FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
MUM wiyo chuo cha akiislam ni chuo cha Waislam. "Morogoro Muslim University" siyo (Morogoro Islamic University).Mimi ni mmoja wa Wanafunzi katika Chuo cha Kiislamu Morogoro, changamoto kubwa ambayo naiona kwenye chuo chetu ni suala la mazingira machafu.
Chuo hakina vifaa vya kuwekea taka hali inayofanya Wanafunzi wanaoishi kwenye Bweni kuwa wanatupa taka hovyo na kumwaga maji bila mpangilio maeneo ya nyuma ya jengo.
Wanajisaidia hovyo pia katika makorido kitu ambacho ni hatari kwa afya zao na hawa wengine wanaopatikana maeneo hayo ikiwemo Walimu wetu.
Kwa asilimia kubwa wafanyausafi pia hawana vitendea kazi wakati wa kufanya usafi kama vile viatu vigumu, hawana gloves n.k kwa ujumla hawana vifaa vya kufanyia usafi.
Maji pia ni kero maji yanasumbua chuoni, vyoo vinakuwa vichafu na hivyo kutishia usalama wa Watumiaji wote.
Kumbuka hilo.
.kama ni pachafu, uongozi haufati maadili ya Kiislam.