Chuo cha Ardhi kuweni makini na huu mtego wa suala la mapacha kudai kufanyiana mtihani

Pale wasafi hakuna wahariri wa vipindi wenye akili na busara hii uliyo ongelea hapa.
 
Nami nikushangae kwa uchambuzi wako ambao haujashiba, chuo kimesema kinachunguza ukweli wa hizo taarifa, manake nini, ni pamoja na kutaka kujiridhisha majina ya wahusika, ikiwa ni pamoja na kuthibitisha pasipo shaka kuwa wamewahi kusoma na kuhitimu chuoni hapo.
Hitimisho taarifa ya matokeo ya uchunguzi ndo inapaswa kuja na yote uliohoji hapo
 
Chuo kifanye UCHUNGUZI, kama walikuwa wanafunzi basi Vyeti vyao vichanwe na washtakiwe..

Kama ikibainika siyo wanafunzi washtakiwe na Chuo kwa kukiharibia sifa ili iwe fundisho kwa watafuta kiki wengine wajao...
 
Na kama hujabadilika aisee una kazi kubwa sana, dunia hii si ya kujitenga kiasi hicho, am sure hata kama umefanikiwa lakn ungefanikiwa zaidi ikiwa ungekuwa na backup na hazina ya watu ambao mlisaidiana huko shule!!
Ulimuuliza amewazidi kimaisha? Mafanikio sio pesa tu majumba ama magari. Mtu kama Prof Shivji utasema hajafanikiwa? Sio tajiri wa kifedha ila wa elimu na wafuasi wanaoamini mawazo na mafundisho yake. Sawa tu mwl Nyerere.
 
Kukiri sio kosa kabisa ila ni njia mojawapo ya kutengeneza mifumo imara ya udhibiti. Ikitokea ni kweli, watajuta maisha yao yote maana ni wajinga mno
 
Mbona kama wewe unahusika. Umekuja kama kuwaatisha chuo cha Ardhi wasifanye chochote. Isitoshe wao wamesema wanafanya uchunguzi,sasa hiyo kukurupuka kwako na mihemko imetokea wapi?.

Hao mabinti wameyakoroga wenyewe,ujuaji mwingi,kutaka sifa sifa sana. Ndio hayo matokeo. Kwenye huu tu watapigwa sekeseke mpaka watamani kurudi utotoni.
 
Huyo jamaa kazingua ila hajui kazingua. Anajitahidi kutetea uozo ,sijui ana maslahi gani nao? Wahusika wamekiri ,yeye anakuja na ngonjera za sijui huo mtego sijui chuo kiwe makini.

Serikali kupitia chuo Cha Ardhi imeonesha umakini mkubwa sana Kwa kuamua kufanya uchunguzi , ingekaa kimya ningekilalamikia chuo
 
Muuza magari na mambo ya kitaaluma wapi na wapi!


We subiri watu
 
Bado mapacha wako wanayo kazi kubwa kama chuo kitasema ni uongo basi Mapacha na kituo cha Wasafi watafunguliwa case ya kuchafua chuo na watachukuliwa hatua kali na TCRA na bado mapacha watapelekwa mahakamani pamoja na wasafi maana hili ni swala la Elimu …kumfanyia myihani mtu ni kosa la jinai kisheria na kuna adhabu yake!
 
Kama watakuwa wamefanya kutafuta kiki bado kuna malipo ya madhara ya kilichofanyika….
 
We unajua maana ya uchunguzi? Porojo zote hizo mbona km kuitisha chuo isifanye uchunguzi. Umetumwa au ndio mhusika?
Hawezi kutisha Xhuo wewe
TV imesajiiliwa kama chombo serious cha habari na TCRA

Sio sehemu ya kudhaliilisha taasisi wale wamedhalilisha taasisi na kuvunja maadili ya kufanya mtihani bayo matokea yake ni kufutiwa degree kuwa walizipata kwa udanganyifu wote wawili
 
Mkuu, ata uki confess uku unagegeda as long as upo recorded, msala wa kujibu unao.
 
Chuo kinachunguza nini sasa? Ingekuwa mtu mwingine ndiyo ametoa tuhuma dhidi yao hapo ndiyo wangekuwa sahihi kusema wanachunguza. Hao wamekiri wenyewe kwenye media na ushahdi upo hivyo kinachopaswa ni kufanywa ni kuzifuta degree zao.
Ingekuwa ni taarifa iliyoandikwa au iliyokuwa reported angalau wangeweza kusema wanachunguza lakini siyo hiyo live interview, au wanachunguuza kama wakati wanatoa hiyo kauli walikuwa timamu au wamelewa?
 
Kwa sifa na ujunga wao wanajutia huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…