Chuo cha Usafiri wa Anga kutoa mafunzo ya urushaji drones kwa ada ya Tsh. 1,980,000 yatayoweza kuomba leseni ya urushaji TCAA

Chuo cha Usafiri wa Anga kutoa mafunzo ya urushaji drones kwa ada ya Tsh. 1,980,000 yatayoweza kuomba leseni ya urushaji TCAA

bwana wewee ni kama vi toy tu una install app ya dji kwenye simu unakiwasha unaki control nilidhani ni yale ma drone makubwa ya kijeshi ,watatuua hawa na vyanzo vyao vya mapato huwa nafanya hizi kazi za creativity ila watu washakata tamaa na hii serikali kufungua tu channel ya you tube sasa hivi uwe na milioni 3...yaani jamani nyieee
Hizi ni class ya D.I.Y. (Do It Yourself) kwa wale wanapenda Practical Electronics, huku wanafikiria utasafirisha wachaga wakati wa krisimasi hivyo utatengeneza hela.
 
Bei ya ada inalingana na bei ndege yenyewe,

Bei ya Drone hizi za maplastic ni ndogo - zingekuwa Drone za kivita hapo tunge elewa lakini hizi za DIY zenye user manual jinsi ya kuzirusha na kuziongoza kwa njia ya radio, wala huitaji kwenda darasani - hapo wanatafuta upigaji wa hela ndefu na mwisho wa siku wataleta sheria ya kusema kwamba husipo kuwa na liseni kutoka Chuo cha usafirishaji husirushe drone, huko ndiko tutakako kwenda muda si mrefu ujao, yanarudi yale yale ya kulazimisha maafisa Serikali kutumia mitandao ya TTCL.
 
Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania kitatoa mafunzo ya urushaji wa ndege zisizo na rubani (Drones) kwa muda wa wiki nne kuanzia Januari 4, 2021. Mwombaji awe na umri kuanzia miaka 21, awe amemaliza kidato cha nne au zaidi, ajue kusoma na kuandika Kiingereza. Ada ni TZS 1,980,000.

View attachment 1653607
View attachment 1653608
Kauli hizi jamani.
Eti mjiajiri unaamua kununua kadrones ili ufungue hata video productions.
Harafu unakuja utaratibu wa kulipa ili upate mafunzo kwa hela mingi mafunzo ya mwezi mmoja.
Ila any way
 
Nauliza hivi kwani hauwezi ukawa unashoot video yako kwa drone bila kibali na usipatikane?
Tuliwahi kutengeneza series flani hapo Mwananyamala, tulitumia drones bila kuomba kibali popote

Nadhani ishu ipo kama utataka kushot maeneo ya mjini kabisa
 
Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania kitatoa mafunzo ya urushaji wa ndege zisizo na rubani (Drones) kwa muda wa wiki nne kuanzia Januari 4, 2021. Mwombaji awe na umri kuanzia miaka 21, awe amemaliza kidato cha nne au zaidi, ajue kusoma na kuandika Kiingereza. Ada ni TZS 1,980,000.

View attachment 1653607
View attachment 1653608
Huku mtaani tunajifunza kuendesha drones kwa kuangalia YouTube na kufundishwa na wapiga picha mtaani, wengi tunarusha drones bila hata ya kupitia chuo tena tunajifunza kwa siku moja tu,chombo hicho angani na kupiga picha kama loote.
 
Sasa nmeelewa n kwann hatukufundishwa jinsi ya kurusha drones tulivyokuwa darasani kusomea fani ya mambo ya uandaaji wa filamu
 
Hiyo 1,980, 000/= fanya hivi nenda kijiji cha Mwarazi mgeta pale morogoro tafuta shamba kwa bei nafuu kabisa lima cabbage kwa hekta kumi kwa miezi tatu. Matokeo utayaona sio huu ujinga wa serikali
Hahahahah, ungemalizia "Hakikisha unaziuzia shamba kabla viherehere kutoka mamlaka ya mapato hawajang'aa shambani kwako"
 
Hiyo 1,980, 000/= fanya hivi nenda kijiji cha Mwarazi mgeta pale morogoro tafuta shamba kwa bei nafuu kabisa lima cabbage kwa hekta kumi kwa miezi tatu. Matokeo utayaona sio huu ujinga wa serikali
Wanaolima cabbage wapo wanaendelea na sisi wa drone tunaendelea, unataka nchi nzima wote tuwe wakulima?
 
Huku mtaani tunajifunza kuendesha drones kwa kuangalia YouTube na kufundishwa na wapiga picha mtaani, wengi tunarusha drones bila hata ya kupitia chuo tena tunajifunza kwa siku moja tu,chombo hicho angani na kupiga picha kama loote.

Tatizo kubwa la taasisi zetu za UMMA ni ukosefu wa ubunifu, wana pounce kwa kila kitu ambacho wanaweza ku-make easy money.

Hao walimu wa Chuo cha usafirishaji wanaweza kueleza wananchi walisomea Chuo gani kozi ya kurusha DIY drones, kama Drones zingekuwa zinaundwa hapo chuoni walao tungeweza kuwaelewa.

Ukweli ni kwamba na wao wanajifunza kwa kuangalia video clips kutoka UTube halafu wanakuja kuzuga watu. Hivi wanaweza kweli ku-justify ulipaji wa karibu million mbili kwa kile wanacho kiita kozi ya wiki mbili ya urushaji Drones za plastic - huu kama sio wizi wa mchana tuiiteje.
 
Hiyo 1,980, 000/= fanya hivi nenda kijiji cha Mwarazi mgeta pale morogoro tafuta shamba kwa bei nafuu kabisa lima cabbage kwa hekta kumi kwa miezi tatu. Matokeo utayaona sio huu ujinga wa serikali
Katika watu ambao akili hawana na wewe umo

Wewe DRone unajua hicho kikamera chako cha kurusha hewani kupiga picha za harusi!!!

Mwendesha drone anaitwa Drone pilot au drone operator ni kazi nzito ambako tuendako itaajiri watu wengi mno kwa kazi ya kusafirisha parcel ndogo ndogo au vifurushi toka sehemu moja kwenfda nyingine yaani courier servises

Mfano Rwanda hapo kuna pilot wa Drone anasafirisha damu au madawa toka mijini hadi dispensary ziliko vijijini ambako hakuna barabara wala nini kwa wakati

Anapakia ki drone chake madawa anakirusha kinatiua mzigo kinageuza

Chuo Cha anga kinaenda kufundisha u pilot wa Drones hiyo pesa ya ada ndogo subiri watu waende hii awamu kama inayofuata soko likilipuka kama usipolipa ada milioni kumi husomi ndipo kichwa chako kitakukaa vizuri

The Medical Drone Delivery Pilot​

Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania kitatoa mafunzo ya urushaji wa ndege zisizo na rubani (Drones) kwa muda wa wiki nne kuanzia Januari 4, 2021. Mwombaji awe na umri kuanzia miaka 21, awe amemaliza kidato cha nne au zaidi, ajue kusoma na kuandika Kiingereza. Ada ni TZS 1,980,000.

View attachment 1653607
View attachment 1653608
Yaani Bongo si ajabu Mr Kuku aliweza kukusanya mabilioni ya TZ, yaani hawa wasomi wetu wamekaa wakaona kuna mtu atatoa milioni 1.8 kwenda kusomea urushaji wa drone, drone hizi za kupiga picha! wakati huo huo sheria yao haikuruhusu kurusha drone bila kibali, baada ya mafunzo hii knowledge unaenda kuapply wapi? Kina milard Ayo wanapiga picha za drone kila siku wamejifunza wapi? tunarusha madrone kwa ajili ya kupiga picha na hatujawahi soma chuo chochote. Hebu njooni na mikakati endelevu wakuu.
 
Huku mtaani tunajifunza kuendesha drones kwa kuangalia YouTube na kufundishwa na wapiga picha mtaani, wengi tunarusha drones bila hata ya kupitia chuo tena tunajifunza kwa siku moja tu,chombo hicho angani na kupiga picha kama loote.
Ipo sheria inayozuia kurusha drones bila kuwa na leseni ya kufanya hivyo. Siku wakianza kuitekeleza itakuwa vilio na kusaga meno. Kumbuka kutokujua sheria si kinga ya kutoshtakiwa.
 
Ipo sheria inayozuia kurusha drones bila kuwa na leseni ya kufanya hivyo. Siku wakianza kuitekeleza itakuwa vilio na kusaga meno. Kumbuka kutokujua sheria si kinga ya kutoshtakiwa.
Najua kuna sheria ya kurusha drone,lakini hakuna sheria kuwa ili upate leseni lazima usome hiyo kozi ya kurusha drone,hapo ndio changamoto,kwani sio kila mtu atakuwa na hiyo 1.4m wakati na si lazima usome ndio uelewe jinsi ya kuendesha hizi drones,mbona tunajua kuendesha na hatujaenda chuo?
 
Tatizo kubwa la taasisi zetu za UMMA ni ukosefu wa ubunifu, wana pounce kwa kila kitu ambacho wanaweza ku-make easy money.

Hao walimu wa Chuo cha usafirishaji wanaweza kueleza wananchi walisomea Chuo gani kozi ya kurusha DIY drones, kama Drones zingekuwa zinaundwa hapo chuoni walao tungeweza kuwaelewa.

Ukweli ni kwamba na wao wanajifunza kwa kuangalia video clips kutoka UTube halafu wanakuja kuzuga watu. Hivi wanaweza kweli ku-justify ulipaji wa karibu million mbili kwa kile wanacho kiita kozi ya wiki mbili ya urushaji Drones za plastic - huu kama sio wizi wa mchana tuiiteje.
Mkuu umeshamaliza kwanza hata wao hawajui kuendesha hizo drones ila naona ni kama wanabuni kamradi fulani,drones zipo siku nyingi na watu wengi wanajua kuziendesha kwa vitendo na si kwa nadharia sasa leo utake eti muendesha drones ajifunze kwa mwezi mzima wakati ni kitu cha masaa 2 na kama mzito kuelewa basi ni siku moja tu unarusha chombo angani.Kuhusu sheria ya kujisajiri hiyo ni sawa na ipo karibu mataifa yote,lakini la kwenda kusugua makalio darasani mwezi mzima na milioni jua yake eti unajifunza kuwa pilot wa drone naona huu ni wizi wa mchana na kutaka sifa tu,wabuni vyanzo vingine vya mapato. Wakati mwingine ndio maana tunawapa sifa wazungu na mataifa mengine kwa kuweza kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wao na sio kufanya changamoto ziwe fursa kwa kuwakandamiza wananchi wao,kwa sasa tutambiwa tulipie hata pumzi tunayopumua,kila kitu malipo sijui tunaelekea wapi.
 
Back
Top Bottom