January ni miongoni mwa viongozi bora sana tulionao kama nchi. Makelele unayosikia dhidi yake, ambayo haya ushahidi, ni kutoka kwa wasaka urais (wa baadae) ambao wanamuona tishio.
Pia, mimi naamini makelele hayo (hasa mitandaoni) ni moja ya mikakati wa baadhi ya vyama vya upinzani kushambulia vijana (viongozi watarajiwa) wa chama tawala, kama njia ya kuimarisha mbio zao za kusaka kushika dola. Inaonekana kama vile vijana wowote wa chama tawala wenye muelekea wa kuwa viongozi wakuu hapo baadae (January, Mwigulu, Kitila, Nape n.k.), lazima wasakamwe na kuchafuliwa hata bila ushahidi wala hoja za msingi.