Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli kabisa..Wala hata sio aibu kuufuta huu mkataba.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya jambo hili la bandari na mswada wa cyber unaouzungumzia.
Wewe huoni nchi nzima inazizima wakati huu?
Mswada lilikuwa ni jambo letu wenyewe ndani ya nchi; na kukiwa na tatizo wakati wowote, hiyo sheria ya cyber inaweza rekebishwa bila kikwazo.
Kwenye hili la Dubai, ni kama tunapambania uhuru wetu kwa mara ya pili!
Sasa basi, kama hao wahusika watadharau na kuendelea na hili kama lilivyo, kama unavyosema wewe, waTanzania watakuwa na haki ya kuwachukulia hatua.
Hawa ni watu tu, wasikutishe, wapo hapo walipo kwa ridhaa ya wananchi wenyewe.
Kwa vile hujawahi kuona waTanzania wakiwatia adabu viongozi korofi, usidhani haitatokea. Hawa wanaweza kuwa mfano maalum.
Pumbavu, shenz typeMh.Rais SSH hakika ni MWANADEMOKRASIA.....
Kinyume na hayo wala tusingeona "kelele" nyingi za ukosoaji ambao mwingine unavuka misingi ya utu ,heshima na Umoja wetu.....
#SiempreSSH[emoji120]
Baba na mama yako waliokuzaa.....Pumbavu, shenz type
Sasa unadhani wenye akili kama zako milioni moja wakiunga mkono, kisha wajuvi kumi tuu wa sheria na mikataba wakapiga magumashi hayo tutasemaje?Wengi idadi yao wangapi ?!![emoji1787]
Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Ndaki ya Sayansi ya Jamii
Kitivo kikongwe cha chuo kikuu cha UDSM chajadili kwa pamoja na jamii nzima mkataba wa bandari
Ndaki ya Sayansi ya Jamii UDSM pia hujikita katika kuchambua tafakuri zilizopo katika jamii na hili jambo la sakata la mkataba wa bandari linaloifikirisha jamii ya kiTanzania linaangaziwa kwa upana.
Video ndefu hapa juu inawakilisha tafakuri inayotuletea yote ya mjadala mpana na mkubwa uliowaleta washikadau wakiwemo wanazuoni waalimu wahadhiri 9 wa chuo kikuu wakiwemo Dr. Richard Bruno Mbunda, Prof. Issa Shivji, wanafunzi wa UDSM na wananchi wanajamii kupitia mtandao
Uchambuzi wa Profesa Shivji mazito yabainika mkataba wa bandari
Chini ya ndaki ya sayansi ya jamii CoSS College of Social Sciences leo wahadhari na wanafunzi wajadili kwa kina mkataba wa bandari na unaleta madhara gani kwa taifa.
Mchokoza mada Dr. Richard Bruno Mbunda pamoja na wahadhiri na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDSM na mgeni mwalika profesa Issa Shivji wamejadili kwa kina mada ya mkataba wa bandari ambao imekuwa habari kuu isiyozimika katika vijiwe na mitandao ya kijamii.
Dr. Richard Mbunda anasema kuwa pamoja na Ofisi ya Katibu wa Bunge kuwa ni mshauri mkuu wa bunge lakini pia secretariat ya bunge kuonesha kwa mapendekezo mapungufu ya mkataba lakini kamati ya bunge husika, waziri na bunge zima liliamua kutoyatilia maanani maangalizo muhimu ya secretariat ya Bunge kuhusu mkataba huu usioupa haki ya sovereignty Tanzania
Ila leo ndaki hiyo ya chuo kikuu cha Dar es Salaam imeamua kurudia enzi ambazo chuo kikuu hicho kongwe kilikuwa hakiko nyuma kuandaa mihadhara ya kuchambua mambo mazito yanayoendelea katika jamii .
Profesa Issa Shivji ameamua kujikita zaidi katika mguso huo wa mkataba una maana gani hasa pia unatuletea nini mezani na kumuachi Dr. Richard Bruno Mbunda akijikita kisheria zaidi una mazuri na mapungufu gani.
Profesa Issa Shivji anasema mkataba huu ni treaty yaani mkataba baina ya nchi na nchi na nchi hiyo ni Tanzania na nchi nyingine ambayo ni ngumu kusema kama ni nchi au la.
Ila kuna jambo ambalo limejitokeza katika hilo maana katika treaty lazima kuwepo nipe na nikupe baina ya wawili katika mkataba. Hilo halipo bali haki zote amepewa Dubai huku wajibu wote amepewa Tanzania bila haki. Yaani mkataba umekuwa uwekezaji ingawa unaitwa ni mashirikiano.
Ila ushirikiano huo si wa kijumla bali ni wa bandari na mwekezaji ametajwa ni DP World siyo wawekezaji wa kijumla wa kuhesabika kwa namba makampuni au wafanyabiashara kutoka Dubai.
Jingine ni kuwa DP World inamilikiwa na serikali yaani ni state company. Maana yake kampuni ya serikali inaweza kuleta mgongano wa kidiplomasia tofauti kama ingekuwa kampuni ya binafsi kwani kampuni binafsi huwa haiwezi kuleta mgogoro wa kidiplomasia maana mambo yote yangeishia mahakamani ila kwa kampuni inayomilikiwa na serikali ni tofauti.
Hii ina maana 80% matayarisho shughuli na mapendekezo ya mradi (early project activities) huu mradi wa serikali ya Dubai kupitia DP World na serikali ya Tanzania yalikuwa yameshaandaliwa hata kabla ya mkataba uliopitishwa na azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano tarehe 10 June 2023 mjini Dodoma.
Hii ina maana mikono ilishafungwa na mkataba hata kabla ya IGA ya Dodoma na hiyo mikataba mingine midogo midogo imeshamalizwa kabla ya HGA . Host Government Government Agreements inayotajwa kuwa itafuatia.
Mfano suala la ardhi kwa sheria za Tanzania rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katiba yetu inasema ni mdhamini / mwangalizi wa ardhi yote ili ndani ya mipaka ya nchi na kuwa mtanzania au mwekezaji akipewa umiliki wa miaka 33 au 66 au 99 Rais ana mamlaka ya kuichukua akiona inafaa kutumika kwa manufaa mapana ya jamii na nchi.
Lakini kwa mkataba wetu na DP World, hili la rais wa Tanzania ni mdhamini / mmiliki wa ardhi yote ya Tanzania amevuliwa mamlaka hayo na ameshanganganywa mamlaka hayo na mkataba huu wa aina yake wa bandari. Maana mkataba na Dubai unasema kuhusu ardhi upo bayana neno la kiingereza incumbrace (in property law) kuwa hakutakuwa na kikwazo chochote ...
Bandari ya Dar es Salaam haijathaminisha ili ijulikane serikali yetu imeshawekeza trilioni ngapi kabla DP World haijaingia mkataba. Hakuna mpango maalum wa kuelezea mapato yatagawanywa vipi baina ya Tanzania na DP World kutokana na mradi huu wa bandari.
Ajira za upande wetu zitakuwa za kada ya makuli ndiyo wataajiriwa pengine na wachache kwenye HR yaani utumishi lakini wataalamu wote watatoka nje. Kuhusu kazi za ndogo ndogo za kandarasi ku supply vitu kwa DP World itatolewa kuna masharti, vigezo na kanuni kibao ambazo wafanyabiashara wa Tanzania watashindwa kutimiza mfano standards, competitive market prices za kimataifa n.k Nani atakuwa mdhibiti kuhakikisha tenda ndogo kampuni za kitanzania zitawe kushinda kuuzia DP World vifaa, vipuri n.k mhadhara huu wa ndaki ya sayansi ya jamii CoSS unakuna vichwa wakiangalia mbele.
Muhadhara huu wa CoSS ndaki ya Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaenda mbali na kuona nini kifanyike maana mkataba huu ni mgumu kunufaisha taifa hata ukifanyiwa marekebisho kupitia hatua za HGA host government agreement.
Muhadhara wa huu CoSS pia uliunganisha jamii nje ya chuo wachangiaji mada na maswali kupitia mtandaoni live na kuona yafuatayo yafanyike .
Bunge liamue kukataa azimio lake lenyewe la tarehe 10 June 2023 kuhusu mkataba huu. Bunge lina mamlaka hayo na haliwezi kuhojiwa na DP World wala jumuiya ya kimataifa. Maana Bunge linachanguliwa na wananchi wa Tanzania na pale wananchi wanapokataa mkataba huu baada ya kusikilizwa, wabunge ni wajibu wao kuandaa azimio lingine linalozingatia maoni ya wananchi kuwa wameukataa mkataba / makubaliano haya.
Muhadhara unafahamishwa kuwa nchi kadhaa zimeweza kuvunja mikataba ya aina hii na haikuonekana ni ajabu na kutolea mifano Ecuador ilifuta mikataba 26, nchi ya Bolivia ikaondoa mikataba 17 huku South Africa nayo mikataba 20 iliondolewa wakati India nayo ilifuata mikataba 58.
Hivyo serikali na kikao cha bunge lake baada ya Azimio la Bunge kupitisha mkataba wa bandari kutoa kauli ya unyenyekevu ipo sikivu na kuahidi kusikiliza kelele pia maoni ya wananchi wake pamoja na maoni ya washikadau kama wataalamu wa sheria, wahadhiri wa vyuo vikuu, vyama vya siasa n.k
Mhadhara wa watu-huru kupitia tafakuri ya kina unafikiri ni wakati sahihi wa Bunge kuitisha kikao cha dharura kukaa na kufuta azimio lake la tarehe 10 Juni 2023 na bunge kuishauri serikali kuanza mchakato mpya kumpata mwekezaji mwenye masharti ya manufaa hata kama katika mchakato huo mpya wa wazi shindani atakuwemo DP World na wengine ambao watashindanishwa ...
Kheeeeh wee mbna huu mziki mnene, na sherehe ni ndogo.Hatuna pesa ya kumlipa dp world kuuvunja mkataba huu itabidi uwalipe faida yote itakayo patikana mbeleni muda usio na kikomo
Tayari Rais na waziri wake walishausaini kabla ya kupelekwa bungeni hapo Kuuvunja huo mkataba ni lazima wabunge warudi bungeni wapige kura ya kumkataa rais je itawezekana? Na hilo ndio maana wamelikwepa
Waliosaini mkataba huu walikuwa na nia ovu kabisa kwa taifa hili
Kwa kweli bora waukatae na wauachee tyuuuh, hakuna namna ingine hapa.Ndio pendekezo lilitolewa hapo km umesoma vizuri, na sio jambo la ajabu. Ecuador, India. S.A, na Bolivia walishavunja makubaliano/ mikataba kama hii hata baada ya kupitisha mwanzoni
Arab Contractors wanakuja kujenga bwawa na kuondoka. Hawapewi walijenge na kuliendesha tena kwa muda usiofahamika. Kama una akili unapaswa kuujua ukweli huo.Hoja ya DP WORLD kumilikiwa na serikali ya UAE ni ya kushangaza sana.....
Hebu angalia hili ....
Arab Contractors ni kampuni binafsi lakini tulimuona Rais wa Misri mh.El Sisi akituma ujumbe mzito kuja na hao Arab Contracts kuingia mkataba nasi wa Trilioni 6.5 kujenga bwawa la kufua umeme Mwalimu Nyerere....
Hoja ni hii....
Haya makampuni pamoja na kuwa ni ya kibinafsi ila yana "affiliation" sana na maslahi ya SERIKALI na madola yao......unaweza kutoigopa ARAB CONTRACTORS isiyo na "mafungamano" na serikali ya Misri na kuiogopa DP WORLD waliodhihirisha mafungano na serikali yao na kubaki binafsi "kujichezesha mchezo wa kadenge"[emoji1787]
Dunia imebadilika TUSIKARIRI TU....
Kule Urusi , OLIGARCHY walianzisha makampuni binafsi kwa "fedha ya hazina ya nchi ".....
#ChifuHangayaAnaupigaMwingi[emoji2956]
#SiempreJMT[emoji120]
Bwawa la Nyerere ni watu wajinga tu wangewe kuunga mkono. 2014 tulikuwa tunaimbishwa umeme wa gas kama watoto wadogo na serikali hii hii ya CCM. Tukaambiwa matatizo ya umeme ni mabadiliko ya tabia nchi. Na huu ndio ukweli kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.Ujenzi wa BWAWA la ufuaji umeme MWALIMU NYERERE ulipingwa na akina ndg.Tundu Lissu kwa kuwashirikisha CDU na "lobbying" zao pale BUNDESTAG kwa kigezo cha uharibu wa mazingira ya turathi ya dunia pale Selous....na pia matumizi mabovu ya fedha za umma TRILIONI 6.5...ila hayati JPM akafanikiwa kuutekeleza[emoji120]
Hakuna litakaloanzishwa likakosa WAPINGAJI.
#SiempreSSH[emoji120]
Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Ndaki ya Sayansi ya Jamii
Kitivo kikongwe cha chuo kikuu cha UDSM chajadili kwa pamoja na jamii nzima mkataba wa bandari
Ndaki ya Sayansi ya Jamii UDSM pia hujikita katika kuchambua tafakuri zilizopo katika jamii na hili jambo la sakata la mkataba wa bandari linaloifikirisha jamii ya kiTanzania linaangaziwa kwa upana.
Video ndefu hapa juu inawakilisha tafakuri inayotuletea yote ya mjadala mpana na mkubwa uliowaleta washikadau wakiwemo wanazuoni waalimu wahadhiri 9 wa chuo kikuu wakiwemo Dr. Richard Bruno Mbunda, Prof. Issa Shivji, wanafunzi wa UDSM na wananchi wanajamii kupitia mtandao
Uchambuzi wa Profesa Shivji mazito yabainika mkataba wa bandari
Chini ya ndaki ya sayansi ya jamii CoSS College of Social Sciences leo wahadhari na wanafunzi wajadili kwa kina mkataba wa bandari na unaleta madhara gani kwa taifa.
Mchokoza mada Dr. Richard Bruno Mbunda pamoja na wahadhiri na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDSM na mgeni mwalika profesa Issa Shivji wamejadili kwa kina mada ya mkataba wa bandari ambao imekuwa habari kuu isiyozimika katika vijiwe na mitandao ya kijamii.
Dr. Richard Mbunda anasema kuwa pamoja na Ofisi ya Katibu wa Bunge kuwa ni mshauri mkuu wa bunge lakini pia secretariat ya bunge kuonesha kwa mapendekezo mapungufu ya mkataba lakini kamati ya bunge husika, waziri na bunge zima liliamua kutoyatilia maanani maangalizo muhimu ya secretariat ya Bunge kuhusu mkataba huu usioupa haki ya sovereignty Tanzania
Ila leo ndaki hiyo ya chuo kikuu cha Dar es Salaam imeamua kurudia enzi ambazo chuo kikuu hicho kongwe kilikuwa hakiko nyuma kuandaa mihadhara ya kuchambua mambo mazito yanayoendelea katika jamii .
Profesa Issa Shivji ameamua kujikita zaidi katika mguso huo wa mkataba una maana gani hasa pia unatuletea nini mezani na kumuachi Dr. Richard Bruno Mbunda akijikita kisheria zaidi una mazuri na mapungufu gani.
Profesa Issa Shivji anasema mkataba huu ni treaty yaani mkataba baina ya nchi na nchi na nchi hiyo ni Tanzania na nchi nyingine ambayo ni ngumu kusema kama ni nchi au la.
Ila kuna jambo ambalo limejitokeza katika hilo maana katika treaty lazima kuwepo nipe na nikupe baina ya wawili katika mkataba. Hilo halipo bali haki zote amepewa Dubai huku wajibu wote amepewa Tanzania bila haki. Yaani mkataba umekuwa uwekezaji ingawa unaitwa ni mashirikiano.
Ila ushirikiano huo si wa kijumla bali ni wa bandari na mwekezaji ametajwa ni DP World siyo wawekezaji wa kijumla wa kuhesabika kwa namba makampuni au wafanyabiashara kutoka Dubai.
Jingine ni kuwa DP World inamilikiwa na serikali yaani ni state company. Maana yake kampuni ya serikali inaweza kuleta mgongano wa kidiplomasia tofauti kama ingekuwa kampuni ya binafsi kwani kampuni binafsi huwa haiwezi kuleta mgogoro wa kidiplomasia maana mambo yote yangeishia mahakamani ila kwa kampuni inayomilikiwa na serikali ni tofauti.
Hii ina maana 80% matayarisho shughuli na mapendekezo ya mradi (early project activities) huu mradi wa serikali ya Dubai kupitia DP World na serikali ya Tanzania yalikuwa yameshaandaliwa hata kabla ya mkataba uliopitishwa na azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano tarehe 10 June 2023 mjini Dodoma.
Hii ina maana mikono ilishafungwa na mkataba hata kabla ya IGA ya Dodoma na hiyo mikataba mingine midogo midogo imeshamalizwa kabla ya HGA . Host Government Government Agreements inayotajwa kuwa itafuatia.
Mfano suala la ardhi kwa sheria za Tanzania rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katiba yetu inasema ni mdhamini / mwangalizi wa ardhi yote ili ndani ya mipaka ya nchi na kuwa mtanzania au mwekezaji akipewa umiliki wa miaka 33 au 66 au 99 Rais ana mamlaka ya kuichukua akiona inafaa kutumika kwa manufaa mapana ya jamii na nchi.
Lakini kwa mkataba wetu na DP World, hili la rais wa Tanzania ni mdhamini / mmiliki wa ardhi yote ya Tanzania amevuliwa mamlaka hayo na ameshanganganywa mamlaka hayo na mkataba huu wa aina yake wa bandari. Maana mkataba na Dubai unasema kuhusu ardhi upo bayana neno la kiingereza incumbrace (in property law) kuwa hakutakuwa na kikwazo chochote ...
Bandari ya Dar es Salaam haijathaminisha ili ijulikane serikali yetu imeshawekeza trilioni ngapi kabla DP World haijaingia mkataba. Hakuna mpango maalum wa kuelezea mapato yatagawanywa vipi baina ya Tanzania na DP World kutokana na mradi huu wa bandari.
Ajira za upande wetu zitakuwa za kada ya makuli ndiyo wataajiriwa pengine na wachache kwenye HR yaani utumishi lakini wataalamu wote watatoka nje. Kuhusu kazi za ndogo ndogo za kandarasi ku supply vitu kwa DP World itatolewa kuna masharti, vigezo na kanuni kibao ambazo wafanyabiashara wa Tanzania watashindwa kutimiza mfano standards, competitive market prices za kimataifa n.k Nani atakuwa mdhibiti kuhakikisha tenda ndogo kampuni za kitanzania zitawe kushinda kuuzia DP World vifaa, vipuri n.k mhadhara huu wa ndaki ya sayansi ya jamii CoSS unakuna vichwa wakiangalia mbele.
Muhadhara huu wa CoSS ndaki ya Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaenda mbali na kuona nini kifanyike maana mkataba huu ni mgumu kunufaisha taifa hata ukifanyiwa marekebisho kupitia hatua za HGA host government agreement.
Muhadhara wa huu CoSS pia uliunganisha jamii nje ya chuo wachangiaji mada na maswali kupitia mtandaoni live na kuona yafuatayo yafanyike .
Bunge liamue kukataa azimio lake lenyewe la tarehe 10 June 2023 kuhusu mkataba huu. Bunge lina mamlaka hayo na haliwezi kuhojiwa na DP World wala jumuiya ya kimataifa. Maana Bunge linachanguliwa na wananchi wa Tanzania na pale wananchi wanapokataa mkataba huu baada ya kusikilizwa, wabunge ni wajibu wao kuandaa azimio lingine linalozingatia maoni ya wananchi kuwa wameukataa mkataba / makubaliano haya.
Muhadhara unafahamishwa kuwa nchi kadhaa zimeweza kuvunja mikataba ya aina hii na haikuonekana ni ajab9u na kutolea mifano Ecuador ilifuta mikataba 26, nchi ya Bolivia ikaondoa mikataba 17 huku South Africa nayo mikataba 20 iliondolewa wakati India nayo ilifuata mikataba 58.
Hivyo serikali na kikao cha bunge lake baada ya Azimio la Bunge kupitisha mkataba wa bandari kutoa kauli ya unyenyekevu ipo sikivu na kuahidi kusikiliza kelele pia maoni ya wananchi wake pamoja na maoni ya washikadau kama wataalamu wa sheria, wahadhiri wa vyuo vikuu, vyama vya siasa n.k
Mhadhara wa watu-huru kupitia tafakuri ya kina unafikiri ni wakati sahihi wa Bunge kuitisha kikao cha dharura kukaa na kufuta azimio lake la tarehe 10 Juni 2023 na bunge kuishauri serikali kuanza mchakato mpya kumpata mwekezaji mwenye masharti ya manufaa hata kama katika mchakato huo mpya wa wazi shindani atakuwemo DP World na wengine ambao watashindanishwa ...
Aiseeh kama kweli hili lipo walio kubali huu mkataba ni Sawa na kufanya uhainEneo ambalo sio la DP WORLD lakini ni karibu na eneo la DP WORLD, mtu akitaka kujenga barabara au flyover ambayo interfere (itaingilia) shughuli za DP WORLD hairuhusiwi kwa mujibu wa mkataba huu (wa uendelezaji wa bandari). Serikali itahakikisha kwamba shughuli hizo hazitokuwepo kando kando na eneo la DP WORLD" Prof. @IssaShivjiView attachment 2672497
Sent using Jamii Forums mobile app
Swali fikirishi je bunge la CCM likotayari kuukataa mkataba wa DPWORLD?
Wewe ni mwehu.Ujenzi wa BWAWA la ufuaji umeme MWALIMU NYERERE ulipingwa na akina ndg.Tundu Lissu kwa kuwashirikisha CDU na "lobbying" zao pale BUNDESTAG kwa kigezo cha uharibu wa mazingira ya turathi ya dunia pale Selous....na pia matumizi mabovu ya fedha za umma TRILIONI 6.5...ila hayati JPM akafanikiwa kuutekeleza[emoji120]