SOLDIER GENIUS
JF-Expert Member
- Mar 3, 2015
- 358
- 241
Unaposema chuma ulete ni vitu vya kufikirika tu na si uhalisia una maanisha nn?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaposema chuma ulete ni vitu vya kufikirika tu na si uhalisia una maanisha nn?
Ni vitu ambavyo havipo au vilokuwepo zamani tena kwa uchache sana ila kutokana na 'mass hallucinations' imekuwa kama ni kitu cha kweli kabisa
Eng issue sio rahisi hivyo tumefanya utafiti wa kutosha na kuzibiti cash mane tukagundua noti zinavhomolewa kimiraclesPanga na fata Budget zako.Kinyume na hapo chuma ulete itaendelea kuwa wimbo wa taifa kwako
Eng issue sio rahisi hivyo tumefanya utafiti wa kutosha na kuzibiti cash mane tukagundua noti zinavhomolewa kimiracles
Mkuu hapo umenisaidia nitai GoogleIpo mada humu jf jinsi ya kuwakabila hao jamaa embu itafute mkuu ila pole
Zinachomolewa ki-miracles?? kwa namna ipi?
Jaribu kufata utaratibu wa kimapato na matumizi kwa kuandika na kuhifadhi kumbukumbu usidharau hata senti moja kuacha ipotee bila kujua imekwenda wapi.
Halafu acha kuwa na mawazo ya kishirki.
Hii kitu inatia karaha na umasikini. Naomba ushauri kwa mwenye kujua jinsi ya kukabiliana na hawa pepo wa chuma ulete. Seriously!
Hii kitu inatia karaha na umasikini. Naomba ushauri kwa mwenye kujua jinsi ya kukabiliana na hawa pepo wa chuma ulete. Seriously!
dawa ni hii,njoo kanisa la eagt kwa katunzi mtoni mtongani njia ya mbagala shuka mtongani mbelekidogo kuna reli inavuka juu ukivukahapo utaona kanisa kubwa mkono wa kushoto hata ukiuliza utafika nakwambia majini,chuma ulete,uchawi kwa mchungaji katunzi Mungu atajibu na ni buree hakuna mafuta wala nini hapo ibada ni kila jtano has ijumaa saa kumi jmos saa 9 jpili saa 3asbh,karibaana mimi nimeona kwa macho yangu seriously karibu ujione kuanzia jtano ni ibada mpaka jpili.
Ok, kiboko yao ni Yesu tu, wachawi hawasogei
Unaweza kudhani ni habari za kufikirika au za redio mbao lakini hili pepo la chuma ulete lipo na linafanya mambo yake ila ni pepo Fukara na la kipuuzi kabisa
Chuma ulete halikupi utajiri wala mali za maana chuma ulete halitaki vitu vizuri chuma ulete halitaki elimu wala maarifa chuma ulete ni pepo chafu lenye mzio na usafi
Ukitembelea maduka ya wahindi kariakoo na posta na miji mingine yenye hii kabisa hutakosa kuona wamefunga kamba yenye majani ya mwembe na wengine kufuga kasuku(msema kweli na msema chochote) hawa wanaamini kuwa hiyo ni dawa ya chuma ulete
Kwa wale wasiojua chuma ulete ninini iko hivi unafanya biashara tangu asubuhi mpaka jioni unauza kama kawaida lakini inapofika wakati wa kufunga mahesabu pesa iliyopo na tofauti na vitu ulivyouza au ulikuwa na laki moja mfukoni anatokea mtu na kukuomba chenchi unampa lakini baadae kila ukipiga mahesabu haibalance..! Hiyo ndio chuma ulete
Pepo la chuma ulete linakaa kwenye noti unayopewa na mhusika mara nyingi akitaka chenchi hapo ndio chuma ulete hufanya kazi vizuri na kwakweli chuma ulete ni mazingaombwe tu ambayo hayana faida yeyote kwa mmiliki zaidi ya kumpatia vitu vya kipuuzi kabisa na vya kifukara
Chuma ulete ni pepo lisilo na faida kwa mmiliki lakini lakini likimtia hasara mlengwa ndio maana chuma ulete ni maarufu zaidi uswahilini kwenye biashara za kawaida kuliko zile biashara kubwa kubwa zenye faida nono na kwakweli chuma ulete ni kitu cha kufikirika zaidi kuliko uhalisia
Umeanza vizuri,umeharibu mwishoni,uliposema ni kitu cha kufikirika zaidi kuliko uhalisia.
Sio cha kufikirika,kipo kweli.
Tatizo ni kwamba haya mambo ni ya ulimwengu wa roho/ulimwengu usioonekana!