greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,060
Soko la hisa la Dar es Salaam lina makampuni 26 yaliyo jiorodhesha. Katika hayo kuna makampuni yanayofanya vibaya na yale yanayo chechemea.
Tuangalie orodha ya makampuni yaliyo na hali mbaya na uchukue tahadhari kabla ya kuwekeza.
JATU
Hili lina husika na cloud farming. Naliweka kwenye orodha kwani sijaona hawajachapisha taarifa za fedha kwa mwaka wa pili mfululizo na hata ripoti yao mwaka haipo mitandaoni.
SWALA
Kampuni inayojihusisha na utafiti wa mafuta huko kitalu cha Morogoro.
-Haijawahi tengeneza faida kwani bado haijafanikiwa kupata hayo mafuta.
-Usije nunua hisa huko mana nchi yetu haina historia kupatikana kwa mafuta.
TATEPA
Mara ya mwisho mwisho hii kampuni kuweka taarifa zake za fedha ni mwaka 2020,nimezisaka mpaka .Ilikuwa na hasara ya Billioni 4.Ikiwa na madeni mengi kuliko amana. Na sioni kama Uongozi wa bodi yake kama una hangaika kuiokoa hii kampuni.
PRECISION AIRLINE
Hii kampuni ya ndege nahisi ishajifia,mana hakuna cha maana nilicho kiona kwenye taarifa zake.
Taarifa zake za mwisho ilikuwa ni za 2019 na zilionesha ilipata hasara ya zaidi ya Billion 44.
MUCOBA
Hii Benki ya wakulima Iringa ni ipo hoi kana kwamba hata taarifa zake hazipatikaniki. Wakinga, Wabena, Wapangwa na Wahehe wekezeni kwenye Benki yenu.
ĎCB
Hii Benki ya Halmashauri ya Jiji la Dar Ina zalisha faida kiduchu, haina mawazo ya ukuaji, haitoi gawio, haiwekezi kwenye tafiti, haina mipango mipya.
Chukua tahadhari unapotaka kuwekeza kwenye haya makampuni.
Uchambuzi huu nimefanya kwa kutumia data zilizopo mtandaoni,kusoma ripoti za mwaka na kuhudhuria baadhi ya vikao vya wanalima.
Karibuni mchangie.