Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam walaani kitendo cha udhalilishaji na shambulizi lililohusisha wanafunzi

View attachment 3310482

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: KULAANI KITENDO CHA UDHALILISHAJI NA SHAMBULIZI LILILOHUSISHA WANAFUNZI

Dar es Salaam, 20 Aprili 2025
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinasikitika na kulaani vikali tukio la kushambuliwa, kudhalilishwa, na kudhuriwa kwa msichana mmoja (jina lake bado halijatambulika) linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia picha mjongeo, linalodaiwa kuwa wahusika ni wanafunzi.

Tayari, Chuo kinafatilia taarifa za tukio hilo kwa kiini ili kubaini uhalisia wake; na utambulisho wa wahusika. Endapo itabainika kuwa wahusika ni wanafunzi wa UDSM, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya UDSM. Aidha, Chuo kitashirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa Sheria za nchi zinazingatiwa.

UDSM inapinga aina yoyote ya ukatili, udhalilishaji au uvunjaji wa haki za kibinadamu ndani na nje ya mazingira ya Chuo. Pia, UDSM itasimama imara kulinda utu, usalama, na hadhi ya kila mwanafunzi na wanajumuiya wengine wa Chuo bila upendeleo. Kwa mantiki hiyo, Chuo kinatoa rai kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu, na miongozo ya chuo; na maadili ya Kitanzania.

Prof. William A. L. Anangisye
MAKAMU MKUU WA CHUO
Poleni sana udsm

Bahati mbaya hao mabinti ni adults
 
Mfano mzuri siku tukianza kujadili kuwa askari, wanajeshi,usalama n.k kwa wingi wao plus wetu hata kama wanazo silaha unadhani wanaweza kutuua wote na kutumaliza halafu wao wakabaki salama????
Hawawezi hata robo
 
Chuo kipo kimya kwa mambo yote yanayoendelea Nchini ila wamejitokeza kwenye mambo ya vyupi hovyo kabisaa...hata tulipoambiwa kutoa umeme Ethiopia ni gharama nafuu kuliko bwawa la Nyerere wapo kimya kama wapo China.
 
Nilikuwa natazama hiyo taarifa, ila katika uandishi wake nimebaini kuwepo kwa makosa mawili ambayo yapo wazi kabisa. Nashukuru kuona mpangilio mzuri wa taarifa ya profesa toka udsm.
 
Chuo kipo kimya kwa mambo yote yanayoendelea Nchini ila wamejitokeza kwenye mambo ya vyupi hovyo kabisaa...hata tulipoambiwa kutoa umeme Ethiopia ni gharama nafuu kuliko bwawa la Nyerere wapo kimya kama wapo China.
Kweli aisee
 
Chuo graduate wake pekee anaefahamika sana ni Mwijaku unategemea nini?
 
View attachment 3310482

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: KULAANI KITENDO CHA UDHALILISHAJI NA SHAMBULIZI LILILOHUSISHA WANAFUNZI

Dar es Salaam, 20 Aprili 2025
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinasikitika na kulaani vikali tukio la kushambuliwa, kudhalilishwa, na kudhuriwa kwa msichana mmoja (jina lake bado halijatambulika) linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kupitia picha mjongeo, linalodaiwa kuwa wahusika ni wanafunzi.

Tayari, Chuo kinafatilia taarifa za tukio hilo kwa kiini ili kubaini uhalisia wake; na utambulisho wa wahusika. Endapo itabainika kuwa wahusika ni wanafunzi wa UDSM, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya UDSM. Aidha, Chuo kitashirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kuwa Sheria za nchi zinazingatiwa.

UDSM inapinga aina yoyote ya ukatili, udhalilishaji au uvunjaji wa haki za kibinadamu ndani na nje ya mazingira ya Chuo. Pia, UDSM itasimama imara kulinda utu, usalama, na hadhi ya kila mwanafunzi na wanajumuiya wengine wa Chuo bila upendeleo. Kwa mantiki hiyo, Chuo kinatoa rai kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu, na miongozo ya chuo; na maadili ya Kitanzania.

Prof. William A. L. Anangisye
MAKAMU MKUU WA CHUO
Na safari yae kielimu imeishia hapo, kisa nn? Mabwana
 
Back
Top Bottom