Chukua hii: 2022 ujio wa Tundu Lissu utaleta Kimbunga

Chukua hii: 2022 ujio wa Tundu Lissu utaleta Kimbunga

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,056
Reaction score
6,208
Ujio wa TL utaleta kimbuga kikubwa mno kwa Samia hasa Tundu atakapoanza zile rabsha zake za maneno ya kukwaza lkn ya kweli.

Tundu ni mtu aliyenyooka na muwasilishaji hoja zake kwa ukali huku akijiamini kupitiliza na huwa hajali.

Samia ajiandae kuitwa majina asiyoyatarajia. Haitashangaza Tundu akimpa jina la 'ma ushungi' huku akimtweza.Kumbukeni TL alimuita Magufuli dikteta uchwara tena mchana kweupe!

Kugawanyika kwa wana CCM ni bayana. Hakutakuwa na siri tena kwenye chama na Serikali jambo ambalo kina Tundu watazipata siri nyingi za sirini na kwazo ndizo zitawasaidia kumsurubu Samia.

2022 itakuwa chungu sana kwa Samia.
 
TL atakuwa anajichimbia kaburi lake na kupotea kwenye ramani kama atamdhihaki Rais SSH.

Ikumbukwe Lissu aliposhambuliwa na risasi za kikundi cha akina Makonda, kisha kufanyiwa emergency treatment pale Dodoma Regional Hospital, alisadirishwa hadi Nairobi kwa matibabu.

Akiwa pale Agakhan hospital hakuna mwana CCM hata mmoja aliyethubutu kumtembelea pale hospitalini zaidi ya Makamu wa Rais wa wakati huo Samia Suluhu. Waliogopa kwa kuwa Magufuli hakutaka Lissu awe hai na hakutaka afarijiwe Wala kulipiwa matibabu.

Kama Lissu atamnanga Rais SSH kwa mdomo wake mchafu basi LAANA kubwa itampata kwa kukosa SHUKRANI
 
Huwa sikubaliani na wewe kwa mambo yote na kwa dharau zako sitarajii kukubaliana na wewe kwa lolote. Lakini...

...tambua Tundu anautaka u Rais wa Tanzania kwa gharama yeyote ile.

...tambua Tundu anarejea na MIKAKATI mahsusi ya namna ya kuiondoa CCM madarakani kutoka kwa wazungu na usifikiri wamewekeza kwa Tundu bure bali muda wote huo wameishi naye wakimuandaa ili aje kuchukua madaraka ili wao walichoki target iwe rahisi kukipata kwalo.

...tambua Tundu hawezi kamwe kuwa na huruma na mwana CCM/mtu yeyote aliyepo CCM kwa namna walivyomfanya.

...2022 ni mwaka mbaya sana kwa CCM kwa sababu kwanza tayari wao kwa wao wamegawanyika na wanatukanana waziwazi!
 
Back
Top Bottom