Chuo cha NDC chahitimisha mafunzo ya muda wa wiki 47, ujumbe watolewa "Tumieni maarifa kuimarisha ulinzi na maendeleo"

Chuo cha NDC chahitimisha mafunzo ya muda wa wiki 47, ujumbe watolewa "Tumieni maarifa kuimarisha ulinzi na maendeleo"

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
WhatsApp Image 2025-07-27 at 06.44.13_82e15839.jpg
Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College - NDC) kimehitimisha rasmi mafunzo ya muda wa wiki 47 (kuanzia Septemba 2024 hadi Julai 2025), kwa viongozi waandamizi wa Jeshi, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa Serikali, kutoka Tanzania na mataifa mengine.

Mafunzo hayo maalum ya ngazi ya juu yalijikita katika masuala ya Usalama na Mikakati (Security and Strategic Studies), na yalihusisha washiriki kutoka nchi 17 tofauti, yakiwemo mataifa ya Afrika na nje ya bara hilo.

Miongoni mwa wahitimu ni FRV. Said R. Mndeme, ambaye ni Mkurugenzi wa Miliki kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). FRV. Mndeme amehitimu mafunzo hayo na kutunukiwa Nembo ya Fahari ya NDC (Prestigious NDC TZ Symbol) pamoja na Shahada ya Uzamili katika Usalama na Mikakati (Master of Security and Strategic Studies).

Hafla ya mahafali ilifanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliwakilishwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stagomena Tax.

Katika ujumbe wake, Rais Samia aliwapongeza wahitimu wote na kuwataka kutumia elimu na maarifa waliyoyapata katika kukuza usalama, amani na maendeleo endelevu katika nchi zao. Alisisitiza kuwa changamoto za kiusalama katika enzi ya sasa zinahitaji viongozi wenye uelewa mpana na uwezo wa kimkakati katika kufanya maamuzi.

Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) ni taasisi ya juu ya kijeshi na kitaaluma inayotoa mafunzo ya kimkakati kwa viongozi wa juu wa sekta ya ulinzi, usalama na serikali, kikilenga kuwaandaa kwa nafasi nyeti za kufanya maamuzi katika mazingira ya usalama wa kikanda na kimataifa.

Kupitia mafanikio haya, FRV. Mndeme amejiunga na orodha ya viongozi wachache waliobobea kitaaluma katika nyanja ya usalama na mikakati, akitarajiwa kuchangia zaidi katika kuimarisha usalama, utawala bora na maendeleo ya taifa.
WhatsApp Image 2025-07-27 at 06.44.12_be575d51.jpg

WhatsApp Image 2025-07-27 at 06.44.13_7f15eaf5.jpg
 
Moja ya chuo kikubwa Chenye hadhi katika medani za ulinzi na Usalama barani Afrika
 
Back
Top Bottom