Chuo cha Biblia hapo hapo kwenye simu yako, bila kuathiri ratiba yako

Chuo cha Biblia hapo hapo kwenye simu yako, bila kuathiri ratiba yako

Raphael Mtui

Senior Member
Joined
Nov 26, 2024
Posts
141
Reaction score
317
Tangazo muhimu.

Chuo cha biblia hapo hapo kwenye simu yako, bila kuathiri ratiba zako

Bwana yesu asifiwe sana watumishi wa mungu. Mbarikiwe kwa kuendelea kuwa sehemu ya kazi hii.

Safari hii tumewaandalia mpango mkubwa kabisa wa baraka utakaoanza rasmi mwezi wa kumi 2025.

Sikiliza kwa makini kabisa, maana maisha yako yanatakiwa yabadilike kabisa kabisa kwa muda wa miezi kama minne.

Baada ya miezi minne hadi sita, utakuwa baraka kwa wengine, kanisani kwako, washirika wako na kwa maelfu ya wengine.

Iko hivi:

Kuanzia mwezi wa kumi tutakuwa na chuo cha biblia hapa hapa (group la, makala: la israeli na wokovu. Kama haupo tuwasiliane).

Tuna mpango kabambe wa kukupitisha kwenye kozi zote muhimu za chuo cha biblia.

Bila kuathiri ratiba yako, wala kazi yako, chuo cha biblia kitakufikia hapo hapo ulipo, tena kwa ubora unaotakiwa!

Ni vile tu kwamba hatutakupa cheti, lakini tunajua hautafuti 'recognition' bali unatafuta kukua kiroho na kutembea na mungu kwa viwango vingine, ili uwabariki na wengine, ufalme wa mungu ukue kwa kasi.

Kwa wewe ambaye unatarajia kumtumikia mungu usikose kabisa shule hii hasa kama umebanwa na mambo kiasi cha kushindwa kujiunga na chuo.

Kila mmoja anapaswa kusoma shule hii. Ni shetani peke yake anaweza kusema shule ya biblia haina umuhimu.

Hizi ndio njia tutakazotumia.

1)Kwa kila kozi, tumekuandalia notes tayari, ambazo zitakuwa mfumo wa PDF, zikiwa zimeshafupishwa kiweledi kabisa. Hivyo, huna kazi ya kuandika. PDF hizo hazizidi kurasa 20. Badala ya kusoma vitabu vikubwa au kadhaa kwa kozi moja, utasoma muhtasari makini unaojitosheleza.

2) Pili, kila kozi utapata kitu kinaitwa Study Guide, yaani mwongozo mdogo ambao lengo lake kuu ni kukupa zile pointi muhimu za lazima kabisa ambazo hutakiwi kuzisahau. Study guides zina kurasa kama tano tu.

3)Tatu, kwa kila kozi utapata video za mwalimu (Raphael Mtui) akikufundisha upate ufafanuzi zaidi.

4)Nne, kwa kila kozi utatengenezewa podcast, yaani audio fulani ambayo itakuwezesha kusikiliza somo huku unaendelea na kazi zingine. Audio hizi zitakusaidia hasa wakati utakosa kabisa muda wa kusoma notes utakazopewa.

5)Tano, ambalo ni muhimu sana, kila kozi itakuwa na darasa moja la 'live' (mubashara) ambalo litafanyikia google meet au zoom. Hapo tutakuwa wote live, mwalimu akiongea, maswali na majibu, mijadala, hapo ndipo panapopendeza sana na kutoa taswira halisi ya darasa, tena linalojengwa na watu kutoka kila pembe ya nchi. Usijali kuhusu Google Meet, au Zoom, sio jambo gumu hilo, anza kuzidownload zikae kwenye simu yako.

6)Sita, kwa kila kozi kutakuwa na mtihani mwishoni. Kufanya mtihani ni lazima, ila kukusanya mtihani kwa mwalimu sio lazima, ila tutafanya masahihisho pamoja. Ukitaka, tutakupa "Answer Key" ujisahihishie mwenyewe.


HIZI HAPA NI BAADHI TU YA KOZI AMBAZO UTAZIPATA:

1)KUITAMBUA BIBLIA (INTRODUCTION TO THE BIBLE)

Hii ndiyo kozi ya kwanza, ambapo tutaona vipengele vifuatavyo:

a) Biblia ni nini hasa. (Definition and origin of the word Bible)
b)Biblia ilipatikanaje. (How we got the Bible)
c)Jinsi vitabu 66 vya Biblia vilivyopatikana (Canonization of the Bible)
d)Ni nini kinaipa Biblia mamlaka (Authority of the Bible)
e)Biblia ilivyogusa jamii na historia (Impacts of Bible on the Society and the entire History)
f) Ni ushahidi gani wa kisayansi na kihistoria unaipa Biblia kuaminika kama Neno la Mungu. (Reliability of the Bible)
g)Biblia ilivyopangwa. (How is Bible organized)
h)Jinsi ya kuisoma Biblia kwa mafanikio (How to study the Bible effectively.)


2)APOLOJIA NA MAADILI YA UKRISTO. (APOLOGETICS AND CHRISTIAN ETHICS)

a)Maana ya apolojia ki-Biblia.
b)Majibu ya Biblia kwa wanaodai hakuna Mungu (Atheism)
e)Majibu ya Biblia kwa wanasayansi wanaochambua mwanzo wa ulimwengu.(Cosmological arguments)
f) Majibu ya Biblia kwa wanasayansi kuhusu ulimwengu ulivyopangika (Teleological argument)
g)Majibu ya Biblia kwa nadharia za Mungu ni wa kufikirika tu (Ontological Arguments)
h)Jinsi ya kujibu kwa upendo na hekima
i)Maadili ya Ki-Kristo yanavyotumika sambamba na apolojia kuonesha ushahidi mkuu wa uwepo wa Mungu.



3)KUPITIA AGANO LOTE LA KALE KWA NJIA RAHISI (OLD TESTAMENT SURVEY)

Katika kozi hii utapitishwa kwenye Agano la Kale kwa weledi utakaokufanya uijue Biblia kirafiki sana. Kila kitabu tutaangalia yafuatayo:

a) Kitabu kiliandikwa mwaka gani?
b)Nani aliandika?
c)Nani au kina nani waliandikiwa?
d)Somo kuu la kitabu hicho ni nini?
e)Kitabu hicho kimetoa picha gani ya kutabiri ujio wa Yesu? (Kila kitabu cha Agano la Kale kina kitu kinaitwa "Aina za Yesu" utashangaa kabisa)



4)KUPITIA AGANO JIPYA LOTE (NEW TESTAMENT SURVEY)

Kila kitabu tutaangalia:

a) Nani aliandika?
b)Lini kitabu kiliandikwa?
c) Aliwaandikia kina nani?
d) Mada kuu kwa kila kitabu ni ipi?
e)Somo kubwa kwetu leo la kila kitabu.


5)MAFUNZO YA HUDUMA NA UONGOZI.
Kwenye kozi tutaangazia yafuatayo:

a) Maana ya wito halisi na karama za Mungu.
b)Njia za kugundua wito wako na kuuendeleza.
c)Kuelewa maana ya uongozi kwa jicho la Kristo.
d)Tabia muhimu na lazima za kiongozi wa kiroho.
e)Namna ya kukabiliana na changamoto za uongozi.
f)Namna ya kuhubiri kwa matokeo mazuri.
g)Namna ya kufundisha kwa matokeo mazuri.

6) HOMILETICS: UFUNDI WA MAHUBIRI.

Kwenye kozi hii tutaangazia yafuatayo:

a)Kujua umuhimu wa tabia na sifa za mhubiri kabla ya mahubiri yako.
b)Kujua kanuni za kuzingatia uwapo madhabahuni
c) Kujua sifa za ujumbe bora wa kuleta mabadiliko.
d)kujua namna ya kupangilia ujumbe
e) Kujua makosa manne ya kuepuka kabisa kwenye ujumbe wako

7) MAISHA NA HUDUMA YA YESU.

a)Kueleza historia na utimilifu wa unabii wa maisha ya Yesu Kristo.
b) Kujua maana ya Yesu kuzaliwa horini na ujio wa mamajusi.
c)Kujua sababu na maana ya ubatizo wa Yesu.
d)Kuelewa aina za miujiza ya Yesu na maana zake.
e)Kujua mafundisho makuu matano ya Yesu.
f)Kuchambua Hotuba ya Mlimani na baraka nane (Beatitudes)
g)Maana ya kifo, ufufuo, na kupaa kwa Yesu Kristo.


8) UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIEL NA UFUNUO.

a)Kuujua ukweli wote kuhusu majuma 69 ya Daniel.
b)Kujua juma la sabini na jinsi linavyoingia kwenye ufunuo.
c)Kujua 'Gap Theory' inayoficha kipindi cha Kanisa (Church Age).
d)Kujua ratiba yote ya matukio ya mwisho wa dunia baada ya juma la sabini.
e)Kufafanua ndoto ya sanamu (Daniel 2)

9) KANUNI 10 ZA KUKUWEZESHA KUTAFSIRI MAANDIKO KWA USAHIHI (HERMENEUTICS)

Katika kozi hii utajifunza:

a) Kanuni ya kutii, (kutoweka gari (wazo lako) mbele ya punda (Neno la Mungu) ukitegemea asukume, weka nyuma avute)

b) Kanuni ya uvuvio, matumizi makuu matatu ya KILA andiko.

c)Kanuni ya muktadha (context)

d) Kanuni ya Yaliyomo. (Content)

e)Kanuni ya urahisishaji. (Simplification)

f) Kanuni ya upatano (Maandiko yanayoonekana kupinga mengine)

h) Kanuni ya Maagano (Kutofautisha Agano la Kale na Jipya)

i)Kanuni ya Ufalme: Jinsi ya kutasfiri ahadi za Mungu kwenye Biblia.

j) Jinsi ya Kutafsiri mifano ya Yesu.

k) Jinsi ya kutafsiri unabii katika Biblia.

Hatuwezi kuandika kozi zote kwa sasa. Kutakuwa na kozi muhimu sana kama kozi ya kupitia KWA UNDANI (sio survey) kitabu kimoja kimoja cha Biblia, Wokovu kwa jicho la ndani sana ki-Biblia, kozi pendwa ya Roho Mtakatifu, kozi ya nyaraka za Mtume Paulo, kozi ya Nyaraka za Wengine, Kozi pendwa ya Historia ya Kanisa, kozi ya Umisheni na Uinjilisti, kozi inayohusu dhambi, kozi inayohusu Utatu Mtakatifu, kozi ya Ukristo unavyosema kuhusu, Ndoa, mapenzi, utoaji mimba, pesa, na technolojia, Tutaendelea kuzitaja kwa urefu baadaye.

Tuna kozi kama 20 hadi 30, na tunatakiwa kuzimaliza kwa muda usiozidi miezi sita, ikiwezekana kwa miezi minne tumalize, ingawa itahitaji 'commitment' kali sana. Kila wiki tunapaswa kutumia wiki moja. (Kuna kozi chache ndefu itashindikana ila tutaangalia namna ya kufidia kwenye zile kozi fupi).


Kozi ya kwanza itatolewa hapa hapa bila kuchangia chochote.

Kwa kuwa kazi hii ni kubwa mno kwetu na inatugharimu kuiandaa, utachangia kidogo mno kila mwezi kuanzia mwishoni mwa mwezi wa kumi)

Kumbuka, tunaandaa mara mbilimbili, kwa maana ya wale wa Kiswahili na wale wa English. Kutakuwa na darasa la Kiingereza tu bila kuchanganya na Kiswahili. Tutatoa utaratibu baadaye.

Kila mwanafunzi atachangia ada ya sh. 30,000/= kila mwezi wakati huo wa masomo. Ina maana darasa likiisha kwa miezi sita, utakuwa umetoa ada ya kitu kama 180,000 tu. Linganisha na gharama ya kuacha shughuli zako na kwenda chuo, linganisha na ada ya chuo, linganisha na muda utakaotumia kukaa chuo, linganisha na gharama za nauli, chakula, gharama za kukaa chuoni, hakika ni milioni kadhaa zitaenda hadi mwaka mmoja tu uishe.

Kila kozi utakuwa umelipia kama 7,500 tu!

Vikwazo vya kushindwa kujiunga chuo visiwe sababu ya wewe kukosa 'madini' ya kukufanya utembee na Yesu viwango vingine! Tayari Mungu ametupa kuishi majira ambayo teknolojia inarahisisha mambo sana kiasi kwamba kuna mambo tutaenda kujibu kwamba tulishindwaje kufanya.

Moja ya kazi ndogo sana yenye baraka unayotakiwa kufanya, ni kusambaza taarifa hii. Mungu sio mrushi, atakulipa. Just kusambaza tu tangazo hili, mtu mmoja tu akapata elimu ya chuo, akasaidia watu mia, watu mia wakasaidia watu maelfu, haraka mno ufalme wa Mungu unabarikiwa.

Kwa kitendo kidogo tu cha kusambaza tangazo hili na kupigia watu ambao unajua kabisa wanampenda Mungu na wako tayari kutimika kwa kazi yake, utaubariki ufalme kwa namna ya ajabu kabisa.

Maombi yenu kwetu wakati tunapokimbizana katika kuandaa masomo haya, tupate kila kinachohitajika, ikiwemo pesa, vifaa, na tupate watu wa kufaa kutusaidia kazi hii kubwa, ikiwezekana na ofisi kwa ajili ya kufanyia kazi hii.

Wale wanaotaka huduma "premium" kutakuwa na uwanja wenu. Gharama zitakuwa elfu hamsini kwa mwezi.

Hawa ni wale wanaohitaji kufundishwa peke yao, mubashara peke yao, kila eneo wanahitaji faragha na mwalimu kutokana na huduma zinazowasubiria mbele yao au wanazofanya, au pengine mambo binafsi na siri mno waliyonayo, ninawakikishia kutunza mambo yao kama ambavyo nimetunza ya wengine hapa miaka yote tangu tuwe hapa.

Ukiwa na swali usisite kunipigia


0762731869 (Whatsapp)
0761346767 Piga muda wowote.

Link ya kuingia kundini hii hapa:
 
Inamfaa kila mtu hii kozi. Lugha rahisi ya kueleweka kabisa. Naomba niwaad kwenye group langu muwepo wakati kozi ya kwanza ikitolewa bure
 
Back
Top Bottom