemshinda.

Kitu ambacho hawajui kuwa, Urais wa Tanzania sio kazi ya kubeba Zege kwamba inahitaji Ubaunsa.

Rais ni Taasisi, ndani ya Urais kuna Mainjinia, Madaktari, Wanasheria, Maafisa Mipango, Wachumi n.k
Ni suala la mifumo kuachwa kufanya kazi.

Then yeye anachotakiwa kuwa nacho ni Ujasiri tu wa kufanya maamuzi kama alivyokuwa Ben Mkapa ama JPM lakini kwa kufuata Sheria na Katiba ya Nchi.

Hata mwenye Kidato cha Nne anaweza kuongoza Nchi hii iwapo ataacha mifumo iwe inafanya kazi.

=======
Tatizo la Nchi hii sio January, Mwigulu ama Biteko

Kama CCM itaendelea kuongoza Nchi hii hata aje Mtume M.S.W ama Yesu Kristo wa Nazareth kuongoza kupitia Chama hicho basi nao hawatatufaa
Hiyo 5 BORA ilikuwa ni majina tu ya mfukoni ya kumsindiikza chaguo la Mkapa, Magufuli.

Wakaweka kijana mmoja (Makamba), wanawake wawili na Membe na Mhusika Magufuli.

HAYO MAJINA HAYAKUPATIKANA KWA KUPIGIWA kura.
 
Chuki dhidi ya Jan Makamba inathibitisha msemo "hasidi hana sababu".
1. Hivi kukiwa na ukame mabwawa ya kufua umeme yakakosa maji na njaa ikaingia waziri wa nishahti na waziri wa kilimo walaumiwe?
2. Ikiwa ni kweli January aliiba mtihani zaidi ya miaka 30 iliyopita, apewe hukumu ya maisha asipate cheo chochote? Wewe unayekomalia kosa la wizi wa mtihani u mtakatifu kiasi gani?
3. Kuhusu level ya elimu hivi unajua katika mawaziri wakuu 57 wa UK hadi Oct.2022 zaidi ya 75% wamepitia vyuo vya Oxford na Cambridge, lakini Winston Churchill ndiye Waziri Mkuu aliyeokoa Uingereza katika vita Kuu ya pili-WWII? Huyu Churchill hakuwa na hata A level. "W.Churchill saved Britain in its darkest hour." Kwenye siasa elimu ni muhimu lakini kuna sifa nyingine muhimu zaidi.
4. Hivi waziri wa nishahti wajibu wake ni Tanesco tu, na awe anavunja bodi ya Tanesco kila umeme unapokatika katika?
Nina swali moja tu, Wakati wa awamu ya Tano Dr Kalemani aliwezaje kufanya umeme usikatike katike akiwa Waziri wa Nishati?
 
January Makamba, mtoto wa Katibu Mkuu mstaafu wa CCM amekuwa akiandamwa katika mitandao mingi ya kijamii na kujaribu kuaminisha umma ya kuwa ni mtu hafai katika uongozi.

Binafsi Makamba nilimuona wakati wa utawala wa Kikwete akiwa ni mmoja wapo wa wasaidizi wa Rais Kikwete.

Mwenye ushahidi wa wazi kuhusu mabaya yake atuwekee hapa ingawa mimi namuona ni mtu humble, focused na mwenye uvumilivu.
Anatembea na laana. Alitengeneza mchongo wa kuiba hela enzi zile mazingira Dkt Magu akiwa nje ya nchi, lilivyobumbuluka basi akafukuzwa. Hakujifunza huyu mwizi na alipopewa nafasi na Dkt Samia tena akaanza sherehe ya kujifanya eti wizara iliendeshwa kwa hasara na akajifanya kumleta maharage na matokeo yake akawa ameharibu kabisa
 
Mengi tu ikiwemo kukomesha matumizi ya mifuko ya Plastics nchini jambo ambalo ni la kihistoria na lilikuwa mzigo kwa Taifa.
Hilo lilikuwa ni agizo la Serikali na aliyetoa hiyo amri ni Waziri Mkuu Majaliwa.Labda tu kukujuza kidogo,palifanyika maandalizi makubwa sana ya wadau waliokuwa wanatumia mifuko ya plastick kama viwanda vya kutengeneza pombe za Spirits (viroba) na wadau wa uzalishaji wa mifuko hii ya kubebea bidhaa.Hilo zoezi liliratibiwa kwa ukaribu sana na Ofisi ya Waziri Mkuu.Makamba alishiriki sawa akiwa Waziri wa Mazingira lakini credit ya ukomeshaji wa mifuko ya plastick apewe Mh.Majaliwa.
 
Hilo ni magufuli ndo alofanikisha Hana zuri lolote ndomana anakulipeni chawa km ww na waganga kiumsafishia njia ya kupata madaraka zaid
Na mratibu mkuu wa zoezi alikuwa ni Waziri Mkuu Majaliwa.
 
Hiyo 5 BORA ilikuwa ni majina tu ya mfukoni ya kumsindiikza chaguo la Mkapa, Magufuli.

Wakaweka kijana mmoja (Makamba), wanawake wawili na Membe na Mhusika Magufuli.

HAYO MAJINA HAYAKUPATIKANA KWA KUPIGIWA kura.
Huenda ilikuwa hivyo

Mtandao umeshaandaliwa kuhakikisha hawa Vijana wanawekwa pale Juu, ndiyo maana wengine wamewekwa jikoni OR kuendelea kupata info zote za Nchi ku-monitor situations
 
Anatembea na laana. Alitengeneza mchongo wa kuiba hela enzi zile mazingira Dkt Magu akiwa nje ya nchi, lilivyobumbuluka basi akafukuzwa. Hakujifunza huyu mwizi na alipopewa nafasi na Dkt Samia tena akaanza sherehe ya kujifanya eti wizara iliendeshwa kwa hasara na akajifanya kumleta maharage na matokeo yake akawa ameharibu kabisa
Blah blah zilikuwa nyingi mno hapo mwanzoni anakabidhiwa Wizara.Kila siku ni kunanga namna awamu ya tano ilivyoiendesha Wizara na shirika la TANESCO.Kaongea wee mwisho uwongo wote ukamuishia akaikimbia na twitter.Mungu alivyo wa ajabu,akamuumbua na hali ikawa inazidi kuwa mbaya mpaka tumetumbukia kwenye mgao rasmi.Nasubiri nione na mteule wake Maharage kama bado ataendelea kuwa pale TANESCO.
 
Nina swali moja tu, Wakati wa awamu ya Tano Dr Kalemani aliwezaje kufanya umeme usikatike katike akiwa Waziri wa Nishati?
Kwanza suala la upatiikanaji umeme kwa uhakika ni muhimu mno kuwa jukumu la mtu mmoja. Linahusu uchumi na usalama wa nchi.
Siamini watendaji wa Tanesco walikuwa wanamhujumu Jan Makamba na taifa baada ya kuondoka Mhe. Kalemani.
Mwisho ndio kusema Kalemani angekuwepo mwaka 2006
Tz ilipokumbwa na tatizo kubwa la kihistoria la umeme (na kashfa ya Richmond)yeye angeweza kuliepusha?
 
Wewe ushakaa Gizani na kusumbuliwa na mgao wa Giza na kupewa majibu ambayo hayana maana ?

Hizi kazi watu hawatafuti wachumba wala marafiki..., wanatafuta utendaji wala hii sio Hisani wanalipwa ili wafanye kile kinachokusudiwa sasa ukiona pesa zako zinatapakazwa utampenda mtapakazi....
 
Kwanza suala la upatiikanaji umeme kwa uhakika ni muhimu mno kuwa jukumu la mtu mmoja. Linahusu uchumi na usalama wa nchi.
Siamini watendaji wa Tanesco walikuwa wanamhujumu Jan Makamba na taifa baada ya kuondoka Mhe. Kalemani.
Mwisho ndio kusema Kalemani angekuwepo mwaka 2006
Tz ilipokumbwa na tatizo kubwa la kihistoria la umeme (na kashfa ya Richmond)yeye angeweza kuliepusha?
Hujajibu swali Mkuu,nimeuliza tu Kalemani na uongozi wa TANESCO uliokuwepo awamu ya Tano uliwezaje kufanikiwa upatikanaji wa umeme kwa uhakika.Kumbuka tunaongelea kipindi cha miaka 5?
 
January Makamba, mtoto wa Katibu Mkuu mstaafu wa CCM amekuwa akiandamwa katika mitandao mingi ya kijamii na kujaribu kuaminisha umma ya kuwa ni mtu hafai katika uongozi.

Binafsi Makamba nilimuona wakati wa utawala wa Kikwete akiwa ni mmoja wapo wa wasaidizi wa Rais Kikwete.

Mwenye ushahidi wa wazi kuhusu mabaya yake atuwekee hapa ingawa mimi namuona ni mtu humble, focused na mwenye uvumilivu.
Watanzania ni wivu na woga ndio unawatesa. Ila yule jamaa ana ngozi ngumu sana hana muda nao. Ndio kwanza amepewa wizara kubwa zaidi. Yule jamaa ana maono makubwa sana. Watanzania hawajapendaga mtu smart watamzushia mauwongo mengi.
 
Kampeni za mitataoni zinaendeshwa na genge moja linalotaka urais. Wanamuona January Makamba kama tishio. Hivyo wanataka kumdhoofisha kwa kuwaaminisha watu kuwa hafai. Na wengine wanafuata mkumbo bila kujua kilichoko nyuma ya hizo tuhuma.

January ni presidential material.
Mitataoni
 
Back
Top Bottom