Chuo cha Ardhi kuweni makini na huu mtego wa suala la mapacha kudai kufanyiana mtihani

kati ya vitu nilivyokuwa nikivikwepa katika shule yangu yote tangu primary hadi universities, ni kuiba mtihani, sijawahi, au niseme sikumbuki. wakati wenzangu walikuwa wanapambana nawaona kabisa wameingia na nondo,mimi nilikuwa nafanya bila nondo na NILIAMINI KUINGIA NA NONDO NI DHAMBI, nadhani hiyo ilinisaidia, ile kuamini ni dhambi na namkosea Mungu hivyo nisingefaulu kwasababu Mungu ataniacha nikitenda dhambi/nikitegemea nondo badala ya kumtegemea yeye. hiki ndicho nilichoambukiza hata watoto wangu.

kosa pekee ninalokumbuka nililifanya, ni watu ninaokaa nao kwenye mtihani wakitaka kuangalizia nilikuwa sifichi mtihani nauacha tu wazi nikiamini ni dhambi zake mimi siwezi kuanza kufunika mikono kwenye majibu kwa kuogopa wenye macho makali wataangalizia, nilikuwa naendelea tu kufanya yangu anayechungulia atajua hukohuko. pengine nilitakiwa niwe na roho ngumu nikiona mtu anachungulia nifunike/nifiche, labda. ilo ndo kosa nalikumbuka, ila kutegemea kitu kingine chochote awe rafiki au nondo, sikumbuki na Mungu alikuwa ananisaidia wale wanaoingia na nondo na wenzangu wametoka mijini wamesoma tuition likizo nzima mimi nikiwa nimeweka daftari huko nazichukua shule ikifungua, nilikuwa nawazidi darasani wote, na nimewazidi hadi nilipofika form six kila shule ninayoenda.
 
Hawakulazimishwa kuongea walichoongea wameongea wenyewe Kwa ujinga wao hivyo acha wajue maana halisi ya msemo usemao ulimi uliponza kichwa.

Taasisi yoyote makini, haiwezi kukaa kimya kwenye issue kama hizo achilia mbali ni taasisi ya elimu inayoheshimika. Kitendo Cha hao mapacha kutoa kauli hiyo ingekuwa ni nchi nyingine TCU ingekuwa imegonga mlangoni chuoni kuomba ufafanuzi zaidi.

Kwa kuwa wamekiri Kwa vinywa vyao basi usiwe na mhemko wowote subiri matokeo ya uchunguzi yakamilikie. Uchunguzi ni simple tu, wanaweza kuwa wanafanana Kila kitu Kwa muonekano wao lakini miandiko yao ikawa ni tofauti kabisa na mwandiko wa binadamu ni Moja ya utambulisho wa kumtofautisha mtu na mtu .

Hapo unachukuliwa mtihani huo aliofanyiwa na pacha mwenzake unalinganishwa miandiko na mitihani aliyofanya mwenyewe na zaidi karahisha uchunguzi Kwa kutaja Hadi somo alilomfanyia mwenzake.

Ikibainika ni kweli wamefanya kitendo hicho ninaomba Serikali ichome vyeti vyao vyote moto hadharani maana wamechafua elimu yetu
 
Ulimi n kiungo kidogo ila kinaleta matokeo makubwa. Kuropoka kwake kumemponza. Ukiangalia kile kipindi unaona aliyefanyiwa hakupenda ile taarifa kuwa wazi.

Ule sio utani kabisa; n taarifa ya kweli. Uchunguzi ufanye hatua zichukuliwe
 
Kwa mujibu wa mahojiano yale kabla ya mahojiano rasmi wale mapacha walikuwa wameshawaambia wale watangazaji kwamba kuna mmoja alimfanyia mtihani mwenzie. Kwa umri wa wale watangazaji na katika hali na akili ya kawaida walipaswa kuwa wamewapa tahadhari na kuwaambia hao mapacha madhara ya kutamka issue kama hiyo kwenye kipindi. Na pengine hata wasingewauliza kitu kama hicho wakati wa mahojiano tena mahojiano ambayo ni live. Hivyo ni wazi kwamba issue hiyo ilikuwa aired kwa makusudi aidha kunogesha kipindi au media husika na wao mapacha wenyewe kupata publicity au vyote kwa pamoja.
 
Wakati unaandika ulikuwa unaamini mwenyewe unaandika kitu cha maana. Shida unasikia sikia habari za vijiweni unakuja anzisha uzi. Kijiweni mnadanganyana kuwa hapo jamaa wanaenda anguka.... Za kuambiwa changanya na zako
 
Chawa wa mapacha failures
 
Nilichokidundua humu jf comment ya kwanza ndio huwa inareflect comment zinazofuata, na sio jf pekee hata huko u-tube. Vijana wa Tz wamekuwa wavivu kufikiri.
Thanks kwa kuligundua hilo watanzania wengi huchukulia jambo juu juu tu na si kuangalia mbele
 
Wakati unaandika ulikuwa unaamini mwenyewe unaandika kitu cha maana. Shida unasikia sikia habari za vijiweni unakuja anzisha uzi. Kijiweni mnadanganyana kuwa hapo jamaa wanaenda anguka.... Za kuambiwa changanya na zako
Shida ni kwamba umesoma juu juu then umekuja kuhukumu na wala hakuna sehemu niliyosema kuwa uchunguzi usifanyike.

Point yangu ni kwamba uchunguzi ufanyike lakini isitumike pressure au maoni ya mihemko kutoa hukum sabab wengi wanaoongea mitandaoni na hata ndani ya thread hii wanawaangushia jumba bovu hawa wanafunzi na wengi washatoa mpaka na hukumu
 
Kuna tofauti ndogo sana kati ya waandishi wa habari na wanasiasa na ufanano mkubwa hasa kwenye tabia ya kutumia mtu kujipatia umaarufu/au kile wanachokitaka
 
Kosa kubwa watakalolifanya Ardhi University ni kukiri kweli ulifanyika udaganyifu kama ilivyoelezwa na muhusika/wahusika. Itadhihirisha weakness kubwa katika hiyo taasisi na wahusika walioshindwa kudhibiti udanganyifu huo nao watapaswa kuwajibishwa pia.

Japo cheating ipo lakini kukiri waziwazi hii inazorotesha reputation ya taasisi
 
Dogo kubali umekurupuka. Wao wenyewe walisema watafanya uchunguzi. Sasa sijaona ambacho umeshauri kipya. Yaani umerudia kwa maelezo meeeeeeeeengi kitu ambacho walishasema watakifanya.
 
Nilichokidundua humu jf comment ya kwanza ndio huwa inareflect comment zinazofuata, na sio jf pekee hata huko u-tube. Vijana wa Tz wamekuwa wavivu kufikiri.
Comment ya kwanza ikiandika CHAI
Zinazofuata zote zinapita humo humo
Utasikia sukari imezidi
Mwingine anapost picha ya kamba
Kuepuka hilo uwe na id mbili
Unaandaa uzi kisha unapost halafu fast id nyingine inajibu
Utaona vichwa panzi wancyopita humo humo
 
Nmefurahi kumuona mtu ambae amefikiria nje ya box
 
nilikuwa nawazidi darasani wote, na nimewazidi hadi nilipofika form six kila shule ninayoenda.
Na kama hujabadilika aisee una kazi kubwa sana, dunia hii si ya kujitenga kiasi hicho, am sure hata kama umefanikiwa lakn ungefanikiwa zaidi ikiwa ungekuwa na backup na hazina ya watu ambao mlisaidiana huko shule!!
 
Nmefurahi kumuona mtu ambae amefikiria nje ya box
Umefurahi nini, kwani mbona hadi havard kuna watu wamekamatwa kwa academic cheating tena staff wa chuo imepunguza nini kwa chuo hiko? Na seif al islam chuoni London School of Economics ilipunguza nini kwa chuo? Wakibainika mapacha watakula nyundo ya seneti kama kawaida, si wa kwanza na wala hawatakuwa wa mwisho kudanganya na kuadhibiwa
 
Kwa hiyo hutaki wafanye uchunguzi au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…