Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Chunusi: Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

[h=1]MATIBABU YA CHUNUSI (TREATMENT OF ACNE)[/h]

Lengo la tiba ya chunusi ni kupunguza uzalishaji wa mafuta ya sebum usoni pia kutibu vijidudu vya bakteria ambavyo hushambulia ngozi ya uso na kusababisha viupele vinavyowasha na wakati mwingine kuleta maumivu usoni.
Uchaguzi wa dawa hutegemea na jinsi ugonjwa ulivyoshambulia uso (severity), sehemu iliyoharibika huhitaji kufanyiwa usafi wa kutosha kila siku tena uwe wa ziada zaidi ya kawaida kwa kutumia sabuni zenye antibaotiki, kubadilisha tabia ya chakula, matumizi ya kemikali za Sulfur salicylic acid na Resorcinol haisaidii kuondoa chunusi.
Matibabu hugawanywa sehemu kuu tatu ambazo kwanza ni wale wenye chunusi kidogo (mild acne), pili wenye chunusi za wastani (moderate acne) na tatu ni wale walioathirika sana yaani hali yao ni mbaya (severe acne).
Wale wenye vipele au chunusi kidogo hutumia dawa moja tu ambayo hujulikana kama Benzoyl peroxide au pia huchanganya na dawa ya antibaotiki, mgonjwa hutumia kila siku kwa kipindi cha wiki sita na zaidi.
Pia dawa kama Adapalene gel na nyingine kama Tazarotene gel hutumika. Dawa zipo nyingi nyingine ni kama vile Azelaic acid cream na Glycolic acid.

MADHARA YA DAWA
Madhara ya hizi dawa siyo makubwa na baadhi ni kama vile uso kukauka sana na baadhi ya dawa hizo hutumika kwa wanawake kipindi ambacho hawana mimba.
Lakini kwa wanawake wajawazito wasitumie dawa zozote bila ushauri wa daktari kwa kuwa baadhi ya dawa ni hatari kwa akinamama wenye mimba.
Wale wenye chunusi za wastani huhitaji dawa za antibaotiki kama vile Tetracycline, Doxycline, Minocycline na Erythromycin.
Dawa hizi hutumika kwa kipindi kisichopungua wiki 12 na hutolewa na daktari baada ya kuridhika kuwa haziwezi kumuathiri mgonjwa, hivyo basi naomba msinunue dawa hizi hovyo.
Wale wenye chunusi nyingi dawa ya kunywa ya Isotretinoin ndiyo dawa sahihi na hutibu vizuri na hutumika baada ya kupima uzito na hutumika kwa wiki 16 hadi 20. Itumike kwa ushauri wa daktari.
 
Asante kwa michango ya wadau
SASA TWENDE KATIKA IMPLEMENTATION BWANA POMPOO
 
mm naona ni bora ukaanza kutumia izo dawa za asil koz most of them hazina effect kama asal na malimao....kuliko hizo izo za tube coz hizo zinaendana na ngozi so ucje ukaharibu zaid mkuu
 
Habari zenu wadau wa jukwaa hili,nina tatizo la chunusi,na hiyo ni baada ya kupata ujauzito,je hua zinapona au mpaka nijifungue,na kama zinatibika ni vitu gani nitumie ili ziweze kwisha maana zimekua kero asanteni
KARANGA TIBA YA KUONDOWA CHUNISI USONI.

TIBA.1

1. Karanga Zinaondoa Chunusi Usoni na kuufanya Uso kuwa Laini na kuleta uzuri wa Sura.

Chukua kijiko kimoja kidogo changanya na kipimo sawa cha juisi ya ndimu Au limao halafu unapaka kila siku Usoni kabla ya kulala.

TIBA.2

KUONDOA MAKOVU YA CHUNUSI.

1. Paka ‘bleach cream' kwenye sehemu zenye makovu, cream hii husaidia kuondoa makovu.

2. Tumia ‘scrub' ambayo huondoa ngozi ya juu (exfoliate) kwa kupaka kwenye sehemu zenye makovu kama usoni na kwingineko ambako ni rahisi kupaka. Unaweza kufanya zoezi hilo angalau mara mbili kwa wiki.

3. Tumia bidhaa ambazo zina ‘hydroxyl acids`, hutibu ngozi yako na itaonekana nyororo. Unaweza kupata hydroxyl acidstofautitofauti za ngozi (skin care products) kama vile cleansers na lotion.

4. Pia unaweza kuyafanyia masaji makovu ya chunusi ili kuvunja mafuta yaliyoganda ambayo huleta chunusi.

5. Fanya ‘diet', unatakiwa kula vyakula vyenye vitamin na nutrition, vinasaidia kutengeneza ngozi yako kuwa na afya.

Ni mabadiliko tuu ya kimwili kulingana na kuongezeka ama kupungua kwa homoni,usijali jinsi siku zinavyokwenda ngozi itarudia hali yake ya kawaida..
 
Ni mabadiliko tuu ya kimwili kulingana na kuongezeka ama kupungua kwa homoni,usijali jinsi siku zinavyokwenda ngozi itarudia hali yake ya kawaida..
Habari zenu wadau wa jukwaa hili,nina tatizo la chunusi,na hiyo ni baada ya kupata ujauzito,je hua zinapona au mpaka nijifungue,na kama zinatibika ni vitu gani nitumie ili ziweze kwisha maana zimekua kero asanteni
 
Habari zenu wadau wa jukwaa hili,nina tatizo la chunusi,na hiyo ni baada ya kupata ujauzito,je hua zinapona au mpaka nijifungue,na kama zinatibika ni vitu gani nitumie ili ziweze kwisha maana zimekua kero asanteni

Kumbe kule MMU mkilog off huwa mnapractice kweli? Hongera zake kidume muhusika.

Back to topic usihofu hiyo ni kawaida sana tena unaweza ukanenepa kabisa na kauzuri kako kakapunguwa kidogo lakini it's just transition period. The most important feel proud to become a mother.
 
hahahaaa!!huku twataka msaada wa kidocta zaidi
ila na wewe lol!!
 
Hongera bi dada,Mungu akujalie Afya njema na uweze kujifungua salama!
 
Mimi nimejaribu dawa mbalimbali zimegoma kuisha kuna mtu akanishauri niwe nanawa uso kwa sabuni kadri niwezavyo kila siku.nikaanza na nanawa mara nyingi sana kila nikipata chance naona sasa zimepungua.sipaki chochote baada ya kunawa
 
Hongera
 
Habari zenu wadau wa jukwaa hili,nina tatizo la chunusi,na hiyo ni baada ya kupata ujauzito,je hua zinapona au mpaka nijifungue,na kama zinatibika ni vitu gani nitumie ili ziweze kwisha maana zimekua kero asanteni

Utazaa mtoto wa kiume. Akiwa wa kike ni pm namba yko nikutumie laki.
Utakua soft tena baada ya kujifungua.
 
Back
Top Bottom