Chuo gani bora cha kusoma Bachelor of Law kati ya hivi?

Chuo gani bora cha kusoma Bachelor of Law kati ya hivi?

Nje ya Mada:

Wazazi ninawaasa jamani wazazi mnaotumia pombe kali keivant minyagi na mipombe mingine mibia mingano jamani wazazi chonde chonde wazazi pombe mnazokunywa msiwape watoto, kuna wazazi ni vichwa maji anataka familia yake yote wawe walevi wanywa pombe kwa hio anaanza kuwabugiza watoto pombe wakiwa watoto yaan mzazi unawanywesha watoto konyagi kweli?

Kweli mzazi watoto miaka 3-8 unapigisha nyagi kisa unataka nao waje kua wanywa pombe? Hii hapana kabisa, ipo hivi kuna mtoto hapa jirani anapitia changamoto ya kuugua kifua kisichoisha na usiku anapata tabu sana anapolala kifua kinambana vibaya mno pia ana tatizo la kukojoa, sasa ipo hivi huyu mtoto mzazi wake akiacha kumpigisha tungi hio hali inapungua hakojoi wala kifua hakibani ila kuna muda anaanza kumpigisha tungi sana sana konyagi chupa ndogo kubwa zimejaa kwenye fridge watoto kila wakifungua fridge wanazikuta na muda mwingine wanataka wanywe nae maana ananywea nyumbani sometimes kwa hio hali inakua mbaya mtoto analala kwa tabu sana unaweza kumhurumia kifua km kimepasuka eksozi anavyokoloma km kifua kimetoboka na anajikojolea mbaya zaidi ni mtoto wa miaka 8 tu, mzazi unamnyweshaji mtoto pombe kali? Mboni wazazi mnapenda kutesa watoto, mtoto na pombe kali wapi na wapi?

Huu ni ukatiri kwa watoto ningeomba Muheshimiwa Waziri na mamlaka zinazohusika na Watoto wajaribu kuwaasa wazazi wenye tabia km hizi waache mara moja kuna wazazi ni vichwa vibovu kabisa
 
Kama alisoma Diploma Chuo cha Uongozi wa Mahakama naamini yupo vizuri maana kile chuo nakifahamu wanafundisha vizuri sana na wanafunzi wao ni very competent unaweza kumuweka meza moja na mwanafunzi wa Bachelor degree na akamshinda kwa nyanja nyingi.

Ninachotaka kusema ni kwamba chuo chochote kati ya hivyo aende tu atafanya vema sana maana masomo mengi atakayosoma huko almost 90% ni yale yale aliyosoma Diploma.
Mimi siyo mwanasheria Ila napinga hoja ya kusema mwanafunzi wa diploma ya sheria toka chuo Cha Lushoto atamshinda au bora kuliko wa bachelor degree ya sheria wa chuo chochote.

Zaidi ya kumshinda kazi za kikarani wa mahakama hawezi kuzichambua sheria kiundani zaidi yake wala kuandika vitu kwa mtiririko wanaofundishwa kwenye bachelor degree.

Hawezi ku apply logic kufikia conclusion kama mtu wa bachelor degree.
Wewe ni kati ya waliopitia chuo unachosifia au waliokosa direct entry ya bachelor of law wakati unasoma.
Au ulikosa admission UDSM enzi hizo.
 
Mimi siyo mwanasheria Ila napinga hoja ya kusema mwanafunzi wa diploma ya sheria toka chuo Cha Lushoto atamshinda au bora kuliko wa bachelor degree ya sheria wa chuo chochote.
Zaidi ya kazi za kikarani wa mahakama hawezi kuzichambua sheria kiundani, wala kuandika vitu kwa mtiririko wanaofundishwa kwenye bachelor degree.
Wewe ni Kati ya waliopitia chuo unachosifia au waliokosa direct entry ya bachelor of law wakati unasoma.
Au ulikosa admission UDSM enzi hizo.
Huyo jamaa yupo sahihi usifikirie anakwambia uongo huo ndio uhalisia wenyewe
 
Huyo jamaa yupo sahihi usifikirie anakwambia uongo huo ndio uhalisia wenyewe
Hakuna kitu kama hicho
Siyo wajinga walio andaa kozi za bachelor degree.
Tatizo hapo watoto wa 1996 hadi 2020 wengi (siyo wote) hawana umakini na mambo. Siyo kosa lao, elimu ya msingi na sekondari imevurugwa sana. Ukiongeza na distractions za teknolojia ni shida zaidi.
 
Umekaririshwa vibaya sana. Usiishi kwa mazoea ishi kiuhalisia.

Hakuna kitu kipya kinachofundishwa Udsm ambacho hakifundishwi vyuo vingine.

Mwanafunzi aliyehitimu bachelor ya sheria Udsm hana tofauti na mhitimu wa diploma kutoka chuo cha uongozi wa mahakama Lushoto.

Hili tulilishuhudia kipindi cha field baada ya ofisi kupokea wanafunzi wa field kutoka vyuo mbalimbali kwa level mbalimbali kama certificate, diploma na degree.

Aise wanafunzi wa diploma kutoka Chuo cha uongozi wa mahakama walikuwa wanawaelekeza kazi mbalimbali wanafunzi wa degree wakiwemo wa Udsm.

Ilifikia mahali mahakimu walikuwa wanawaamini zaidi wanafunzi wa diploma kuliko wa degree maana walikuwa wepesi kuelewa na kufanya kazi kwa usahihi.

Sasa wewe kariri eti Udsm ndicho chuo bora wakati kwenye uhalisia ni weupe vichwani wanashindwa kazi na wanafunzi wa stashahada.
Acha chuki kijana. Yaani vipanga waliopata nafasi UDSM wazidiwe na vilaza wa Lushoto? UDSM bado ni namba moja kwa hapa Tanzania hasa hiyo sheria.
 
Kuna module gani tofauti inayofundishwa Udsm ambapo vyuo vingine havifundishi?

Tatizo baadhi ya watu mnaishi kwa kukariri vitu visivyo na uhalisia kwa kuaminishwa ujinga.

Niliomba vyuo vitano nikapta vyote ikiwemo Udsm lakini sikuconfirm Udsm maana ni chuo cha kawaida sawa na vingine tu.
So mkuu wewe uliconfirm kipi na kwanini?
 
Mimi siyo mwanasheria Ila napinga hoja ya kusema mwanafunzi wa diploma ya sheria toka chuo Cha Lushoto atamshinda au bora kuliko wa bachelor degree ya sheria wa chuo chochote.
Zaidi ya kazi za kikarani wa mahakama hawezi kuzichambua sheria kiundani, wala kuandika vitu kwa mtiririko wanaofundishwa kwenye bachelor degree. Hawezi ku apply logic kufikia conclusion kama mtu wa bachelor degree.
Wewe ni kati ya waliopitia chuo unachosifia au waliokosa direct entry ya bachelor of law wakati unasoma.
Au ulikosa admission UDSM enzi hizo.
Mkuu soma na uelewe.Ni hivi kijana kamaliza diploma chuo cha Lushoto mwa huu,,sasa anaaplly kusoma Degree.Swali ni kwamba amepata kwenye vyuo vyote nilivyovitaja isipokuwa UDSM ndo maana nikauliza je aconfirm chuo kipi Bora kati ya hivyo vyuo vikuu?So mkuu hebu mshauri kulingana na ubora wa Chuo katika kutoa wahitimu mahili
 
So mkuu wewe uliconfirm kipi na kwanini?
Tumaini University kwasababu ni chuo kizuri hasa kwenye upande wa sheria. Kile chuo kipo chini ya Waingereza japo Kanisa ni kama wasimamizi hivyo licha ya kutoa elimu ya viwango vya juu pia vinazingatia sana maadili ya mwanachuo kuanzia kwenye mavazi hadi maadili ya kiroho.
 
Mkuu soma na uelewe.Ni hivi kijana kamaliza diploma chuo cha Lushoto mwa huu,,sasa anaaplly kusoma Degree.Swali ni kwamba amepata kwenye vyuo vyote nilivyovitaja isipokuwa UDSM ndo maana nikauliza je aconfirm chuo kipi Bora kati ya hivyo vyuo vikuu?So mkuu hebu mshauri kulingana na ubora wa Chuo katika kutoa wahitimu mahili
Aendee Mzumbe University tena haraka zaidi
 
Acha chuki kijana. Yaani vipanga waliopata nafasi UDSM wazidiwe na vilaza wa Lushoto? UDSM bado ni namba moja kwa hapa Tanzania hasa hiyo sheria.
😂😂 Pole sana mkuu inaonekana bado unaishi karne ya 20 ya kudanganyana.

Nili apply vyuo vitano ikiwemo UDSM na vyote nilipata lakini sikutaka kwenda UDSM kwasababu unasoma miaka minne halafu hakuna kipya tofauti na vyuo vingine kama Mzumbe na Tumaini vinavyotoa course ya sheria kwa miaka mitatu na idadi ya modules unazosoma ni zile zile.
 
Mkuu soma na uelewe.Ni hivi kijana kamaliza diploma chuo cha Lushoto mwa huu,,sasa anaaplly kusoma Degree.Swali ni kwamba amepata kwenye vyuo vyote nilivyovitaja isipokuwa UDSM ndo maana nikauliza je aconfirm chuo kipi Bora kati ya hivyo vyuo vikuu?So mkuu hebu mshauri kulingana na ubora wa Chuo katika kutoa wahitimu mahili
Sikukujibu wewe. Nilitaka kuweka record sawa kwa jamaa aliye potosha ubora wa wanafunzi wa diploma vs degree ya sheria.
Nilikuelewa vizuri tu nikaacha wenye majibu ya swali lako waje kukujibu.
 
Mimi siyo mwanasheria Ila napinga hoja ya kusema mwanafunzi wa diploma ya sheria toka chuo Cha Lushoto atamshinda au bora kuliko wa bachelor degree ya sheria wa chuo chochote.

Zaidi ya kumshinda kazi za kikarani wa mahakama hawezi kuzichambua sheria kiundani zaidi yake wala kuandika vitu kwa mtiririko wanaofundishwa kwenye bachelor degree.

Hawezi ku apply logic kufikia conclusion kama mtu wa bachelor degree.
Wewe ni kati ya waliopitia chuo unachosifia au waliokosa direct entry ya bachelor of law wakati unasoma.
Au ulikosa admission UDSM enzi hizo.
Imeshasema wewe sio mwanasheria halafu unapingana na mtu aliyesoma sheria, hii imekaaje?

Nili apply vyuo vitano nikapta vyote ikiwemo UDSM lakini sikwenda UDSM kwasababu unasoma miaka minne wakati vyuo kama Mzumbe na Tumaini unasoma miaka mitatu na modules ni zile zile unazosoma UDSM.

Nilichogundua miaka minne ya UDSM ni kwamba kwa semester unasoma sessions chache tofauti na Mzumbe ama Tumaini ambapo unasoma sessions nyingi ili ku cover gap la mwaka mmoja.

Lakini masomo ni yale yale na tulikuwa tunakutana discussion na wanachuo kutoka vyuo mbalimbali hakuna cha ziada wanachosoma UDSM ni yale yale tu mkuu.

Watu wengi wanasomea majina ya chuo wakidhani kuna cha ziada wanapata kumbe ni juhudi na kujiongeza tu hata usome chuo chochote kama huna juhudi supp ama repeat course zitakuhusu tu.
 
😂😂 Pole sana mkuu inaonekana bado unaishi karne ya 20 ya kudanganyana.

Nili apply vyuo vitano ikiwemo UDSM na vyote nilipata lakini sikutaka kwenda UDSM kwasababu unasoma miaka minne halafu hakuna kipya tofauti na vyuo vingine kama Mzumbe na Tumaini vinavyotoa course ya sheria kwa miaka mitatu na idadi ya modules unazosoma ni zile zile.
Acha kujipa moyo. Kama hukutaka kwenda UDSM hizo ni shida zako binafsi ila UDSM bado ni chuo bora.
 
Sikukujibu wewe. Nilitaka kuweka record sawa kwa jamaa aliye potosha ubora wa wanafunzi wa diploma vs degree ya sheria.
Nilikuelewa vizuri tu nikaacha wenye majibu ya swali lako waje kukujibu.
Degree ya sheria wanasoma theory mwanzo mwisho wanaenda field mara moja lakini wale wa Lushoto huwa wanaenda mahakamani mara kwa mara ku practice.

Diploma wa Lushoto ana uwezo wa hadi wa kuandaa judgment ukimpa proceedings ya kesi nzima lakini vijana wengi wa Degree wanakwama.

Kijana wa bachelor degree anaambiwa aandae plaint au Written statement of defence anashindwa kwasababu anasoma zaidi nadharia tofauti na mwenzake anayeanza ku practice mahakamani mara kwa mara.

Naongea haya from my experience nimejionea mahakimu wenyewe wanazungumzia hili na huwa wakiacha kazi kwa wanachuo wa Lushoto wanajua kazi itakamilika ipasavyo.
 
Mkuu, huyu kijna kamaliza Diploma ya sheria kutoka chuo cha Lushoto mwaka huu na ameclear so akawa ameomba sasa law lakini UDSM hakupata nadhani labda waliishachagua vipanga wao mapema , ngo kaambiwa aconfirm kati ya hivyo hapo.So kwa uelewa wenu , please mpe ushauri
Mzumbe
 
Acha kujipa moyo. Kama hukutaka kwenda UDSM hizo ni shida zako binafsi ila UDSM bado ni chuo bora.
Ubora wake ni upi ukilinganisha na vyuo vingine?

Kwamba mwanafunzi hata asipojisomea kwa juhudi anafaulu tu kutokana na ubora wa chuo?

Ni sawa na mtu anayeamini private schools ni bora zaidi kuliko government schools wakati kuna watoto wanasoma government schools lakini kwakuwa wana juhudi na kujituma wanawakimbiza hata wale wa private school.

Hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kinachoitwa chuo bora na ufaulu bali uhusiano wa moja kwa moja upo kati ya kusoma kwa bidii na kufaulu bila kujali chuo gani unasoma.
 
Back
Top Bottom