Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam walaani kitendo cha udhalilishaji na shambulizi lililohusisha wanafunzi

View attachment 3310482

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: KULAANI KITENDO CHA UDHALILISHAJI NA SHAMBULIZI LILILOHUSISHA WANAFUNZI

Dar es Salaam, 20 Aprili 2025
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinasikitika na kulaani vikali tukio la kushambuliwa, kudhalilishwa, na kudhuriwa kwa msichana mmoja (jina lake bado halijatambulika) linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia picha mjongeo, linalodaiwa kuwa wahusika ni wanafunzi.

Tayari, Chuo kinafatilia taarifa za tukio hilo kwa kiini ili kubaini uhalisia wake; na utambulisho wa wahusika. Endapo itabainika kuwa wahusika ni wanafunzi wa UDSM, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya UDSM. Aidha, Chuo kitashirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa Sheria za nchi zinazingatiwa.

UDSM inapinga aina yoyote ya ukatili, udhalilishaji au uvunjaji wa haki za kibinadamu ndani na nje ya mazingira ya Chuo. Pia, UDSM itasimama imara kulinda utu, usalama, na hadhi ya kila mwanafunzi na wanajumuiya wengine wa Chuo bila upendeleo. Kwa mantiki hiyo, Chuo kinatoa rai kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu, na miongozo ya chuo; na maadili ya Kitanzania.

Prof. William A. L. Anangisye
MAKAMU MKUU WA CHUO
Vijana wadogo wametudhalilisha pia wamelidhalilisha Taifa. Wazazi wanahangaika kulipa ada wao wanafanya mambo ndio siyo
 
Ikithibitika, pasina shaka kwamba ni wanafunzi wa UDSM,

basi pamoja na hatua nyingine muhimu za kinidhamu na kisheria,
wanafunzi hao kwa ujumla wao, waondolewe mara moja kwenye hostels za chuo hicho mpaka pale itakavyoamuliwa vinginevyo miaka ijayo 🐒
 
Mambo niaje wadau.

Leo katika pitapita yangu online nimekutana na hizo videos za wanafunzi wa udsm

Hivi inawezekanaje kumnyanyasa mwenzao kiasi kile? Wanawake mbadirike fanyeni kazi njaa sio nzuri kabsa

Ule ni uovu kabsa ,Wazazi watoto wenu wako chuo muwakumbushe sana maisha.
 
Au "teeth" wanacheza na akili zetu kupotezea ishu ya lissu
1) Manara na mkewe=Alipokamatwa Lisu.Nyongeza ushindi wa Simba.Vipi ile ajali ya mkurugenzi wa Taa giza?????

2) Wanafunzi wa chuo kudhalilishana=Tamko la maaskofu plus kusikilizwa kesi ya Lisu .Nyongeza utambulisho wa mke mtarajiwa wa Manara plus Simba walivyokosa goli!

Nb: Hii ipo dunia nzima na kwenye serikali zote! Zima mijadala yenye tija coz nyumbu ni wengi na sisi ni wachache, hivyo wakianza kujadili vitu vya msingi kuna uwezekano mkubwa wakaja kujitambua!

Mfano mzuri siku tukianza kujadili kuwa askari, wanajeshi,usalama n.k kwa wingi wao plus wetu hata kama wanazo silaha unadhani wanaweza kutuua wote na kutumaliza halafu wao wakabaki salama????
 
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinasikitika na kulaani vikali tukio la kushambuliwa, kudhalilishwa, na kudhuriwa kwa msichana mmoja (jina lake bado halijatambuliwa) linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia picha mjongeo, linalodaiwa kuwa wahusika ni wanafunzi.

Tayari, Chuo kinafuatilia taarifa za tukio hilo kwa kiini ili kubaini uhalisia wake; na utambulisho wa wahusika. Endapo itabainika kuwa wahusika ni wanafunzi wa UDSM, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya UDSM. Aidha, Chuo kitashirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa Sheria za nchi zinazingiatiwa.

UDSM inapinga aina yoyote ya ukatili, udhalilishaji au uvunjaji wa haki za kibinadamu ndani na nje ya mazingira ya Chuo. Pia, UDSM itasimama imara kulinda utu, usalama, na hadhi ya kila mwanafunzi na wanajumuiya wengine wa Chuo bila upendeleo. Kwa mantiki hiyo, Chuo kinatoa rai kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu, na miongozo ya chuo; na maadili ya Kitanzania.
KURIPOTI HABARI AMBAYO TAYARI IMESHARIPOTIWA HUO NI UZWAZWA
 
Back
Top Bottom