Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haina umuhimukwani ina tatizo gani ?
Wewe jamaa unapenda uchawi na ni mchawi haswa.
Hadi umewaroga mods thread yako imekuwa sticky!
Sishangai sana maana hata Mshana Jr. Thread zake nyingi zimekuwa sticky!
Naomba kuweka kumbukumbu sawa nina mada mbili ambazo ni sticky ya magari na ya watoto... Nyingine zoote zinakufa na kufufuka zenyewenaona hii thread haina tofauti sana na zile za mshana jr embu ngoja niangalie wemezstick. labda tofauti tu ni kwa mleta mada kutangaza contact zake.
Mimi mwenyewe nipo darasani naongeza maarifamshana jr , njoo huku utoe elimu ya chuma ulete
Nenda makaburini na kwenye miti mkubwa usiku wa manane utawapata tu.Mleta mada,
Hivi hii dunia ina viumbe wanaoitwa majini?
Kama wapo,wanapatikana wapi?
Nina shida nao sana!
nazungumzia zile mada zinazofanana na hii. kwa nini wameonelea hii iwe stick. zako kama hii ukiweka contact watastick au ....Naomba kuweka kumbukumbu sawa nina mada mbili ambazo ni sticky ya magari na ya watoto... Nyingine zoote zinakufa na kufufuka zenyewe
Hakuna hata mada moja ya mambo ya kichawi na kishirikina hapa jamvini ambayo iko sticky hivyo naona mods wameichagua hii iziwakilishe nyingine zoteh
nazungumzia zile mada zinazofanana na hii. kwa nini wameonelea hii iwe stick. zako kama hii ukiweka contact watastick au ....
Wewe ulitaka waichape ama?JamiiForums na nyie mna mambo kwa hiyo na hii nayo mmeistick....
Kwako na si kwa wote, kumbuka watu wanaoingia jf wanautofauti wa mawazo hivyo usishangae kitu kukosa umuhimu kwako na kuwa na umuhimu kwa mwingine.Haina umuhimu
elimu nzr cna.huyo.ututukanga ndo nn asee
MATANGAZO YA WAGANGA MTANDAONI KATIKA UBORA ULIOTUKUKA! ILA SINAGA IMANI NAO! HATA CHEMBE YA HARADARI! ILA!!! CJUI!Nimeshangaa sana,nilitaka kuhoji hili pia.
NDIO SABABU IKAWEKWA NAMBA YA SIMU YA MTOA MADA, ILI MIAMALA IHUSIKE ZAID. NA JINA KAMA UTUTUKANGA SIJAWI LISIKIA DUNIANI, MBINGUNI HATA JEHANUM!. WAJINGA NDIO WALIWAO CHIEF. SANUKA!hututukanga ndio nini? tusaidie hapo
elimu nzr cna.huyo.ututukanga ndo nn asee
PIGA NAMBA ALIYOYOWEKA UPIGWE KISOMI!elimu nzr cna.huyo.ututukanga ndo nn asee
Hee kazi kweli kweli,, sasa kumbe ndivyo tunavyoibiwa hivyo,, utakuta kizee kina wake zake 3 na vitoto kadhaa kwake,, hana kazi wala shamba lakini kipo kipo tu mtaani,,JINSI YA KUIDHIBITI CHUMA ULETE.
Mwandishi 😀r.Mungwa Kabili…..0744 000 473
CHANZO : ULIMWENGU USIOONEKANA: JINSI YA KUDHIBITI CHUMA ULETE
![]()
Jini wa Chuma Ulete
Kwa muda mrefu nimekuwa nikipokea simu na barua pepe kutoka kwa watu mbalimbali wakiniomba niwaelezee jinsi ya kudhibiti chuma ulete.
Chuma ulete ni uchawi ambao unarudisha nyuma jitihada za maendeleo ya watu wengi sana.
Kwa ufupi Chuma ulete ni wizi wa kimazingara ama wizi wa kichawi au wizi wa kiini macho.
Macho anayefanya wizi kwa kutumia chuma ulete anakuwa ameingia mkataba wa kiroho na jinni au majini wanao husika na wizi wa vitu na mali za watu.
Chuma ulete zimegawanyika katika makundi makuu mawili. Ya kwanza, ni Chuma Ulete katika mapenzi na mahusiano na ya pili Chuma Ulete ambayo haihusiani na masuala ya mapenzi.
Watu wengi hawafahamu kuhusu Chuma Ulete ya Mapenzi, bali wanafahamu kuhusu Chuma Ulete hii iliyo zoeleka kwa watu wengi.
Chuma ulete katika mapenzi ni pale ambapo mwanamke anamfanyia uchawi wa mapenzi mwanaume mwenye kipato na kumfanya mwanaume huyo awe anampa mwanamke huyo pesa na mali zake zote. Zoezi hilo litaendelea mpaka mwanaume huyo atakapo filisika.
Chuma ulete hii hufanywa zaidi na wanawake, lakini wapo pia wanaume wanao jihusisha na chuma ulete ya aina hii.
Katika makala ya leo sitaielezea sana chuma ulete ya mapenzi, nitajikita zaidi katika chuma ulete iliyo zoeleka ingawa nitagusia kidogo kuhusu Chuma ulete ya mapenzi.
Chuma ulete za mapenzi zipo za aina nyingi, lakini zenye nguvu, zipo za aina kumi na tatu. Nitaelezea kwa ufupi sana, aina moja tu kati ya hizo kumi na tatu.
Kuna ndege mmoja anapatikana porini. Ndege huyo ana rangi nyeusi na kahawia, na macho yake huwa yenye ku’gaa. Dume la ndege hawa huwa na umbo dogo zaidi kuliko jike na huatamia na kulalia makinda. Kichali ama kiota cha ndege huyu, hutumika kuhifadhi mayai ya ndege wa aina nyingine ambae pia huishi porini.
Basi mwanamke akimlisha mwanaume wake nyama ya ndege huyo pamoja na dawa ya mti fulani wa porini ambao matawi yake hutoa manyunyu wakati wa usiku. Mwanaume huyo atakuwa mtumwa wa mwanamke huyo katika siku zote za maisha yake na atakuwa anampatia mwanamke huyo kila anacho chuma.
Naomba niishie hapo kwa leo kuhusu chuma ulete ya mapenzi, Nitaelezea aina zote kwa kina katika siku zijazo.
Sasa tuje kwenye chuma ulete iliyo zoeleka na watu wengi. Kama nilivyo elezea hapo juu, chuma ulete ni wizi wa kichawi, au wizi wa kimazingira au wizi wa kiini macho.
Anakuja mtu dukani kwako au kwenye eneo lako la biashara, anakupatia noti ya shilingi elfu kumi na kuagiza vitu vya shilingi elfu mbili. Utamrudishia chenji shilingi elfu ishirini na nane badala ya shilingi elfu nane. Tofauti utakuja kuiona wakati wa kupiga mahesabu na mwisho wa siku utaishia kugombana na mfanyakazi nakadhalika.
Wengine anakuja kwa gia ya kuomba chenji, ukimpa chenji, kiasi fulani cha hela zako, kinahamia kwenye kibubu chake. Anaweza pia kununua vitu, ukimpa chenji, kiasi fulani cha hela kinahamia nyumbani kwako.
Chuma ulete nyingine ni ya wizi wa vyakula majumbani na madukani. Wachawi wanatumia ndumba kuiba vitu kama vile unga, mchele sukari nakadhalika kwenye maduka na majumba ya watu. Nitaelezea chuma ulete hii katika siku zijazo, leo nitazungumza kuhusu chuma ulete ya hela.
JINSI CHUMA ULETE INAVYO TENGENEZWA.
Ili kutengeneza chuma ulete , mchawi huchukua njugu mawe nyeusi na kuimeza nzima nzima bila kuitafuna halafu anainya na kuichukua tena. Baada ya hapo atachukua mti unaitwa Kilinda Mgunda, anaunguza pamoja na hiyo njugu mawe nyeusi aliyo imeza na kuitoa kwa njia ya haja kubwa. Vinachomwa kisha vinasagwa na kuwa unga unga. Anachanjwa kwenye pembe zote za mwili wake na kupakwa hiyo ndumba halafu ndumba nyingine inawekwa kwenye chungu kisha inapikwa pamoja sarafu halafu anatumia kuoga
Baada ya hapo ataenda kuwaalika majini wa chuma ulete ulete. Jinsi majini wa chuma ulete wanavyo alikwa. Kinachukuliwa kipande cha ngozi ya hayawani wa mwituni, ngozi ya kinyonga iliyo kaushwa, pamoja na pangaa ya mti. Pangaa ya mti ni mti ulio ota juu ya mti mwingine.
Vitu vyote hivi vinachomwa pamoja na njugu mawe na kisha kusagwa na kufungwa kwenye kitambaa chekundu pamoja na jinni halafu vinaenda kufungwa kichawi kwenye mti mkubwa kwa muda wa siku tatu usiku na mchana.
Baada ya hapo, ndumba hiyo itatolewa mahali hapo na kwenda kuwekwa kichawi katika eneo la sokoni vinapo uzwa vitu.
Baada ya siku tatu ndumba hiyo inachukuliwa inaenda kuzikwa kaburini kwa muda wa siku tatu.
Siku ya saba, ndumba hiyo inachukuliwa na kupelekwa kwenye chumba maalumu, kwa ajili ya kupikwa kichawi. Basi baada ya hapo, hiyo chuma ulete itakuwa inafuata amri ya mtu huyo na kumpatia chochote anacho kitaka.
JINSI YA KUIDHIBITI CHUMA ULETE.
Zipo njia za kudhibiti chuma ulete, si rahisi kuzielezea zote kwa wakati mmoja, leo nitaelezea njia hii ifuatayo ;
Chinja kuku mweupe halafu chukua firigisi. Pasua hiyo firigisi halafu weka ndani yake shilingi elfu moja ya noti . Baada ya hapo nenda kaichimbie chini ya ardhi kwa muda wa siku sita. Siku ya saba nenda kafukue hiyo firigisi, chukua shilingi elfu moja yako na uiweke kwenye droo ya biashara yako na ututukanga.
Basi hakuna mchawi yoyote Yule atakuja kuiba hela kichawi kwenye biashara yako.
MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI, MTAALAMU ALIYE BOBEA KATIKA ULIMWENGU USIO ONEKANA. ANAPATIKANA JIJINI DAR ES SALAAM KWA SIMU NAMBA
0744 000 473
Kwa habari mbalimbali kuhusu mambo yanayo endelea katika ulimwengu usio onekana, tembelea kila siku : www.mungwakabili.blogspot.com
Haina umuhimu
Mkuu LIKUD hututukanga ndio nini?? Samani lakiniUr so ungrateful!