Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Habari zenu wana JF,

Mdogo wangu anasubuliwa na tatizo la chunusi kifuani, mgongoni na mabegani usoni zipo ila sio nyingi jambo hili linamkosesha raha maana anashidwa kuvaa baadhi ya nguo na hasa kipindi cha joto.

Kwa anayefahamu dawa ya tatizo hili, naomba anisaidie.

Asanteni.
 
Bora aendelee tu kuugua hizo chunusi maana ninachokiona anatafuta kuvaa sleeveless tops na nguo zingine za wazi wazi. Sasa sijui anataka kuvaa sudiria kutwa nzima.
 
Habari zenu ndugu zanguni,..?.
Naomba msaada wenu kitu kimoja,..
mimi ninatatizo la chunus,..yan tangu nianze kupevuka mhhhh
chunus hazikuisha had leo hii,..
nina umri wa miaka26,..ila daahh zinaninyima raha kabisa,..
maana huwa zinanitesa sana sana,..
hadi nmeenda hospital wapiiii
nimeenda S.H. Harmony yaani ni bure2,.sikupata impact yoyote yan
zaidi dawa zao zikawa zinaniongezea chunus,..
nmetumia gharama sana hadi nmeamua niache2,..
ila dahh nakosa raha kabisa ,...
Scrabs,madawa tofauti,nmetumia sana ila wapi
NAOMBA USHURI WENU WANDUGU,..




NB; dawa ya gharama yoyote ninamudu,..
 
Pole sana! Hata mimi zilinisumbua sana hizo chunusi enzi za upevukaji wangu, kiasi kwamba nikawa naona aibu kwa vijana wenzangu! Kipindi kile nikawa nahangaika na sabuni za Dettol, Protex au wakati mwingine Roberts Medicated lakini zote hazikufua dafu! Kuna baadhi watu wakaniambia kwamba sababu ya hizo chunusi ni kutokufanya mapenzi! Dawa kuondoa chunusi in kuduu tu, niliamini! Niliamini, kwa sababu kwa muda uume wangu ulikuwa ukihiitaji sana nipate k, Nikizangatia kwamba kwa wakati ule nilikuwa nawaogopa sana hawa viumbe, nilijipa ujasiri nikafanikiwa, baada kuona utamu nikanogewa!!! Na nikawa nawamega mademu si kwa lengo LA kuondoa chunusi Bali ule utamu wa tendo! Ukweli ni kwamba hata sijui hizo chunusi zilipotea muda gani! Swali kwako mleta mada, je unawagonga mademu? Inawezekana chunusi zako ni za "ugumu" ulionao!
 
Hahah watu mnawapoteza wenzenu dah!
Haya mkuu fata huo ushauri ukikusaidia tuletee mlejesho tafadhali
 
Habari zenu wakuu.
Mwenzenu ninatatizo la chunusi toka kuvunja ungo mpaka sas nina miaka 29 sijawahi kuw na raha na uso wangu.msaada jaman anaejua dawa maana umri huu ngozi mbaya kama kenge.mbaya zaidi yanatoka makubwa kama majipu.msaada tafadhadi.
ukipata jibu nijuze na mimi,...
maana hii shida ni tatizo zinanitesa pia
 
Tumia udongo wa Zaynab Clay, unatangazwa sana humu jf. Nilimpa dada mmoja alikuwa na chunusi za mgongoni ziliisha kabisa hadi leo
 
DAWA YA KUONDOWA CHUNUSI USONI

chunusi.jpg
chunusi 2.jpg



Hii ni dawa nzuri kwa wale wote wenye Chunusi, kama utafuata maelekezo vizuri utaweza kupata matokeo mazuri.


Mahitaji

Kijiko cha chai kimoja - Juice ya Viazi mbatata

Nusu kijiko cha chai - Unga wa Lozi
robo kijiko cha chai - Manjano
Jinsi ya kutengeneza


Changanya vitu vyote pamoja kisha pakaa kwenye vipele vyeusi (usipake uso mzima kwenye vipele tu). Iache kwa muda wa nusu saa au hata unaweza kulala nayo. Pakaa kila siku kwa muda wa wiki mbili. Baadae utapaka kwa wiki mara mbili mpaka uone umeondoka weusi.

MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu

nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto. Watu wenye chunusi wanashauriwa kula mlo kamili wenye vyakula vyenye

madini ya zinki,nyuzinyuzi,matunda , mboga za majani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula

vya maziwa,tumbaku,sukari,vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi.

KARANGA TIBA YA KUONDOWA CHUNISI USONI.

TIBA.1


1. Karanga Zinaondoa Chunusi Usoni na kuufanya Uso kuwa Laini na kuleta uzuri wa Sura.

Chukua Karanga kijiko kimoja kidogo zisage kisha changanya na kipimo sawa cha juisi ya ndimu Au limao halafu unapaka kila siku Usoni kabla ya kulala.


TIBA.2

KUONDOA MAKOVU YA CHUNUSI.


1. Paka ‘bleach cream’ kwenye sehemu zenye makovu, cream hii husaidia kuondoa makovu.

2. Tumia ‘scrub’ ambayo huondoa ngozi ya juu (exfoliate) kwa kupaka kwenye sehemu zenye makovu kama usoni na kwingineko ambako ni rahisi kupaka. Unaweza kufanya zoezi hilo angalau mara mbili kwa wiki.

3. Tumia bidhaa ambazo zina ‘hydroxyl acids`, hutibu ngozi yako na itaonekana nyororo. Unaweza kupata hydroxyl acidstofautitofauti za ngozi (skin care products) kama vile cleansers na lotion.

4. Pia unaweza kuyafanyia masaji makovu ya chunusi ili kuvunja mafuta yaliyoganda ambayo huleta chunusi.

5. Fanya ‘diet’, unatakiwa kula vyakula vyenye vitamin na nutrition, vinasaidia kutengeneza ngozi yako kuwa na afya.


UKIWA NA SWALI AU SHIDA YOYOTE UNAWEZA KUNITAFUTA KWA KUBONYEZA HAPA.Mawasiliano
 
mbona pic ya kwanza ni mwafrica ukafatisha wazungu inamaana huyo mwafrica haifai au ukitumia hivyo inakufanya mzugu? na Huo unga wa viazi mbatata&lonzi unapatikanaje?
 
mbona pic ya kwanza ni mwafrica ukafatisha wazungu inamaana huyo mwafrica haifai au ukitumia hivyo inakufanya mzugu? na Huo unga wa viazi mbatata&lonzi unapatikanaje?
Kwanza umenikosoa kisha unataka kujuwa unga wa viazi mbatata na unga wa lozi unapatikana wapi? nenda katafute wewe mwenyewe nimekupa dawa badala ya kushukuru unani laumu Kiumbe usiye kuwa na shukrani wewe.
 
Kwanza umenikosoa kisha unataka kujuwa unga wa viazi mbatata na unga wa lozi unapatikana wapi? nenda katafute wewe mwenyewe nimekupa dawa badala ya kushukuru unani laumu Kiumbe usiye kuwa na shukrani wewe.
Msamehe!ndo binadamu walivyo hawana shukrani mkuu!
 
Back
Top Bottom