Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
kati ya vitu nilivyokuwa nikivikwepa katika shule yangu yote tangu primary hadi universities, ni kuiba mtihani, sijawahi, au niseme sikumbuki. wakati wenzangu walikuwa wanapambana nawaona kabisa wameingia na nondo,mimi nilikuwa nafanya bila nondo na NILIAMINI KUINGIA NA NONDO NI DHAMBI, nadhani hiyo ilinisaidia, ile kuamini ni dhambi na namkosea Mungu hivyo nisingefaulu kwasababu Mungu ataniacha nikitenda dhambi/nikitegemea nondo badala ya kumtegemea yeye. hiki ndicho nilichoambukiza hata watoto wangu.
kosa pekee ninalokumbuka nililifanya, ni watu ninaokaa nao kwenye mtihani wakitaka kuangalizia nilikuwa sifichi mtihani nauacha tu wazi nikiamini ni dhambi zake mimi siwezi kuanza kufunika mikono kwenye majibu kwa kuogopa wenye macho makali wataangalizia, nilikuwa naendelea tu kufanya yangu anayechungulia atajua hukohuko. pengine nilitakiwa niwe na roho ngumu nikiona mtu anachungulia nifunike/nifiche, labda. ilo ndo kosa nalikumbuka, ila kutegemea kitu kingine chochote awe rafiki au nondo, sikumbuki na Mungu alikuwa ananisaidia wale wanaoingia na nondo na wenzangu wametoka mijini wamesoma tuition likizo nzima mimi nikiwa nimeweka daftari huko nazichukua shule ikifungua, nilikuwa nawazidi darasani wote, na nimewazidi hadi nilipofika form six kila shule ninayoenda.