kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,746
mshana jr, huwa nakubali sana hizi mada zako, kwenye hili naomba niongeze kitu kidgo.
Hzi chuma ulete zina stage zake, na hizi za mtaani ni zile wanazotumia viroho vichafu na vidogo.
Ukija kwenye money Ritual, kuna mambo hufanyika kwa kiwango kikubwa kidogo. Haya ndio yanayoweza patikana kama matokeo ya hizo money ritualz, huleya haina hizi za uchumaji mali kwa mazingara.
1.Walet money, hii inakuwa unapewa pesa ya kiwango kikubwa lets say kwa hapa bongo ni 10,000. Hii unaend itumia kwenye store au sehemu mbalimbali na lengo ni kuichanganya na pesa zingine zisizo za ushirikina, akikupa chenchi kaumia, baada muda mfupi ile hela itarudi na pesa zingine. Hii ndio imezoeleka mitaani, kutokana na uchumj mdogo hawa wanashindwa.kwenye sehemh kubwa kununua vitu vikubwa ili wapige hela. ( kimbuka hao wakubwa wamejipanga haswa).
2.Mikopo yenye kutaka dhamana. Kuna watu kazi yao ni kupiga hela na utajiri kwa njia hiii, HOW…? Ukichukua.mkopo kwa mtu huyu, ukiweka dhaman yako kwake, hata ufanyeje, Huwezi lipa deni lake so mwisho wa siku anaichukua dhamana yako. Hapa jamaa anakuwa na uhakika wew piga pindua hutopata pesa ya kulipa hilo deni so utakuta jamaa kashapata mteja anauza tarehe ikifika. Kumbuka dhaman inayotakiwa huwa inakuwa na thamani kubwa kidogo kuliko pesa uliyochukua, hapa ndio faida utengenezwa pindi umefeli lipa.
3. Kwenye mabenki, kuna watu walio jipanga haswaaa. Hawa hupeleka hela zao zenye michakato kwenye mabenki, kumbuka benki huzungusha hela kukopesha na kazi zingine mbalimbali, baada ya wiki 3 ndio jamaa huanza kuvuna pesa zake, kama mwenye benkj akiwa hayupo vzuri utakuta pesa inapigwa tu na watu wanapewa kesi. Huyu mtu anakuwa na sehemu au kitu special cha kukusanyia pesa. Akiwisho au kuhitaji kiasi fulanj cha pesa kinakuja.
Note. kila mtu hupewa masharti ya matumiza kulingana na nyota yake. Mfano, kuna mwingie huambiwa kabla ya kuzitumia hizo hela. Chukua noti 3 za hizo heela then wapatie mabikra, hapa mtu anatafuta vibinti vinavyokuwa anavipa hela ( mkosi unakuwa kwao hao mabinti hawataweza kupata uzazi).
Hela zingine huwezi pata akili kabisa ya maendeleo bali kuzifuja tu
hapo namba mbili kwenye red inasemekana aliyekuwa mpigaji/tapeli maarufu jijini dar anaye ozea gereza la ukonga mpaka leo,papa musofe alitajirika sana kwa mtindo huo.inasemekana alijipatia nyumba nyingi dar kwa walio mkopa kushindwa kumlipa deni kwa wakati.labda alikuwa anatumia aina ya "chuma-ulete" uliyo iongelea.
tukija hapo chini kabisa kwenye red,maelezo yako yamenifanya nikumbuke story moja niliyosimuliwa inayomuhusu mpigaji mwingine maarufu hapa town wa kuitwa ostaz juma na musoma,inadaiwa kwamba pamoja na kwamba huyo jamaa anapiga mtonyo wa nguvu ktk madili yake ya kutapeli watu kwa kujifanya mganga wa kienyeji mwenye uwezo wa kuongeza pesa,lakini mpaka hii leo hana hata kibanda,akiwa dar huwa analala kwenye guest house na viji-hotel vya pale kinondoni.moja ya ufujaji wake wa pesa ni kugawa kwa wanamziki wa dansi na watangazaji wa redio ili atajwe.