Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti?

Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti?

Mkuu mshana jr ebu jitahidi kuelezea namna nzuri ya kujihami na chuma ulete maana ufafanuzi wako bado hautoshelezi kabisa naomba usiishie hapo kwenye kufuga kasuku na kamba ya muembe tu...
Ukienda kule kigoma na s'wanga noti zote kule huwa zinakatwa kidogo kujihami na chuma ulete. Wengine wanadai ukitaka kuzuia chuma ulete tenganisha pesa ya mtu unaemstukia kuwa ni chuma ulete... bado imekaa kidhahania zaidi.
Utamtambuaje chuma ulete???

Hii ni kitu ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia ingekua inalipa kihivyo matajiri wengi wangefilisika na kutajirisha wengine
 
Last edited by a moderator:
mshana jr, huwa nakubali sana hizi mada zako, kwenye hili naomba niongeze kitu kidgo.
Hzi chuma ulete zina stage zake, na hizi za mtaani ni zile wanazotumia viroho vichafu na vidogo.
Ukija kwenye money Ritual, kuna mambo hufanyika kwa kiwango kikubwa kidogo. Haya ndio yanayoweza patikana kama matokeo ya hizo money ritualz, huleya haina hizi za uchumaji mali kwa mazingara.

1.Walet money, hii inakuwa unapewa pesa ya kiwango kikubwa lets say kwa hapa bongo ni 10,000. Hii unaend itumia kwenye store au sehemu mbalimbali na lengo ni kuichanganya na pesa zingine zisizo za ushirikina, akikupa chenchi kaumia, baada muda mfupi ile hela itarudi na pesa zingine. Hii ndio imezoeleka mitaani, kutokana na uchumj mdogo hawa wanashindwa.kwenye sehemh kubwa kununua vitu vikubwa ili wapige hela. ( kimbuka hao wakubwa wamejipanga haswa).

2.Mikopo yenye kutaka dhamana. Kuna watu kazi yao ni kupiga hela na utajiri kwa njia hiii, HOW…? Ukichukua.mkopo kwa mtu huyu, ukiweka dhaman yako kwake, hata ufanyeje, Huwezi lipa deni lake so mwisho wa siku anaichukua dhamana yako. Hapa jamaa anakuwa na uhakika wew piga pindua hutopata pesa ya kulipa hilo deni so utakuta jamaa kashapata mteja anauza tarehe ikifika. Kumbuka dhaman inayotakiwa huwa inakuwa na thamani kubwa kidogo kuliko pesa uliyochukua, hapa ndio faida utengenezwa pindi umefeli lipa.

3. Kwenye mabenki, kuna watu walio jipanga haswaaa. Hawa hupeleka hela zao zenye michakato kwenye mabenki, kumbuka benki huzungusha hela kukopesha na kazi zingine mbalimbali, baada ya wiki 3 ndio jamaa huanza kuvuna pesa zake, kama mwenye benkj akiwa hayupo vzuri utakuta pesa inapigwa tu na watu wanapewa kesi. Huyu mtu anakuwa na sehemu au kitu special cha kukusanyia pesa. Akiwisho au kuhitaji kiasi fulanj cha pesa kinakuja.


Note. kila mtu hupewa masharti ya matumiza kulingana na nyota yake. Mfano, kuna mwingie huambiwa kabla ya kuzitumia hizo hela. Chukua noti 3 za hizo heela then wapatie mabikra, hapa mtu anatafuta vibinti vinavyokuwa anavipa hela ( mkosi unakuwa kwao hao mabinti hawataweza kupata uzazi).

Hela zingine huwezi pata akili kabisa ya maendeleo bali kuzifuja tu
merengop90 naikubali sana michango yako
 
Last edited by a moderator:
Sasa hizo ndulele watu hutumia kuzuia chuma ulete, wanaziweka kwenye pesa za mauzo n.k.

Ila ukitaka kucheka chuma ulete aende kwa mtu mwenye majini au mizimu ya kwao kichwani, utaona mchakamchaka.

Ila ukitaka huwe safe zaid, jikabidhi kwa Mungu tu
 
Mm mdogowangu alipigwa laki3 za mpesa..alikua wakala na biashara ikafia hapo coz mtaj ulikua mdogo uswahilini nomasana
 
Au tura zinatumika sana kujikinga na chuma ulete

Sasa hizo ndulele watu hutumia kuzuia chuma ulete, wanaziweka kwenye pesa za mauzo n.k.

Ila ukitaka kucheka chuma ulete aende kwa mtu mwenye majini au mizimu ya kwao kichwani, utaona mchakamchaka.

Ila ukitaka huwe safe zaid, jikabidhi kwa Mungu tu
 
mshana jr niliwahi kusikia kila bank hapa Tanzania Zikizinduliwa kuna wazeee wanakuja kusimika ZINDIKO
Pia kuna tetesi Mahakama zote hapa Bongo ZIMEZINDIKWA!!

Natumai mshana jr utakuja na Thread yake kuhsu hizi Taasisi.

Hizo habari zipo sana tu na Nazifanyia kazi ili siku nikija nije na kitu kamili
 
Last edited by a moderator:
Hizo habari zipo sana tu na Nazifanyia kazi ili siku nikija nije na kitu kamili

Hapa naona tujifunze namna ya kukanyaga madhabau za shetani kwa kutumia nguvu za mungu alieumba mbingu na nchi. Ukijua hilo wataweka vichungu vyao kutengeneza madhabahu njia panda na kwengine, WEWE UNAKANYAGA KWA SPIDI ZOTE NA KUSONGA MBELE bila kuingia katika mitego yao, vinginevyo..................
 
Back
Top Bottom