Chuki dhidi ya January Makamba inatoka wapi?

Chuki dhidi ya January Makamba inatoka wapi?

No, siyo kwamba anachukiwa. Watu wenye akili wanajaribu kupima hivi vyeo anavyopata haraka namna hiyo ni kweli anavistahili au ni kwa vile baba yake ndio watawala wa nchi hii! Tukichukua vyeti vyake vya shule, je anaufaulu outstanding to deserve such accelerated promotions to those levels?

Sawa na Ridhiwani Kikwete, amepata ubunge siyo kwa vile alishindanishwa, ni kwa vile influence ya baba yake played the whole part. Kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, siyo kwa vile ana merit ya kuwa pale, ni influence ya baba yako!

Sawa na NAPE, ana sifa kweli za kuwa pale? Mtu Form four failure, tena div 4 point 30! Huyu ataandamwa kwa vile yuko pale kwa kujuana, siyo merit!
Div 1 ndio inakufanya kuwa Kiongozi? Waziri ni mtaalamu kwamba anaenda kufanya mahesabu? Kumbe chuki binafsi tuu.
 
Makamba ni moja viongozi wabovu akifuatiwa na mwigulu angekuwa nje ya mfumo tungekuwa tushamsahau mda mrefu ni mfumo tu wakifamilia unaomlinda

Tanesco hiyo imemshinda pamoja na kupewa pesa nyingi za maboresho na mama lakini migao imeendelea

Mpaka hapa haujiulizi mtangulizi wake aliwezaje hyo wizara
Tanesco imemshindaje ,eleza
 
Haijalishi kuwa wewe ni Dogo, Braza au Dingi, au Kikongwe.... Cha msingi jua kuwa Mzee wa Chato alikuwa Rais bora, imagine miaka 5 tu, Bongo ilianza kutoka kwenye ubongonyoso, tukaanza kuingia kwenye ubongoraha... Tukaanza kuwa Recognized, Watalii wakaanza kutua, Miradi ikaanza kutembea, Serikali ikaamia Dodoma, Treni ya SGR na Bwawa la umeme likaanza kujengwa, Daraja refu Afrika mashariki pale mwanza, Meli kubwa ziwa Victoria, MV hapa kazi tu... Rushwa ilianza kupotea maana, mchizi wangu mmoja naye alikamatwa kwa rushwa, ata mwananchi wa kawaida akaanza kuheshimika... Yule mwamba apumzike tu... Ukipinga huu ukweli, wewe unatakiwa ukapimwe akili uenda akili zako ni moja kasoro robo
Kamfuate kaburini ukamwimbie hizo sifa za kijinga
 
Katuibia sana huyu jamaa.

Dada yake pale Kwa Madiba ndio mtunza fedha, akiiba tu anazirusha pale.

Pili; Siasa za baba yake pia zinamuharibia.

Tatu; huyu mwamba amefanya figisu nyingi sana enzi za utawala wa JPM; hujuma zake zilikuwa za kishenzi. Hafai hata kuwa kwenye ofc ya umma.

Nne; ni ntu wa dili; hafanyi jambo bila rushwa. Ofc yoyote anayoingia lazima alambe dili ndio akili ikae sawa.

Tano; Anajiona kama yeye ndio mwenye hii nchi peke yape; Pamoja na Nape wake. Hawa Wawili ni wa kuchunga sana. Hawana maana na nchi yetu
Wewe umekatazwa Kuiba? Kwa nini dada yako nae asiwe mtunza pesa?

Kwani JPM wako ni nani Hadi asifanyiwe figisu? Mbona huyo unaemtetea sio tuu amefanya hujuma Kwa wenzie Bali amekatisha Uhai wao,yupi ni binadamu kati Yao wawili?

Wewe unanifahamu Dili gani ambako analifanya? Kufanya Dili Kuna shida gani? Wewe umekatazwa kufanya Dili?

Kujiona ndio kukoje au wewe ndio unaona hivyo? Unaweza thibitisha?
 
Hakuna chuki, Watanzania wote Hawa hawawezi kumchukia makamba. Lazima kuna Shida sehemu. Why always makamba?? Jibu ni Hafai na Hafai Tena kuongoza wizara zetu
Watanzania wote wapi wanamchukia au nyie misukule ya Mwendazake? Lazima mumchukie maana alikuwa anampa spana za kutosha Jiwe
 
Binafsi nilikua namuamini sana kipara ila ishu ya kreni bwawa la Nyerere ndio iliyonikata stimu,, jamaa janja janja nyingi sana huyu
Kama issue ni crane,vipi Jiwe aliyekuwa anadanganya Wasiwasi? Tunajenga Kwa pesa zetu kumbe matilioni ya mikopo ya kibiashara
 
January ni miongoni mwa viongozi bora sana tulionao kama nchi. Makelele unayosikia dhidi yake, ambayo haya ushahidi, ni kutoka kwa wasaka urais (wa baadae) ambao wanamuona tishio.

Pia, mimi naamini makelele hayo (hasa mitandaoni) ni moja ya mikakati wa baadhi ya vyama vya upinzani kushambulia vijana (viongozi watarajiwa) wa chama tawala, kama njia ya kuimarisha mbio zao za kusaka kushika dola. Inaonekana kama vile vijana wowote wa chama tawala wenye muelekea wa kuwa viongozi wakuu hapo baadae (January, Mwigulu, Kitila, Nape n.k.), lazima wasakamwe na kuchafuliwa hata bila ushahidi wala hoja za msingi.
Una uwezo mdogo wa kufikiri kama Makamba
 
Haijalishi kuwa wewe ni Dogo, Braza au Dingi, au Kikongwe.... Cha msingi jua kuwa Mzee wa Chato alikuwa Rais bora, imagine miaka 5 tu, Bongo ilianza kutoka kwenye ubongonyoso, tukaanza kuingia kwenye ubongoraha... Tukaanza kuwa Recognized, Watalii wakaanza kutua, Miradi ikaanza kutembea, Serikali ikaamia Dodoma, Treni ya SGR na Bwawa la umeme likaanza kujengwa, Daraja refu Afrika mashariki pale mwanza, Meli kubwa ziwa Victoria, MV hapa kazi tu... Rushwa ilianza kupotea maana, mchizi wangu mmoja naye alikamatwa kwa rushwa, ata mwananchi wa kawaida akaanza kuheshimika... Yule mwamba apumzike tu... Ukipinga huu ukweli, wewe unatakiwa ukapimwe akili uenda akili zako ni moja kasoro robo
Upumbavu,limtu limekaa miaka 6 hakuna hata mradi limekamilisha.

Samia is way better off than Jiwe Kwa angles zote.

Unataka vimiradi vya kukurupuka ambavyo vilimshinda achilia mbali kuharibu uchumi na maisha ya watu.
 
Mkuu na pale wami daraja jipya likajengwa chaap na roho za umauti zikakoma kuwaandama madereva wa malori na mabasi na abiria wao.
Huwa nawashangaa sana nyie watu wajinga wajinga,ukiacha kuanzisha , Mwendazake alikamilisha miradi ipi Kwa miaka 6? Alikuwa anafichia udhaifu wake Kwa Kuanzisha 😆😆
 
Binafsi simchukii, sema January bila lile jina la Makamba basi angekuwa muosha Magari au kinyozi. Mwanangu huwa ananiambia hizi kazi hazihitaji kabisa uwe intelligent.
Hizo ndio chuki zenyewe,wewe hupangi destiny ya mtu
 
Unajidanga sana kijana Makamba jr ni mmoja wa vijana wa hovyo kuwai kutokea enzi za JK walikuwa miungu watu wakifuta mtoto wa JK na nape Jr

Jecha alivyofuta uchanguzi zanzibar akaesema ccm hauwezi toka madarakani kwa njia ya karatasi
Kwani wewe unaona ccm itatoka madarakani Kwa njia ya karatasi?
 
Ngoja tuone sasa iwapo tatizo la kukatikakatika kwa umeme litakoma.

Tutajua tatizo lilikuwa ni mtu au mfumo mzima?!

Niko pale nasikilizia mrejesho.
Maharage Chande alishaweka clear hakuna siku umeme utaachankukatika ikiwa miundombinu ilishaoza nothing new.

January hajatolewa huko Kwa sababu za kukatika Kwa umeme Bali sababu zingine kabisaa tena za Kisiasa kuelekea 2025.
 
Hii mitoto ambayo haijui bili za umeme Wala gharama za kuunganishiwa umeme ndio inakuja na mada kama hizi huyu unaemtetea fisadi makamba katutoa kwenye umeme wa elfu ishirini na Saba mpaka laki tatu na kitu wewe kibofu wa akili huoni? Au Kwa sababu umezoea kula na kunya Bure?
Kwanza categorically it's false.


Pili mwaka jana Tanesco imeunganisha wateja laki tano kwa mwaka. First time ever.
 
Maharage Chande alishaweka clear hakuna siku umeme utaachankukatika ikiwa miundombinu ilishaoza nothing new.

January hajatolewa huko Kwa sababu za kukatika Kwa umeme Bali sababu zingine kabisaa tena za Kisiasa kuelekea 2025.
Ukiwa ccm hata kama umesoma akili za kufikili zinapungua unakuwa kama kichaa
 
Sijawahi kumkubali Huyo January makamba hata siku moja na sina alama ya kusimulia kuhusu uongozi wake zaidi ya nafasi yake kupwaya kwenye Kila WIZARA anayopewa. Kwa ufupi ni kiongozi anayewekwa kwasababu tu ya wakubwa kumwonea aibu kutokana na historical background ya familia yake. The same same to Riz1 kikwete, Nape, mwana FA, na wengine wa nafas ndogondogo za ukuu wa wilaya kama Good luck Mlinga na wengine wengi. Hawana uwezo wa Kiuongozi ila family background zinawabeba.

Kuna watu wamezaliwa kwenye familia ambazo historia zao haziwabebi kisiasa Wala Kiuchumi lakini Wana uwezo mkubwa sana wa Uongozi kiasi kwamba akipewa eneo la uongozi ndani ya mwaka mmoja tu watu wanashuhudia mabadiliko makubwa waliyodhani hayatatokea. That's all I can say.
Kama kina nani hao wenye uwezo mkubwa,mbona huwataji? Wewe au nani?
 
Chuki dhidi ya Jan Makamba inathibitisha msemo "hasidi hana sababu".
1. Hivi kukiwa na ukame mabwawa ya kufua umeme yakakosa maji na njaa ikaingia waziri wa nishahti na waziri wa kilimo walaumiwe?
2. Ikiwa ni kweli January aliiba mtihani zaidi ya miaka 30 iliyopita, apewe hukumu ya maisha asipate cheo chochote? Wewe unayekomalia kosa la wizi wa mtihani u mtakatifu kiasi gani?
3. Kuhusu level ya elimu hivi unajua katika mawaziri wakuu 57 wa UK hadi Oct.2022 zaidi ya 75% wamepitia vyuo vya Oxford na Cambridge, lakini Winston Churchill ndiye Waziri Mkuu aliyeokoa Uingereza katika vita Kuu ya pili-WWII? Huyu Churchill hakuwa na hata A level. "W.Churchill saved Britain in its darkest hour." Kwenye siasa elimu ni muhimu lakini kuna sifa nyingine muhimu zaidi.
4. Hivi waziri wa nishahti wajibu wake ni Tanesco tu, na awe anavunja bodi ya Tanesco kila umeme unapokatika katika?
Excuses za kipuuzi
 
Back
Top Bottom