CHUKI YA MAKAMBA KWA HAYATI MAGUFULI IKO WAZIWAZI.
Pamoja na kwamba hayati Magufuli alitangaza hadharani kwamba amewasamehe lakini kwa mambo yanavyoenda sasa hivi ni dhahiri Makamba na Nape waliomba msamaha kinafiki na walipokea msamaha kinafiki pia.
Makamba alipoteuliwa tu uwaziri wa nishati kazi ya kwanza ilikuwa ni kwenda kufukuza ma electrical engeneers wote pale Tanesco na alipoulizwa kwa nini unafukuza watendaji wote ? Akajibu hataki kufanya kazi na watu walioteuliwa na Magufuli!!, leo ni miaka miwili imepita lakini kila tatizo linapoibuka pale Tanesco , Makamba husema sababu ni Magufuli alilazimisha mashine kuwaka bila kufanyia service!
Chuki ya Makamba kwa Magufuli imesababisha miradi yote ya Tanesco kuzorota kwa kasi, mgao wa umeme, usambazaji umeme vijijini ni kama haupo kila kukicha ni visingizio vya kila aina.