Chuo cha Usafiri wa Anga kutoa mafunzo ya urushaji drones kwa ada ya Tsh. 1,980,000 yatayoweza kuomba leseni ya urushaji TCAA

1.
Hivi kurusha aina yeyote ile tanzania ni lazima upate mafunzo na leseni? Yaani nazungumzia drone zile simple tu unarusha zina camera unarikodi na kupiga picha nazo pia unataka leseni? Maana mimi najua kurusha hizi na nimejifunza kwa rafiki yangu tu na hata haikuchukua zaidi ya saa moja kuweza kuweza kuirusha! Huku kwa mama msuka nywele hata watoto wadogo tu wanazirusha bila leseni wala age restrictions.

2.
Hivi drone za kubeba mizigo ziko nyingi Tanzania? ni makampuni mangapi wanamililki na yanatumia drone kusafirisha mizigo yao? Maana naona bei ya masomo ni kubwa mno kiasi kwamba kama mtu ana pesa zote hizo na hana hope ya kupata kazi baada ya kujifunza naona ni bora mtu achukue pesa hizo akatafute shamba japo la kukodi apige kazi kuliko kununua karatasi tu.
 
L
Lengo ni kukomoa wananchi masikini
 
Tafuta kwanza hela unaweza kusoma hata nje ya nchi.
 
Yaani kurusha tu ndo iwe gharama yote hiyo? A mere UAV platform flying ndo kuwe na gharama zote hizo? Kwanza kurusha huko ni kwa ajili ya kupata nini, kusafirisha mizingo, UAV photogrammerty, au kuchukua picha kwa ajili ya waandishi wa habari? Gharama hii inacover data processing and analysis pia? Nje na hapo hii ina ukakasi!
 

Gharama ya kusoma kwa wiki nne ni zaidi ya ada ya mwaka mzima ya shahada ya awali Chuo kikuu cha Dar es salaam ama Dodoma ama Sokoine
 
Maendeleo Haya Chana au nasema huongo ndugu zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…