Chuo cha Ardhi kuweni makini na huu mtego wa suala la mapacha kudai kufanyiana mtihani

Kwa mujibu wa mahojiano yale kabla ya mahojiano rasmi wale mapacha walikuwa wameshawaambia wale watangazaji kwamba kuna mmoja alimfanyia mtihani mwenzie. Kwa umri wa wale watangazaji na katika hali na akili ya kawaida walipaswa kuwa wamewapa tahadhari na kuwaambia hao mapacha madhara ya kutamka issue kama hiyo kwenye kipindi. Na pengine hata wasingewauliza kitu kama hicho wakati wa mahojiano tena mahojiano ambayo ni live. Hivyo ni wazi kwamba issue hiyo ilikuwa aired kwa makusudi aidha kunogesha kipindi au media husika na wao mapacha wenyewe kupata publicity au vyote kwa pamoja.
Pale wasafi hakuna wahariri wa vipindi wenye akili na busara hii uliyo ongelea hapa.
 
Habari.
Naomba niende moja kwa moja kwenye hii issue.

Kuna taarifa ambayo kwa sasa inatambaa sana hapa jf na hata kwenye mitandao ya kijamii kama x,na you tube.

Issue inahusu swala la mapacha wawili waliokuwa wanafunzi wa ardhi kusema kuwa kuna Mtihani mmoja wa supplementary walishawahi kufanyiana hasa kutokana na mfanano wao sawa kiasi cha kushindwa kutofautisha yupi Kurwa na yupi Doto.

Wadada hawa ikumbukwe walifanya interview yao kupitia kipindi kinachorushwa na wasafi ambayo ni channel ya burudani na vijana,sehemu ambayo utani na uongo bila kusahau majigambo ni sehemu ya kunogesha content ili kuvutia hadhira ambao kwa kiasi kikubwa ni vijana i hope tunajua mengi huwa yanaelezwa humo ya uvumi kama issue ya nyumba ya mwijaku ya 1.5b kule kigamboni kitu ambacho watu watathimini wakiingia kazini lazma wapingane na hyo thamani.

Sababu ya kuandika haya yote ni baada ya kuona tangazo/taarifa mliyoitoa kuwa mnafanyia uchunguzi suala hilo kama ni kweli au uongo ili mchukue hatua.

Niwe muwazi kwa jinsi nilivyosoma taarifa/tangazo lenu ni kitu ambacho nina hakika ni wachache waliokaa chini na kukubaliana kuiandika taarifa ile sababu ni taarifa ambayo haikushiba kiasi cha kwamba vitu vidogo vidogo ambayo vingepaswa kuipa nguvu taarifa yenu havikuwepo kama majina ya wahusika,uthibitisho kuwa walishawahi kuwa wanafunzi wenu n.k. kupitia hvyo nikiri hii taarifa mliitoa kwa msukumo na haraka mno kiasi cha kunifanya niandike haya ili kwenye uchinguzi wenu msitoe hukum/maamuzi ya kimhemko.

Nikiri wazi kuwa kesi hii/au maamuzi yatakayotoka yanaweza kutengeneza kesi ya muda mrefu kwenu endapo mtachukua maamuzi ya kufuta degree za hawa mabinti kwa maamuzi ambayo hayatakuwa na mashiko na nikiri tu wazi nafasi ya chuo cha ardhi kushinda ndani ya kesi hii ni ngumu sana kwa kuzingatia mda mtihani uliokwisha pita toka mtihani ufanyike,na pia aina na sehemu maneno hayo ya wanafunzi yalipotolewa.

Ni utabiri wangu kuwa endapo chuo kitakurupuka kufuta degree za wanafunzi hawa basi kutatokea mawakili wengi wataotaka na watakaopata umaarufu mkubwa kupitia kesi hii na hata chuo kama chuo kuingia doa na hata hasara ya fidia na madudu mengi kuibuka.kwani kwa wanasheria/mawakili hii ni kesi yao ya kutengeneza majina kwenye tasnia yao ya sheria.

Ni matumaini yangu kuwa chuo kitafanya maamuzi sahihi na kuja na uchunguzi wenye sababu zenye mashiko ili kulinda heshima ya chuo na hata migogoro isiyo ya lazima.

Pia soma
- Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo
Nami nikushangae kwa uchambuzi wako ambao haujashiba, chuo kimesema kinachunguza ukweli wa hizo taarifa, manake nini, ni pamoja na kutaka kujiridhisha majina ya wahusika, ikiwa ni pamoja na kuthibitisha pasipo shaka kuwa wamewahi kusoma na kuhitimu chuoni hapo.
Hitimisho taarifa ya matokeo ya uchunguzi ndo inapaswa kuja na yote uliohoji hapo
 
Chuo kifanye UCHUNGUZI, kama walikuwa wanafunzi basi Vyeti vyao vichanwe na washtakiwe..

Kama ikibainika siyo wanafunzi washtakiwe na Chuo kwa kukiharibia sifa ili iwe fundisho kwa watafuta kiki wengine wajao...
 
Na kama hujabadilika aisee una kazi kubwa sana, dunia hii si ya kujitenga kiasi hicho, am sure hata kama umefanikiwa lakn ungefanikiwa zaidi ikiwa ungekuwa na backup na hazina ya watu ambao mlisaidiana huko shule!!
Ulimuuliza amewazidi kimaisha? Mafanikio sio pesa tu majumba ama magari. Mtu kama Prof Shivji utasema hajafanikiwa? Sio tajiri wa kifedha ila wa elimu na wafuasi wanaoamini mawazo na mafundisho yake. Sawa tu mwl Nyerere.
 
Kosa kubwa watakalolifanya Ardhi University ni kukiri kweli ulifanyika udaganyifu kama ilivyoelezwa na muhusika/wahusika. Itadhihirisha weakness kubwa katika hiyo taasisi na wahusika walioshindwa kudhibiti udanganyifu huo nao watapaswa kuwajibishwa pia.

Japo cheating ipo lakini kukiri waziwazi hii inazorotesha reputation ya taasisi
Kukiri sio kosa kabisa ila ni njia mojawapo ya kutengeneza mifumo imara ya udhibiti. Ikitokea ni kweli, watajuta maisha yao yote maana ni wajinga mno
 
Mbona kama wewe unahusika. Umekuja kama kuwaatisha chuo cha Ardhi wasifanye chochote. Isitoshe wao wamesema wanafanya uchunguzi,sasa hiyo kukurupuka kwako na mihemko imetokea wapi?.

Hao mabinti wameyakoroga wenyewe,ujuaji mwingi,kutaka sifa sifa sana. Ndio hayo matokeo. Kwenye huu tu watapigwa sekeseke mpaka watamani kurudi utotoni.
 
Nami nikushangae kwa uchambuzi wako ambao haujashiba, chuo kimesema kinachunguza ukweli wa hizo taarifa, manake nini, ni pamoja na kutaka kujiridhisha majina ya wahusika, ikiwa ni pamoja na kuthibitisha pasipo shaka kuwa wamewahi kusoma na kuhitimu chuoni hapo.
Hitimisho taarifa ya matokeo ya uchunguzi ndo inapaswa kuja na yote uliohoji hapo
Huyo jamaa kazingua ila hajui kazingua. Anajitahidi kutetea uozo ,sijui ana maslahi gani nao? Wahusika wamekiri ,yeye anakuja na ngonjera za sijui huo mtego sijui chuo kiwe makini.

Serikali kupitia chuo Cha Ardhi imeonesha umakini mkubwa sana Kwa kuamua kufanya uchunguzi , ingekaa kimya ningekilalamikia chuo
 
Muuza magari na mambo ya kitaaluma wapi na wapi!

We subiri watu
 
Kilichopo na nikionacho mimi ni kwamba chuo hakiwezi kukubali kuonekana kilipwaya kwenye swala la usimamizi , na ni hasara sana kwa chuo kukubali kuwa kweli walifanyiana mtihani jambo ambalo litazua mengi sana kwani wataonekana ni wazembe sana nakuhisiwa kuwa huenda wengi wamepita kwa style hiyo na zaidi ya hayo, kuliko chuo kukataa kwamba kitu hicho hakikutokea hapo chuoni bali ni habari za uongo na za kujifurahisha tuu walizo zua hao wadada na watapigwa fine kwa kutoa ushahidi wa uongo unao chafua taswira ya chuo mbele ya jamii na jambo litaisha bila bugudha, kinyume na hapo safari moja itaanzisha zingine nyingi maana hakuna chuo kisafi nchi hii.
Bado mapacha wako wanayo kazi kubwa kama chuo kitasema ni uongo basi Mapacha na kituo cha Wasafi watafunguliwa case ya kuchafua chuo na watachukuliwa hatua kali na TCRA na bado mapacha watapelekwa mahakamani pamoja na wasafi maana hili ni swala la Elimu …kumfanyia myihani mtu ni kosa la jinai kisheria na kuna adhabu yake!
 
Kwa mujibu wa mahojiano yale kabla ya mahojiano rasmi wale mapacha walikuwa wameshawaambia wale watangazaji kwamba kuna mmoja alimfanyia mtihani mwenzie. Kwa umri wa wale watangazaji na katika hali na akili ya kawaida walipaswa kuwa wamewapa tahadhari na kuwaambia hao mapacha madhara ya kutamka issue kama hiyo kwenye kipindi. Na pengine hata wasingewauliza kitu kama hicho wakati wa mahojiano tena mahojiano ambayo ni live. Hivyo ni wazi kwamba issue hiyo ilikuwa aired kwa makusudi aidha kunogesha kipindi au media husika na wao mapacha wenyewe kupata publicity au vyote kwa pamoja.
Kama watakuwa wamefanya kutafuta kiki bado kuna malipo ya madhara ya kilichofanyika….
 
We unajua maana ya uchunguzi? Porojo zote hizo mbona km kuitisha chuo isifanye uchunguzi. Umetumwa au ndio mhusika?
Hawezi kutisha Xhuo wewe
TV imesajiiliwa kama chombo serious cha habari na TCRA

Sio sehemu ya kudhaliilisha taasisi wale wamedhalilisha taasisi na kuvunja maadili ya kufanya mtihani bayo matokea yake ni kufutiwa degree kuwa walizipata kwa udanganyifu wote wawili
 
Mkuu, ata uki confess uku unagegeda as long as upo recorded, msala wa kujibu unao.
 
Habari.
Naomba niende moja kwa moja kwenye hii issue.

Kuna taarifa ambayo kwa sasa inatambaa sana hapa jf na hata kwenye mitandao ya kijamii kama x,na you tube.

Issue inahusu swala la mapacha wawili waliokuwa wanafunzi wa ardhi kusema kuwa kuna Mtihani mmoja wa supplementary walishawahi kufanyiana hasa kutokana na mfanano wao sawa kiasi cha kushindwa kutofautisha yupi Kurwa na yupi Doto.

Wadada hawa ikumbukwe walifanya interview yao kupitia kipindi kinachorushwa na wasafi ambayo ni channel ya burudani na vijana,sehemu ambayo utani na uongo bila kusahau majigambo ni sehemu ya kunogesha content ili kuvutia hadhira ambao kwa kiasi kikubwa ni vijana i hope tunajua mengi huwa yanaelezwa humo ya uvumi kama issue ya nyumba ya mwijaku ya 1.5b kule kigamboni kitu ambacho watu watathimini wakiingia kazini lazma wapingane na hyo thamani.

Sababu ya kuandika haya yote ni baada ya kuona tangazo/taarifa mliyoitoa kuwa mnafanyia uchunguzi suala hilo kama ni kweli au uongo ili mchukue hatua.

Niwe muwazi kwa jinsi nilivyosoma taarifa/tangazo lenu ni kitu ambacho nina hakika ni wachache waliokaa chini na kukubaliana kuiandika taarifa ile sababu ni taarifa ambayo haikushiba kiasi cha kwamba vitu vidogo vidogo ambayo vingepaswa kuipa nguvu taarifa yenu havikuwepo kama majina ya wahusika,uthibitisho kuwa walishawahi kuwa wanafunzi wenu n.k. kupitia hvyo nikiri hii taarifa mliitoa kwa msukumo na haraka mno kiasi cha kunifanya niandike haya ili kwenye uchinguzi wenu msitoe hukum/maamuzi ya kimhemko.

Nikiri wazi kuwa kesi hii/au maamuzi yatakayotoka yanaweza kutengeneza kesi ya muda mrefu kwenu endapo mtachukua maamuzi ya kufuta degree za hawa mabinti kwa maamuzi ambayo hayatakuwa na mashiko na nikiri tu wazi nafasi ya chuo cha ardhi kushinda ndani ya kesi hii ni ngumu sana kwa kuzingatia mda mtihani uliokwisha pita toka mtihani ufanyike,na pia aina na sehemu maneno hayo ya wanafunzi yalipotolewa.

Ni utabiri wangu kuwa endapo chuo kitakurupuka kufuta degree za wanafunzi hawa basi kutatokea mawakili wengi wataotaka na watakaopata umaarufu mkubwa kupitia kesi hii na hata chuo kama chuo kuingia doa na hata hasara ya fidia na madudu mengi kuibuka.kwani kwa wanasheria/mawakili hii ni kesi yao ya kutengeneza majina kwenye tasnia yao ya sheria.

Ni matumaini yangu kuwa chuo kitafanya maamuzi sahihi na kuja na uchunguzi wenye sababu zenye mashiko ili kulinda heshima ya chuo na hata migogoro isiyo ya lazima.

Pia soma
- Mapacha waliokiri kufanyiana mtihani chuo matatani, Chuo cha Ardhi wasema wanachunguza suala hilo
Chuo kinachunguza nini sasa? Ingekuwa mtu mwingine ndiyo ametoa tuhuma dhidi yao hapo ndiyo wangekuwa sahihi kusema wanachunguza. Hao wamekiri wenyewe kwenye media na ushahdi upo hivyo kinachopaswa ni kufanywa ni kuzifuta degree zao.
Ingekuwa ni taarifa iliyoandikwa au iliyokuwa reported angalau wangeweza kusema wanachunguza lakini siyo hiyo live interview, au wanachunguuza kama wakati wanatoa hiyo kauli walikuwa timamu au wamelewa?
 
Kwa sifa na ujunga wao wanajutia huko

Back
Top Bottom