KERO Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) tunaomba kutatuliwa changamoto ya matokeo tangu 2020 hatujapata vyeti

KERO Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) tunaomba kutatuliwa changamoto ya matokeo tangu 2020 hatujapata vyeti

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Takriban wahitimu 20 wa chuo kikuu Cha Dodoma (UDOM) kitivo Cha Elimu tuliohitimu mwaka wa masomo 2019-2020 hatujapatiwa vyeti vya kuhitimu

Tumefatilia wanasema changamoto ni matokeo ya mwaka wa kwanza yaani 2017-2018 kuwa baadhi yetu walipata incomplete baadhi ya masomo na we gine Carry, but kiuhalisia matokeo yalikuwa mazuri na hayakuwa na hiyo changamoto ndio maana tuliweza kuendelea na mwaka wa pili hadi kumaliza mwaka wa tatu

Maana kwamba kutokana na Sheria na taratibu za chuo, kama mtu alipata incomplete means ame discontinue na haendelei na mwaka unaofatia lakini kwetu haikuwa hivyo na SR kipindi hicho ilionesha tumefaulu ndio maana tukaendelea na mwaka wa pili

Huu sasa ni mwaka wa nne tangu kumaliza chuo na hatujui hatima yetu

Mwaka huu mwezi wa 2 walituambia matokeo ya semister ya kwaza kwa hawa waliopo chuoni yakitoka watatatua na hiyo changamoto lakini hadi leo hakuna kilichotatuliwa maana nilienda wakaangalia wakasema bado shida ni Ile Ile

Sasa hivi nafasi za ajira zilizotangazwa siwezi kuomba sababu sina vyeti, lakini pia familia inaona ninaidanganya labda nilifeli Ila sitaki kusema ukweli

Kingine nilisomeshwa na loan board na Nina deni, Ila mpaka sasa sijui nalipa vipi kama tu cheti cha taaluma sijapata mwaka wa nne sasa

Nakuomba nisaidiwe hili kuli address ili lipatiwe ufumbuzi maana JamiiForums imekuwa msaada na mkombozi wetu katika changamoto nyingi

Asantee

Majibu ya UDOM ~ UDOM: Wanaodai hawajapata vyetu tangu 2020 waje watuone, inawezekana system imewasana labda walifanya udanganyifu
 
Daa kwani wenyewe UDOM wanasema tatizo ni nini. Isijekuwa nyie ndio wenye tatizo, au wanawaambia tu msubiri.
 
Aisee poleni sana.
Hivi vyuo sijui ni kubadili taratibu gafla au ni shida gani.

Nina ndugu yangu nae amesimamishwa mpaka mwakani. Yeye ni mwaka wa tatu ilikua apige pepa amalize ila bahati mbaya alikua na carry ya somo moja.
Mwanzo kabisa ile Nov mwaka jana aliambiwa alipe ada ya mwaka wa tatu aendelee kusoma hiyo carry ataifanya semister ya pili na pia atafanya na UE ya kumaliza mwaka.

Kalipa ada freshi kabisa, kapiga tests za semister ya kwanza fresh, kapiga UE na jina lake linaappear kama mwaka wa tatu anaestahili kumaliza.

Imefika UE semister ya pili siku moja kabla ya kuanza pepa anaambiwa haruhusiwi kufanya mpaka afanye ile carry kwanza then Nov ndo aanze tena mwaka wa tatu.
Kuuliza mbona mliruhusu mpaka nafanya tests za Semister ya kwanza na ya pili na UE ya semister ya kwanza, hawana jibu ati taratibu ndivyo zilivyo na wao wanafata order tu.

Vyuo vijaribu kutoa taarifa za mabadiliko mara kwa mara, wanavyuo wengi mno hawajui hata ufaulu ukoje. Hawajui akipata carry au sup iko vipi.
Mpaka liwakute jambo ndo anazijua korido zote na kupotezeana muda kwingi.
 
Alivyoenda chuo wakamwambia 'bado shida ni ileile" maana yake kuna msimamo fulani chuo wameshikilia dhidi yao ndio sijaelewa hapo.
4yrs na kila mwaka wanatoa vyeti iweje kwenye hiyo ishu yao

Wabongo tuna safari ndefu ya kupenda kusoma

Para ya pili tu kwenye maelezo yake imetosha kuelezea hiyo shida unayodai huelewi
 
Wabongo tuna safari ndefu ya kupenda kusoma

Para ya pili tu kwenye maelezo yake imetosha kuelezea hiyo shida unayodai huelewi
Oky bhana wewe msomi unaeona hayo maelezo hayana mkanganyiko mahali
 
Daa kwani wenyewe UDOM wanasema tatizo ni nini. Isijekuwa nyie ndio wenye tatizo, au wanawaambia tu msubiri.
Changamoto wanasema ni mfumo, kila siku ni kuzungusha na hakuna wanachotatua na mbaya zaidi unakuta unasafiri mkoani unafatilia hiyo ishu kwa gharama kubwa lakini hakuna msaada
 
Unao ushahidi wa matokeo ya huo mwaka wa kwanza??
Ukishamaliza chuo huwa huwezi ku access SR, lakini ushahidi ni hayo matokeo ya miaka mingine yapo na wakiingia wao wenyewe kwenye mfumo wanayakuta matokeo ya miaka ya mbele Ila mwaka wa kwanza wanasema ndio Kuna hizo changamoto na Wana admit kuwa ni shida yao ndio maana kila Leo wanasema wanashughulikia lakini miaka inazidi kupita tu
 
Mdogo wangu matokeo ya Test ya somo moja hakuwekewa kwenye mfumo na Mwalimu ambaye inasemekana kuwa alikuwa anauza vitabu vya 4,000 kwa 10,000 sasa wanafunzi wakaona isiwe shida wakaenda Kununua kwenye maduka ya Dodoma Mjini kumbe si ikawa nongwa! Zaidi ya Wanafunzi 20 hawajafanya mtihani wa mwisho wa somo lake mpaka mwakani kwa sababu hiyo.

Aliingiza matokeo ya baadhi ya wanafunzi, wengine amewarudisha Makusudi chuo mwakani kwa ajili ya Test na kumalizia Mtihani wa Somo lake.

UDOM kuna shida sana, ukiona Mwanao ametoka bila shida yoyote Shukuru Mungu
 
Yani ndugu yangu kamaliza UDOM 2014 lakini alipata mchongo akaenda nje ya nchi kabla ya kuchukua cheti chake. Sasa leo anafatilia cheti anaambiwa kuwa ana deni.

Cha ajabu receipt zote za malipo anazo na wala hakuwa na mkopo, ila wahasibu wanamkomalia alipe deni ndo apewe cheti.

Udom ni chuo cha hovyo sana, hakuna kitu kinachoonekana kinafanyika kwa ukamilifu pale. Inakuwaje mtu aliyefanya clearance na receipt zote anazo afu leo awe na deni! Yani walimfanyia clearance huku akiwa na deni?!
 
Back
Top Bottom